OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Sheria mpya inayopendekezwa nchini Iraq inayolenga kupunguza umri wa ridhaa ya Ndoa kwa Wanawake hadi miaka tisa jambo linalolenga kuruhusu Wanaume Nchini humo kuoa Wanawake wakiwa na Umri mdogo, imepingwa vikali na Wanaharakati Nchini humo wakidai kuwa ni yenye kuhalalisha udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto ambapo pia inaelezwa kuwa Sheria hii inataka kufuta moja ya sheria bora zaidi za haki za Wanawake katika Mashariki ya Kati, ambayo inawapa Wanawake haki za kudai talaka, malezi ya Watoto, na urithi.
Wanaharakati na baadhi ya Wabunge wa Iraq wanapinga kwa nguvu pendekezo hili, wakisema kuwa litakuwa janga kwa haki za Wanawake na Watoto, Raya Faiq, ambaye ni Mratibu wa Makundi ya kupinga sheria hii, alisema kuwa pendekezo hili litaruhusu Ndoa za Watoto na kuminya haki za Familia za kukataa Ndoa hizo huku akiweka wazi kwamba sheria hii itakuwa ni njia ya kisheria ya kuruhusu udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto.
Aidha Serikali ya Iraq, kwa upande wake, inadai kuwa mabadiliko haya yatasaidia kufuata sheria za Kiislamu, wakisema kwamba yatawalinda Wasichana kutoka kwa mahusiano yasiyofaa lakini hata hivyo, Wanaharakati wanasisitiza kwamba sheria hii itawarudisha nyuma Wanawake na Watoto kwa miaka mingi.
Sheria hii ilipitishwa kwa mara ya pili Bungeni mnamo Septemba 16, 2024, na inatarajiwa kupitishwa tena kutokana na msaada kutoka Vyama vya Shia Nchini humo lakini hata hivyo inaelezwa si Vyama vyote vya Shia vinaunga mkono sheria hii, na bado kuna juhudi kubwa za kupinga.
Mapambano haya ni muhimu kwa Wanawake wa Iraq, ambao wanapinga vikali hatua hii, wakiitaka Serikali kuepuka kurejesha nyuma haki za msingi za Wanawake na Watoto.
====================================================
Iraq is set to pass legal amendments to the country's marriage law that allows men to marry girls as young as nine. Amendments have also been proposed to deprive women of the right to divorce, child custody and inheritance, reported The Telegraph.
The bill would also allow citizens to choose either religious authorities or the civil judiciary to decide on family affairs.
The conservative government led by a coalition of Shia parties aims to pass the proposed amendment in an attempt to protect girls from “immoral relationships”. The second amendment to the law was passed on September 16.
Source: Hindustan Times