Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Awamu ya tano. Serikali hii sio mpya, ni muendelezo wa serikali ya JPM hakukua na uchaguzi.
 
Ninavyojua ni Awamu ya Sita, maana awamu inaenda na Rais mwenyewe japo awamu yake imeanzia njiani kumalizia alipoachia JPM, ni kama Zanizibar alivyofariki Karume Jumbe alkua Rais wa awamu ya pili na sio ile ie ya kwanza.
Hili ndilo tatizo la kuchukua neno la lugha nyengine na kutaka kulifanya lako.
 
Unatuuliza sisi tena ?

Nyie si ndio mlijipa ukuu wa kutawala milele...?

Ama kwa hakika Mungu ametufuta machozi ya October mwaka jana tulipokuwa na majonzi na itakuwa fundisho kwa viongozi wote watakaofuata..
 
Mwanamke wa kizanzibar anaongoza Tanganyika hadi Zanzibari, SAFI SANAAAA!
Hakuna namma subiri kuepetiwa petiwa kizanzibari ni aina ya utawala ambao naamini hautakuwa wa machungu sana kama ule... Japo ccm ni ileile
 
Uchaguzi wa mwaka 2020, Hashim Rungwe angeshinda angekuwa ni Rais wa 6 wa JMT. Awamu (japo neno hili halipo popote kisheria) ingekuwa pia ni ya 6.

Tunapopata Rais mpya na awamu inakuwa ni mpya.
 
Tafuta mwanasheria umuulize.

We jamaa, sio kila mwanasheria anaelewa anachokisema.

Awamu ni muhula wa miaka mitano au kumi? Kuna marais wametawala zaidi ya miaka kumi na wengine kumi kumi. Awamu inahusishwa na kiongozi anaeingia madarakani, haihusiani na muhula wa mzunguko wa uchaguzi.

Mie sio mwana sheria, ila kwa uelewa wa kawaida tu, hii ni awamu ya sita (1 Nyerere, 2Mwinyi,3 Mkapa, 4Kikwete, 5Magufuli, 6Samia)
 
Hii ni Awamu ya 6. Kwa kuwa anaingia ikiwa imebaki zaidi ya miaka3 kwa awamu ya 5.
Kwa hiyo kama atagombea 2025 ataruhusiwa kipindi kimoja tu. Na itaitwa awamu ya 6 pia.
Kama ingekuwa imebaki miaka 2 au 1ingekuwa awamu ya 5 hiyo hiyo.
Kwa hiyo mama ni Rais wa 6 katika awamu ya 6.
 
Hilo neno maendeleo hayana vyama inabidi uache kulitumia
 
We jamaa, sio kila mwanasheria anaelewa anachokisema.

Awamu ni muhula wa miaka mitano au kumi?
Mie sio mwana sheria, ila kwa uelewa wa kawaida tu, hii ni awamu ya sita (1 Nyerere, 2Mwinyi,3 Mkapa, 4Kikwete, 5Magufuli, 6Samia)
Hakuna haja ya kubishana mkuu.Na mbona mwenyewe umekiri kwamba sio mwanasheria.This proves that you don't know.

Anyway,nimesema tafuta mwanasheria unayemuanini wewe kama unataka kupata ukweli.

Sidhani kama TBC1 wanaweza kumualika mwanasheria kihiyo kiasi hicho asiyejua hata kitu kidogo kama hiki.Jamani ubishi mwingine hauna maana.
 
Back
Top Bottom