Serikali: Wanafunzi waliopata mimba kuendelea na Masomo katika mfumo rasmi

hangaya itabidi ajenge wodi la wazazi kila shule, asijenge tu madarasa....
 
Akidungwa mimba atafukuzwa kwao aende kwa aliyemdunga ili washirikiane kulea mimba,kifupi ataolewa.akijifungua atakuwa anakwenda shule akitokea kwa mmewe.Shule itampokea kwa waraka wa serkali.Kifupi shule itakuwa ikisomesha wake za watu walioolewa.
 
Aliyepata ujauzito ni mtoto. Yafuatayo ni changamoto zisizo na majibu kutoka kwa aliyetoa amri hiyo:
  • Kama ni wa familia maskini unakuwa mzigo kwa hiyo familia kumtunza mtoto wao na kijukuu;
  • Mzazi ni mtoto ambaye hajawa tayari kuwa mzazi;
  • Hatari kiafya mimba ya utotoni;
  • Uwezo wa kumudu masomo na kulea mtoto; nk
 
Kweli hakuna mkate mgumu mbele ya chai
 
Binafsi naunga mkono hoja kwamba aendelee na masomo, nimezunguka sana hii Tanzania nimeona ni kwa jinsi gani umaskini unachangia hizo mimba za utotoni, sasa kumnyima huyo mzazi elimu kutazidi kuchangia umaskini maana huenda mzazi asione umuhimu wa elimu kiasi asijali hata kumpatia huyo mtoto wale elimu.
Lakini waswahili tuna misemo yetu kwamba, KOSA LA KWANZA SIO KOSA BALI KURUDIA KOSA, tuwasomesheni jamani kuna faida huko mbele.
 
Sawia kaka, sisi mambo mengi hatuyawezi inabid tujifunze kwa walioendelea
Kwa ufuatuliaji wangu mdogo nimeona jinsi ambayo wenzetu wanaongea na watoto wao kwa uwazi, kuanzia wavulana mpaka wasichana, nimeshuhudia mimi binti aliyebakwa lakini hakutoa taarifa kwao mpaka mwalimu wake aloposhtuka kwamba huyo mtoto hayuko salama, suala likaenda Polisi mzazi anaambiwa hajui hata kinachoendelea.
 
Tungekuwa tunaongelea sana neno la kumzuia na kumlinda mtoto mjamzito kupata mimba akiwa shule ingesaidia sana kuliko kuendelea na mtoto mjamzito kuendelea au kutoendelea na shule.....kujadili hivi ni kukubaliana na tatizo..

Tutapambane zaidi na mbinu za kumlinda mtoto wa kike awe salama na ikiwezekana na wa kiume awe salama pia...

Ikigundulika binti kaingiliwa na mtu mzima hata bila kupewa mimba basi mhusika atiwe mbaroni akatumikie 30yrs....ikigundulika mchezo huu wanafanya wenyewe kwa wenyewe watoto walio shule basi wazazi waitwe watoto wahamishwe shule tofauti tofauti na adhabu kali, ikiwa pamoja na wazazi wote kuilipa faini serikali..Ulinzi huu uendane sambamba na ulinzi wa maadili ya jamii nzima...
 
Wananchi tuanze sasa kuwafungulia kesi za kuwadai fidia wasanii wa Bongo fleva na wacheza filamu dhidi ya nyimbo za matusi zinavyoharibu jamii...fidia hizo walipe ustawi wa jamii angalau kutibu majeraha na manyimbo yap yapigwe marufuku pamoja na wasanii kupigwa life ban..

Hizi nyimbo na filamu zimechangia sana watoto kuwaza kufanyana kuliko kufanya mambo ya msingi...
 
Kusoma ni wajibu, no matter what happened.

Huku kwetu Katumbasongwe na Mpunguti, unaweza kukuta kabinti kanakataa kurudi masomoni pamoja na serikali kutoa hiyo fursa, bado hawa vijana wanahitaji psychological n financial support zaidi ya hiyo ya kurudi shule.
 
Na akiwa na mimba aendelee tu kwenda shule hadi siku za kujifungua apate likizo ya uzazi!
Hilo linazungumzika. Inawezekana kuwa atarudi shule baada ya mwaka au mwaka mmoja na nusu n.k. Hayo yote ni maswala ya taratibu tu, kikubwa huo mlango wa uwezekano wa kurudi shule uwe wazi na ni suala la familia kujipanga juu ya kachanga katatunzwa vipi.

Ninawafahamu wasichana wengi waliopata uja mzito wakiwa shuleni, baadae kwa mbinu tofauti ama kujificha na mbinu nyinginezo na baada ya kujifungua wakarudi shule na kuendelea na kufanya vizuri sana katika masomo. Kuna watatu nawafahamu, mmoja leo hii ni Daktari, mwingine ni mwalimu wa sekondari na watatu ni mhasibu. Si wamejikomboa kiuchumi hawa!

Wakati umefika kwa wale wasichana waliojigungua shule na baadae wakasoma na kufanya vizuri, wajitokeze na wawe mabalozi kwa wasichana wenzio na kwa serikali kwa ujumla. Kwani kuna wengi hatuelewi impact ya tatizo hilo kiuchumi kwa mwanamke.
 
Ongezeni pia kuunga mkono mapenzi shuleni. Halafu then mwanzishe thread zingine za kulalamikia mfumo wetu wa elimu, kiwango duni cha taaluma na ufanisi wa Madokta na Maprofesa wetu. Mnapalilia mizizi wenyewe, then mlalamikia aina ya majani ya matunda yanayopatikana kwenye mti wenu wenyewe!??? Shame on you mara ^tar-two!!!^ There are things in life ambazo hazihitaji negotiations za kipuuzi kama hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…