Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Leo naomba tujikite katika mjadala wa athari za uuzwaji wa NBC kwa kampuni ya ABSA ya Afrika kusini.Miaka ya 90s NBC ilikuwa moja ya bank kubwa sana kusini mwa jangwa la sahara ikimilikiwa na serekali ya Tanzania.Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali bank hii ilikuwa ikitengeneza faida kubwa sana na si hilo tu bali ilikuwa kikwazo kikubwa kwa bank za nje zilizotaka kufanyabiashara Tanzania.
Moja ya faida kubwa ya NBC ilikuwa ni kuisaidia serekali wakati ilipokuwa ikiitaji fedha kwaajili ya uendeshaji wa shughuli zake za kawaida na hata kugharamia baadhi ya miradi mikubwa.
Mara baada ya Mwl Nyerere kupata taarifa kwamba NBC ipo mbioni kuuzwa alijaribu bila mafanikio kuzuia uuzwaji wa bank hiyo kubwa lakini alifanikiwa walau kuanzishwa kwa bank ya NMB ambayo serekali ina hisa nyingi.
Ni wazi NBC ilikuwa chanzo kikubwa cha mapato ya serekali ya awamu ya kwanza na pili ya Mzee Ruksa kabla ya Rais B Mkapa kuamua kuiza kwa bei ya kutupwa tena kwa kampuni ya nje (mjadala mrefu unatakiwa).
Baada ya chanzo hiki muhimu kuondolewa na Rais wa awamu ya nne je athari zake kwa serekali ya Kikwete ni zipi ?.
Mimi naweka moja ambalo sasa lipo wazi kabisa.Serekali ya Kikwete baada ya kukosa chanzo hiki muhimu cha mapato imevamia mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF,PPF......)Matokeo yake umri wa kustaafu umeongezwa kutoka miaka 55 hadi miaka 60 na sheria nyingine ipo mbioni ambayo italazimisha wafanyakazi watakaoacha kazi au kufukuzwa kazi hawatalipwa mpaka watakapofikisha miaka 60.Mifuko hii ipo taabani kifedha kwakuwa fedha zake nyingi zinanyakuliwa na serekali bila kurejeshwa matokeo yake wachangiaji wa mifuko hii ni kulipwa fedha zisizo endana na hali halisi ya maisha.
Unaweza kuongeza athari nyingine kadri uonavyo.