Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 7,225
- 9,830
View: https://youtu.be/8KZulT0i1nk?si=OmucN8PMwbOADTlj
Kwa unyama huu waliotendewa Wanasheria na Wanaharakati toka nchi za jirani zetu Kenya na Uganda kimeharibu kabisa uhusiano wa kidplomasia.
Tujiulize: Kulikuwa na ulazima gani wa kuwakamata, kuwatesa na kuwa dhaliilisha kingono baadhi yao? Mtu ni raia wa nchi nyingine ameingia Tanzania, amekatwa na hatakiwi, kwanini umfanyie unyama?
Hao raia toka Kenya na Uganda wana balozi zao hapa Tanzania. Serikali na mapolisi waliona ugumu gani kutumia balozi zao kuwarudisha nchini kwao badala ya kuwatesa na kuwafhalilisha?
Nakumbuka Marehemu JPM akiwa Waxiri aliwai kwenda Kenya kumpigia kampeni rafiki yake Oginga Odinga. Hakufaniwa vurugu hata chembe!! Leo kuna Watanzania wengi tu wako Kenya na Uganda wanahangaika na kutafuta Maisha kupitia Biashara mbalimbali km. Muziki n.k..
Hivi leo Wakenya na Waganda wakiamua kulipiza visasi kwa Watz walioko huko kitatokea nn?