Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naomba majibu Tafadhali ili kuwa na reference nzuri na ya uhakika humu jamvini.

Baada ya Rais SSH kuapishwa leo je anaendelea kuongoza serikali ya awamu ya 5 au tumeingia awamu mpya ya 6?

Naelewa kuwa ilani ya CCM inayotekelezwa ni ile ile.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kalamu nyeusi au nyekundu, Mh. Rais Samia Suluhu Hassan akumbusha yeye ni Rais hivyo aletewe kalamu sahihi.

Hata masuala ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kurithi kalamu nyekundu, inayotumiwa na Rais leo kutokana na mambo kwenda kasi akaletewa kwa bahati mbaya kalamu nyeusi.

Ikabidi Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kukumbushia aletewe kalamu nyekundu ya utendaji ambayo ndiyo hutumiwa na mkuu wa nchi.

Hiyo imetokea leo live / mubashara katika mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri ulioongozwa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.

Muda unaenda kasi, hivyo itachukua siku kadhaa mpaka kila jambo liende na kutambulika kama inavyotakiwa kutokana na Tanzania kwa mara ya kwanza kumpoteza rais aliyekuwa bado yupo ktk utumishi kuacha kuitumikia nchi kutokana na kufariki akiwa madarakani.
 
Tanzania flag-XXL-anim.gif
 
Awamu ni mtu,je wakati Mzee Jumbe anatoka madarakani na anakuja Mzee Mwinyi naye akatoka ilikuwa hawamu ile ile au zilibadilika??
 
Naona wanamjaribu tena kama walivyomwambia siku za maombolezo ni 14. Anahema kama ametoka kutembea umbali mrefu, Mama please Afya ni muhimu.
 
Mwalimu Nyerere aliyeongoza kwa miaka 24 ilikuwa awamu ya ngapi hadi ya ngapi? Na Mwinyi, Mkapa, Kikwete waliofuatia kila mmoja miaka 10 walitawala awamu ya ngapi hadi ya ngapi mtawalia (respectively)? Majibu ya hilo swali yatakusaidia kujua awamu ya Samia ni ya 5 au ya 6!
 
Awamu ya sita (maana Samia hata akiamua kugombea baadaye, atagombea 2025). Sababu ni kuwa, mpaka 2025 atakuwa ameshaongoza kwa miaka mi4.
Mkuu wanasheria wanasema ni awamu ya tano,ila ni ruksa kugombea akimaliza awamu hii ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom