Serikali ya Iran yafunga kiwanda chake cha kutengeneza magari kilichojengwa Syria miaka 20 iliyopita, sababu za kiuchumi na mahusiano mabaya zatajwa

Mie nina wazee TRC,walinipa fununu kuwa ilikua bado kidogo wajenge Iran,na Iran wako na teknolojia nzuri sana ya reli,ila ubahili wa 10% ukawafanya wakose tenda na kupewa mzabuni Yepi Merkezi.

allah akbar, subhana watallah dah watu wana siri sana kumbe iran ndo ilikuwa ajenge sgr,
 
Kama una ndugu mameneja pale TRC tafuta hizi fununu watakwambia.
Ila ubahili wa kutoa ukawanyima tenda.
Tenda takriban zote huwa anayetangaza zabuni ili akupe Kuna ka percent umpe kama ahsante ya kukuchagua.
Ukigoma umeikosa.
 
Kama una ndugu mameneja pale TRC tafuta hizi fununu watakwambia.
Ila ubahili wa kutoa ukawanyima tenda.
Tenda takriban zote huwa anayetangaza zabuni ili akupe Kuna ka percent umpe kama ahsante ya kukuchagua.
Ukigoma umeikosa.
Kwenye manunuzi % kawaida tena serikalini ndo kabisaa hivyo sijashangaa
 
Iran hawezi kubadili sera kwaajili ya watu wachache kuwalamba miguu mazayuni, hio haitawezekana kwa dunia inaenda kubadilika BRiCS ikipata momentum kuna unafuu mkubwa unakuja hapo mbeleni
Kuna kitabu kimoja tulisoma enzi hizo kikiitwa Ndoto ya Ndaria.
 
Naifahamu historia ya Iran miaka mingi sana kaka; unacho kisema nakijua. Unakumbuka wakati tunafanya mjadara na wewe humu, nilikuonesha I know that country before and after Islamic revolution? Naweza kurudi nyuma even before Christ. Iranian ni intelligent for years. Najua hata chanzo cha mgogoro wao na Israel ni nini? Wengi wanadhani ni DINI, sio dini. Hawa wameanza mgogoro miaka 70 baada ya dola ya Babel( leo Iraqi) kuanguka, before that they were friends wakifanya biashara pamoja and in fact hawa Iran ndio waliowasaidia Israel kurudi kwao baada ya dolla ya Babel kuwateka na kubomoa mji wa Jerusalem na kuteka vijana wenye akili to their country, it was Iran ndio waliwasaidia kurudi home, that time Iran ndio alikua king wa middle east baada ya Babel.
Now kwenye issue ya biashara hi ya magari, kwanza naijua for years hasa baada ya vita vyake na Iraqi kwisha, France ndio alikua wa kwanza kupeleka kiwanda cha Peugeot pale, kwamba walikua wanatengeneza gari kwa technology yao na brand yao, hi ndio sikua naijua BUT again kwasasa kupenya kwenye soko la Toyota bro, ni ngumu sana. Wajeruman pamoja na gari zao kutumiwa na VIPs worldwide but Toyota kawapigisha magot chini, Italy alitamba na gari zake miaka ya 80, nae chali; Uingereza ndio kwaanza kaamua kupeleka Landrover zake India but still Toyota anamchezesha anavyo taka. Ni ngumu sana; I also knows why Iran decided to put some his factories, industries to other countries; VIKWAZO alivowekewa na mataifa ya magharibi. Ingawaje kwenye reli tuweni wakweli tu; nchi yetu tuna uzembe mwingi sana, hi ilikua sio ya kutushinda, sema tunawekeza akili nyingi sana kwenye siasa badala ya production/uchumi. Reli ya Tazara ilitakiwa kutupatia funzo BUT tunakwenda shule sijui hata zinatusaidia nini. Hi linakera. Ndio sasa unaona kinacho endelea Kariakoo. Vifaa ya kuulia watu, kuteka na kutesa tunavyo vya kisasa sana, lakini vifaa na ujuzi wa kuokolea watu HATUNA. Inaudhi
 
Iran hawezi kubadili sera kwaajili ya watu wachache kuwalamba miguu mazayuni, hio haitawezekana kwa dunia inaenda kubadilika BRiCS ikipata momentum kuna unafuu mkubwa unakuja hapo mbeleni
Hakuna nchi inayoweza kufika popote kwa kutengwa na Dunia, na Dunia, hasa mataifa ya Ulaya na America. Hiyo ndiyo Dunia yenye soko kubwa lenye nguvu na imara kuliko regional markets zote za Dunua. Urusi ya kale, USSR, pamoja na ukubwa wa nchi na resources nyingi na tekinolojia, haikufika popote kutokana na kutengwa na masoko hatlya makubwa, na baadaye ilisalimu amri kwa mataifa ya Magharibi, na kuishia kuomba msaada, na ili kupata msaada ikapewa masharti ya kuheshimu uhuru wa watu, iliporidhia, ikawa ndiyo mwisho wa USSR. Leo Urusi imegeuka kuwa adui wa nchi zilizokuwa sehemu ya muungano wa kisovieti.

Iran, hata ifanye nini, kwa kujitenga na Ulimwengu, itaishia kuwatesa raia wake, wakati nchi ilikuwa na potential kubwa ya maendeleo makubwa.

BRICS, bado sana. Uchumi na soko la BRICS bado ni mdogo sana ukilinganisha na ule wa nchi za Magharibi. BRICS mpaka kuweza kuwa na uchumi na soko shindani ni process, siyo tukio la mara moja.
 
Yaan kwamba kwenye hiyo tenda hata kampuni za china zilikuwa chini ya hiyo kampuni ya kiirani? maana mchina kwenye reli yupo vizuri sanaaa sasa najiuliza muiran aliwapitaje wachina kwenye tender analysis? kwa maana ya technical, na financial? Hebu itaje hiyo kampuni ya Iran unayosema
 
Shida sio kujitenga na dunia, shida ni malengo ya hao mabwana zidi ya Iran, nakuhakikishia iran akilegeza mpango ni uleule kama wa Libya ndio lengo la western. Mpaka sasa mafuta ambayo wameshindwa kuyachukua kihuni ni hayo ya Iran. Wao sio wajinga na Iran anatamani kuingia soko huria lakini hofu ya western zidi ya Iran ndio inayomkwamisha
 
FAKE NEWS
 
Iran toka imekuwa na vikwazo ni lini? Je, tanzania isiyo kuwa na vikwazo imeizidi?
Iran, sawa tu na Tanzania, ni nchi ambayo serikali haina ridhaa ya wananchi lakini inaongoza tu kwa sababu inalindwa na dola.

Lakini kwenye nchi ya Iran kungekuwa na mfumo kamili wa kidemokrasia ambapo wananchi ndio wanaamua nani awe kiongozi wao leo hii akina Ayatollah na genge lake wangekuwa hawajulikani kabisa.

Sawa tu na Tanzania kama tungekuwa na mfumo wa uchaguzi ambao wananchi ndio wanaamua nani awe kiongozi hakuna ambao wangemfahamu Samia Suluhu Hassan.
 
Hivyo ndivyo unaaminishwa na propaganda za kimagharibi. Duniani kote, hakuna sehemu ambapo raia wanaikubali serikali wote kwa asilimia mia hata huko marekani tumeona uchaguzi wa juzi hadi trump kashinda tena kwa kishindo bado kuna raia hawataki.
Iran sio kama tanzania kuanzia miundombinu, viwanda, standard of living, influence yani si kama tanzania kwa chochote.
Sisi tuendlee tu kujicompare na uganda, kenya, mali si iran kwa sababu si level zetu kwa chochote.
 
Jina sikutajiwa ila wacha nikawachokonoe wazee wanitajie.
Mkuu zabuni inapotangazwa Kuna mambo mengi ambayo yanatizamwa.
Kama ukizungumzia hayo basi CHINA ndiye angetakiwa achukue tenda na sio Uturuki Yepi Merkezi.
Je Uturuki anamzidi lolote China?
Jibu nooop Uturuki haimzidi China kwa lolote.
Ila mbona zabuni alishinda Yapi Merkezi!?
Katika zabuni kuna masuala mengi yanatizamwa mkuu.
 
Tasnia ya traditional motor vehicle unaishi kibishi.
Hao Benz n.k wanajua joto wanalivumilia
 
Iran hakuwa na ubavu wowote ule wa kumshinda mchina kwenye hiyo tender ya SGR na hata mturuki alipewa tu kwa mlango wa uwani.

Halafu hawa wairan wa deal chafu za kuuza mafuta kwa magendo ndo wakatae kutoa 10% ili wapate tenda? Hapa umedanganywa
 
Iran hakuwa na ubavu wowote ule wa kumshinda mchina kwenye hiyo tender ya SGR na hata mturuki alipewa tu kwa mlango wa uwani.

Halafu hawa wairan wa deal chafu za kuuza mafuta kwa magendo ndo wakatae kutoa 10% ili wapate tenda? Hapa umedanganywa
Huwa unafikiria pafupi sana aisee mkuu.
Jaribu kutanua akili.
Kama Uturuki alivyopewa kwa mlango wa uwani basi na Iran vivyo hivyo alitaka kupewa kwa mlango wa uwani.
Suala la uuzaji wa mafuta kimagendo ni kwasababu Iran inakwepa vikwazo vya kiuchumi ndio maana inauza mafuta kwa mlango wa nyuma,haitoi pesa ili iuze mafuta.
Embu tofautisha kuuza kitu kwa siri na kupata zabuni kwa kulipa 10% ya pesa ya mradi,kiakili ya kawaida utaona kama unadhulumiwa.

Embu usiwe unaifunga akili tanua akili mazeeh.
 
Unajichanganya sana yaan hujui hata unaandika nini,
Kwa akili yako unataka kusema kuwa hao wairan walishangaa sana walipoambiwa kutoa 10%? maana wao ni wasafi sana na hufanya deal safi tu no rushwa? kitu ambacho ni uongo mtupu kwenye tenda kubwa kama hizo kila kampuni inayobid inajua kabisa mkono mtupu haulambwi na tena hii africa ndo kabisaa
Hebu taja jina la hiyo kampuni ya Iran acha blah blah na ngano zako
 
Mbona Netanyau %90 ya raia wake hawamtaki kila siku wanaandamana lakini hataki kuondoka?
Ebu nitajie nchi moja ambayo raia wote huwa wanaiunga mkono serikali?
Viwanda nchini Ujerumani vimefirisika na uchumi wake umeingia kwenye mdororo mkubwa na kupelekea serikali kuanguka mbona hujaja hapa kubwabwaja hizo ngonjera zako?
Iran inamiliki viwanda vya magari nchini Iraq na Pakistan mbona hawajavifunga hivyo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…