Actually kupeleka mtoto chini ya miaka 12 boarding ni bad parenting.
Kenya wako mbele sana kwenye kufikiri, ni ukabila tu unawatia doa.
Hata mtaala wa elimu ni wa aina yake, sio huu wa kwetu wa kukomalia ufaulu tuu.
Wakenya wakiwa kitu kimoja ni rahisi kutawala Afrika mashariki.
Kenya ya Sasa na katiba waliyo nayo ukabila imeshapitwa na wakati.
Tanzania Kwa Sasa ukabila Upo mkubwa sana. Kinachotusaidia ni dini mbili kubwa uislam na Ukristo ambao mara nyingine udini unavuruga ukabila. Yaani dini inakua ni kabila jipya katikati.
Uchaguzi wa Juzi Kenya umethibitisha kuwa Kenya hakuna ukabila. Siku zote ukabila na udini unajengwa na watawala kwenye katiba kama tuliyo nayo. Ukiwa na katiba ya hovyo na ya kidikteta lazima uwe mkabila au mdini Vinginevyo usalama wako Utakua mdogo.
Ukabila unajitokeza Kwa sababu ya mtu mmoja kuwa na nguvu za teuzi. Kama katiba haimbani mwenye mamlaka ya kuteua ni lazima apendelee wa kwao mana ndio namna ya kuwasaidia Kwa kuwapa nafasi zenye maslahi. Kama ana mtoto Jeshini lazima ampe cheo Cha juu au mtu wa kabila au dini yake ili apate Taarifa za ndani. Ukiwa na katiba ya kifalme halafu ukataka kuwafurahisha wote basi nchi itagubikwa na ubadhirifu kila Kona mana utaogopa kuwatumbua watu na watakua wanakutisha .
Wakenya wameshajikomboa kwenye ukabila na hata udini mana kila mtu sasa ana uhuru wa kumlalamikia yeyote anapoona Kuna uonevu. Kabila Fulani wanaweza kuandamana Kupinga kubaguliwa na isiwe ni uchochezi.
Tanzania hata kama Kuna harufu za udini au ukabila ni kosa la uchochezi Kwa mwananchi wa kawaida kusimama na Kupinga viashiria vya udini au ukabila.
Tundu Lisu alipigwa Risasi baada ya kusema kuwa Serikali ya awamu Ile ilizuia viongozi kusafiri nje ya nchi isipokuwa Roma peke yake na alisema kuwa Roma haikuzuiwa Kwa sababu Rais wa awamu hiyo alikua ni Mroma. Haikupita siku tatu Lisu alipigwa Risasi. Watu wakajidanganya kuwa alipigwa Risasi Kwa sababu sijui za makinikia sijui maelekezo sijui Nini . Hapana kauli ya Kupinga viashiria vya udini vilimponza mana Kuna watu wanaonufaika na upendeleo wa kidini au kikabila. Hawapendi jambo Hilo litoke mana kwao ni faidi kwenye teuzi.
Hapo Mtawala Wala hahusiki ila Chawa ndio wanajichukulia SHERIA mikononi ili kulinda ulaji wao.
Kwa katiba mbovu Kuna watu wanasema Tanzania uongozi uwe wa kupokezana kati ya Waislam na wakristo . Yote ni sababu ya Fursa za uteuzi na kupeana ulaji bila sifa.
Watu wanateuana kama fadhila na kama mashinikizo .
Leo hii Rais wa awamu hii ni muislam Kuna mambo inabidi ayaache yaende hivyo hivyo ili TU asija akalaumiwa kuwa ni mdini.
Kuna wakristo wengi wangepaswa kutumbuliwa na kupelekwa gerezani lakini akifanya hivyo watapenyeza uongo kuwa wanaonewa Kwa sababu ni Wakristo.
Pakiwa Katiba inayopunguza mamlaka ya Rais kuteua kila mtu itawafanya watu waadilifu tuu kuteuliwa bila kujali dini zao.
Kama sio mwadilifu ujue kubaki madarakani kutakupelekea kifungo.
Leo watu wanaiba Mali za umma wanakimbilia kujenga nyumba za Ibada na kutoa masadaka Mengi . HALI INAYOWAFANYA KUONEKANA KUWA NI WATU WA MAANA SANA KWENYE DINI ZAO.
HALIKADHALIKA KWENYE MAKABILA MTU ANAIBA SERIKALINI HALAFU ANAPELEKA JIMBONI KWAKE ANAONEKANA NI WA MAANA SANA. UKIMTUMBUA UNAAMBIWA UTAUA CHAMA MANA JIMBO LAKE BILA CHAMA HAKIPATI KURA NA WATU WANALETA fitina kuwa anatumbuliwa mana ni kabila Fulani na mkubwa ana chuki na kabila Hilo . Ukabila unachukua nafasi ya utetezi na sio uzalendo Tena.