Serikali ya Kenya muachieni Mchungaji Paul McKenzie haraka sana

unaijua funga ya walokole lakini? Acheni kuhusisha walokole na imani za kishenzi. Padri/sheikh hawezi kuongeza vitu ambavyo havipo kwenye mifumo yao ya kuabudu. Wakatoliki wana liturujia na waislam wana msaafu wao kuwaongoza namna ya kufanya ibada zao, hakuna anayeleta yake. Walokole wako samart sana kuhusu mafundisho feki, hawadanganyiki na mitume na manabii feki,
 
umewahi kuingia kwenye makanisa ya kilokole usikie misimamo yao juu ya wahubiri feki? Wale hawadanganyiki, wanajua siku za mwisho watatokea manabii feki wadanganyao watu wengi na kuwaangamiza, ndio maana hukuti mambo ya maji, mafuta na keki ya upako makanisani mwao. Hawana huo upuuzi msiwahusishe na wahuni wanaotumia jina la Yesu kudanganya watu wasiojua kusoma maandiko
 
Sahihi kbsa mkuu Wala mm sikuwataja waislamu mm nimewataja wakristo waislmu wako vzr kwenye kufunga kwa utaratibu unao eleweka kote duniani
mjue mambo ni yaleyale, hizi sio funga Mungu anazozitaka, haya ni maagizo ya wanadamu tu na kufuata mkumbo. Wengine mpaka wanaogopa kula mchana kwa kuwa wenzao wamefunga, wanadhihakiwa ni kobe la mchana. Hatufungi kwa kufuata mkumbo, sifungi mifungo ya ajabuajabu eti kwa kuwa watu wengi hufunga
 
Hili suala ngoja tuone mwisho wake baada ya uchunguzi ,bwana Mackenzie mwenyewe kwenye mahojiano anasema hausiki kabisa na hajui hizo habari za kuua watu na kazi ya uchungaji alishaiacha....ukistaajabu ya musa....
 
Waislamu si nao wana tawi la magaidi?
Wanafundishwa ujinga hadi wanajilipua?
unakuta mtu anatokwa povu jingi kulinda dini yake isinyooshewe kidole wakati nayo ina mafundisho hatari. Wakiambiwa wapuuzi wapo kila dini wasibishe bali wachukue tahadhari kuachana na mafundisho hatari
 
Na wewe utakufa pia acha ujinga...
 
Kheri yetu sie tumeamrishwa kufunga km walivyoamrishwa kabla yetu ili tupate kumcha Allah...na hii ni aya katika Qur-an na ndio tunaifuata...na tumeelekezwa namna ya kufunga, kuanzia kuchwa jua mpk kuzama kwake, na katika kufunga pia tumeelekezwa nani anatakiwa atekeleze ibada hio, kuna waliokuwa wanaruhusika kutokufunga (watoto, vikongwe, wagonjwa, walio kwenye safari n.k...hii kuonesha kuwa hakuna kukalifisha kwenye dini. )

Isitoshe tayari waumini wana mazoea ya kufunga maana tunaanza kufunga tangu tukiwa baleigh unajikuta unazoea na kuona ni kitu cha kawaida tu. Km siku hizi baada ya eid kuna wanaofunga 6 za mwezi huu wa shawal, kuna wanaofunga kila J3 na Alkhamis, kuna wanaofunga kila mwezi siku 3 n k. Na watu walozoea kufunga ndio wana afya nzuri kuliko ht watu wanaokula kula ovyo...

Sasa tukirudi kwa hawa wakenya, wamefungishwa baada ya kuambiwa au kudanganywa na binaadam mwenzao hamna hata andiko au agizo kutoka kwa muumba wao. Pia hata mazoea ya hizo swaumu hawana...sijui wamedanganywa vp maskin
 
Sasa huu uzi unauhusu Uislam? Tunachokitaka ni kuwa Uislam usiingizwe kwenye hili kwa namna yoyote ile. Nyie kukitokea vituko kwenu lazima mtake kuugusa gusa na Uislam.
Inahusu imani potofu bila kujali dini ewe alqaeda
 
Yule WANYONYI nilicheka sana wakati mke wake anaelezea kabisa kuwa huyu unaweza ukaona ni mtu wa kawaida ila ni mungu kabisa. Pia amekaa na dhana zake kabisa ambazo anasema atatumia kutesea waliomuasi siku ya kiama.
 
Naam, Allah akulipe kheri dada yangu.

Kuna watu wajinga sana humu. Kuna mpumbavu anajiita Shilla sijui aliongea maneno ya kashfa kwa Yesu. Ikarushwa WasafiTv, baadhi ya vichwa maji humu wakaanza kuutukana Uislam katika uzi wa kujadili lile. Yule Tito nae alivyoleta mambo yake baadhi ya watu humu wakaanza kuwa gusa gusa Waislam. Matatizo ni ya kwao kabisa, lakini kuna watu humu lazima watalazimisha na Waislam waingie.
 
Mkuu naomba nikuulize..mwamposa,gwajima na mwakasege ni walokole au dhehebu gani?
 
Mkuu naomba nikuulize..mwamposa,gwajima na mwakasege ni walokole au dhehebu gani?
nakujibu, mwamposa ni mhubiri wa huduma ya maombezi inayoitwa inuka uangaze, gwajima ni mchungaji na askofu mkuu wa makanisa yake ya ufufuo na uzima, mwakasege ni mwalimu wa kilutheri mwenye huduma yake inayojitegemea iitwayo mana. Wote hawa wanahubiri kama wapentekoste mliozoea kuwaita walokole. Wawili kati yao wamepitia upentekoste kabla ya kuanzisha huduma zao. Ifahamike kuwa wapentekoste hawakubalaini na mafundisho yao kwa kuwa kuna mafundisho wanayofundisha si ya kipentekoste yaani yako nje na upentekoste. Kwa hiyo wakifanya mabaya wasihusishwe na ulokole wale wana imani zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…