Serikali: Watanzania waliopo Israel na Iran kurejeshwa nchini

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
HALI YA WATANZANIA NCHINI ISRAEL NA IRAN KUFUATIA MASHAMBULIZI BAINA YA TAIFA LA ISRAEL NA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN

DODOMA, 19 JUNI 2025​

Kufuatia mashambulizi yanayoendelea kati ya Taifa la Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyoanza tarehe 13 Juni 2025, hali ya usalama katika mataifa hayo imeendelea kuwa tete. Mgogoro huu umesababisha mataifa mbalimbali kuchukua hatua za dharura kuwaondoa raia wao waliopo katika maeneo hayo ya hatari.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa Watanzania waliopo nchini Israel na Iran wapo salama. Aidha, hatua za haraka za kiutendaji zimeanza kuchukuliwa ili kuhakikisha raia hao wanarejeshwa nyumbani salama.

Kupitia Balozi zake zilizopo katika nchi za Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (ambao unaiwakilisha Tanzania nchini Iran), Kuwait na Israel, Serikali inaendelea na juhudi za kuwaorodhesha Watanzania waliopo katika nchi hizo.

Taarifa zilizopo hadi sasa zinaonesha kuwa kuna Watanzania 168 waliopo nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran. Kwa upande wa Israel, inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya Watanzania 200 wakiwemo watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, wanafunzi, na wafanyakazi katika taasisi mbalimbali. Kati yao, Watanzania 50 tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kurejea nyumbani.

Pamoja na changamoto za kiusalama zilizopo, Serikali inathibitisha kuwa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Israel halijaathirika na mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran.

Wakati mashambulizi hayo yalipotokea, hapakuwa na mtu yeyote ndani ya jengo hilo, na maafisa wa ubalozi pamoja na familia zao wote wapo salama.

Aidha, Balozi zetu nchini Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) zimekuwa zikiwasiliana na Watanzania waliopo katika maeneo ya Iran na Israel, zikiwataka kuchukua tahadhari za kiusalama, wakati Serikali ikiendelea kushughulikia masuala yanayohusu usalama wao ikiwa ni pamoja na mustakabali wao wa kurudi nyumbani.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wa ndani na nje ya nchi, inaendelea na taratibu za kiutendaji ili kuhakikisha Watanzania waliopo katika maeneo hayo hatarishi wanarejeshwa nyumbani salama.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO NA AFRIKA MASHARIKI​


 
Waburushi
 
USA yuko na Israel ilhali Mrusi yuko na Iran

Je, hatuelekei kwenye vita ya dunia?

Jumaa karim!
 
Wizara ya mambo ya nje imewahakikishia Watanzania kuwa raia wake waliopo Israel na Iran wapo salama licha ya mashambulizi yanayoendelea kati ya mataifa hayo tangu Juni 13, 2025, Hatua za haraka zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha wanarejeshwa nyumbani salama kupitia balozi zilizopo Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Kuwait
Taratibu za kiutendaji zinaendelea kwa ushirikiano wa wadau wa ndani na nje kuhakikisha wote wanarejea nyumbani kwa usalama.



 
Walioko Iran wabakie humo ni kutokea visiwa pendwa
 
USA yuko na Israel ilhali Mrusi yuko na Iran

Je, hatuelekei kwenye vita ya dunia?

Jumaa karim!
Nadhani stage dunia ilipofika vita ya dunia ni ngumu sana...kutakuwa na ubabe tu wa mwenye nguvu kumuonea mnyonge...mataifa makubwa karibu yote yana silaha za nuclear. Hakuna wa kumtisha mwenzake. Tumebaki sisi manyani tu ndiyo wa kutishwa.
 
Ikifika zamu ya waliopo Canada jamani mnikumbushe kuna kibibi kimezamia huko mwaka wa ishirini huu hakitaki kurudi kutwa kutupiga porojo humu
 
Hali ya Watanzania Nchini Israel na Iran Kufuatia Mashambulizi Baina ya Taifa la Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

TAARIFA KWA UMMA

HALI YA WATANZANIA NCHINI ISRAEL NA IRAN KUFUATIA MASHAMBULIZI BAINA YA TAIFA LA ISRAEL NA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN

DODOMA, 19 JUNI 2025

Kufuatia mashambulizi yanayoendelea kati ya Taifa la Israel na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyoanza tarehe 13 Juni 2025, hali ya usalama katika mataifa hayo imeendelea kuwa tete. Mgogoro huu umesababisha mataifa mbalimbali kuchukua hatua za dharura kuwaondoa raia wao waliopo katika maeneo hayo ya hatari.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa Watanzania waliopo nchini Israel na Iran wapo salama. Aidha, hatua za haraka za kiutendaji zimeanza kuchukuliwa ili kuhakikisha raia hao wanarejeshwa nyumbani salama.

Kupitia Balozi zake zilizopo katika nchi za Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (ambao unaiwakilisha Tanzania nchini Iran), Kuwait na Israel, Serikali inaendelea na juhudi za kuwaorodhesha Watanzania waliopo katika nchi hizo.

Taarifa zilizopo hadi sasa zinaonesha kuwa kuna Watanzania 168 waliopo nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran. Kwa upande wa Israel, inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya Watanzania 200 wakiwemo watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, wanafunzi, na wafanyakazi katika taasisi mbalimbali. Kati yao, Watanzania 50 tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kurejea nyumbani.

Pamoja na changamoto za kiusalama zilizopo, Serikali inathibitisha kuwa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Israel halijaathirika na mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran. Wakati mashambulizi hayo yalipotokea, hapakuwa na mtu yeyote ndani ya jengo hilo, na maafisa wa ubalozi pamoja na familia zao wote wapo salama.

Aidha, Balozi zetu nchini Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) zimekuwa zikiwasiliana na Watanzania waliopo katika maeneo ya Iran na Israel, zikiwataka kuchukua tahadhari za kiusalama, wakati Serikali ikiendelea kushughulikia masuala yanayohusu usalama wao ikiwa ni pamoja na mustakabali wao wa kurudi nyumbani.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wa ndani na nje ya nchi, inaendelea na taratibu za kiutendaji ili kuhakikisha Watanzania waliopo katika maeneo hayo hatarishi wanarejeshwa nyumbani salama.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO NA AFRIKA MASHARIKI

Xmfa_tanzania

foreign.go.tz
 
Waje wabatizwe kuwa machawa wapya!
Uzuri watapewa kadi, baiskeli, kofia, khanga, buku saba, pilau na hata kupakizwa kama wanyama kwenye mafuso!
Karibuni udanganyikani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…