Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Hii ndo maana sahihi ya Muongoza njia. Hatimaye Serikali ya Ghana imemuiga Mama asiye na maneno mengi bali matendo mengi, asiye na mbwembwe za kujitangaza hovyo na promo za kijinga anayependa vitu kwenda kwa usahihi na kupata matokeo sahihi, Si mwingine ni Rais Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha tozo ya miamala ya simu
Piga kazi Samia. Unayofanya Tanzania sasa yanaanza kuigwa nje. Afrika bila kujitoa Kweli hatuwezi kufika. Hata Ghana tozo zinapingwa na upinzani Ila Serikali wameona ndo njia sahihi.
Lazima tulipe kodi kwa maendeleo yetu!
-===========
Wabunge nchini Ghana wamelazimika kutwangana makonde bungeni baada ya kutokea ubishani wakati wa mjadala juu ya sheria ya tozo ya miamala ya kidigitali.
Ugomvi huo ulianza baada ya Mbunge wa Upinzani kumzuia Msaidizi wa Spika kunyanyuka kwenda kupiga kura. Chama cha Upinzani cha NDC kinapinga mapendekezo ya tozo ya 1.75% kwa miamala ya kidigitali kikidai kuwa tozo hizo zitaathiri watu wa kipato cha chini.
Waziri wa Fedha wa nchi hiyo amesema tozo hizo zitasaidia kuongeza makusanyo ya kodi kufikia cedi bilioni 6.9 (zaidi ya Tsh. trilioni 2.3). Kikao cha bunge kililazimika kuahirishwa baada ya vurugu hizo kutokea.