Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Awamu hutimilika kwa ile miaka 5 au 10 ya kikatiba na wala si uwepo wa mtu fulani
 
Ninavyojua ni Awamu ya Sita, maana awamu inaenda na Rais mwenyewe japo awamu yake imeanzia njiani kumalizia alipoachia JPM, ni kama Zanizibar alivyofariki Karume Jumbe alkua Rais wa awamu ya pili na sio ile ie ya kwanza.
Usipotoshe umma mkuu ulichoandika kakifanyie kazi alafu uandike upya.
 
Uchaguzi wa mwaka 2020, Hashim Rungwe angeshinda angekuwa ni Rais wa 6 wa JMT. Awamu (japo neno hili halipo popote kisheria) ingekuwa pia ni ya 6.

Tunapopata Rais mpya na awamu inakuwa ni mpya.
Tunapopata Rais mpya na Bunge jipya katika Uchaguzi tunapata Awamu mpya kwa hiyo kama Rungwe angeshinda tungekuwa na Rais mpya na Bunge la CCM jipya leo ingekuwa Awamu ya Sita na Awamu ya Tano ingekuwa ya Kipindi kimoja tu kama ya Repblican ya Rais Trump wa Marekani na Mama Samia angekuwa out of the scene.
 
Ufafanuzi Mheshimiwa Rais SSH ni Rais wa awamu ya sita. Awamu inaendana na rais kubadilika siyo Miaka aloongoza

Ufafanuzi wa Kwanza

Zanzibar alipofariki Karume, aliyefuata iliitwa awamu ya pili wala siyo ya Kwanza

Pili Wanaodhani awamu ni Miaka 10 je Nyerere aliyeongoza miaka 23 ameongoza awamu mbili? Ni moja

Ingetokea Lissu akawa Rais Mwaka 2020 serikali yake ni awamu ya sita so Kwamba anakamilisha Kumi ku combine na Magufuli ili iwe miaka 10 watengeneze awamu kamili

Pia Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya Sita,

Ufafanuzi wa Samia Suluhu kugombea

Anzia Ibara ya 37(2) inaeleza kuwa Makamu Endapo Rais akifa yeye anahapishwa kuwa rais, Ila anaruhusiwa kugombea awamu ya pili , yaan akimalizia kipindi cha aliyekufa anaweza gombea Mihula 2 kama Rais aliyekufa alikuwa ameshaongoza Zaid ya Miaka 2 hiyo haihesabiki , hakatazwi kugombea mara mbili mbeleni, lakin akichukua madaraka wakati Rais alokufa kashaongoza Chini ya Miaka 2 hapo anaruhusiwa kugombea term moja

Mfano
Magufuli angefariki 2023 hapo Samia angechukua madaraka na kumalizia na anaruhusiwa kugombea 2025 na 2030,

Lakin kwakuwa Magufuli ameaga dunia 2021, Samia ataruhusiwa kugombea mara moja tu ya 2025

Poleni CCM mliotegemea kugombea 2025,

Britannica
That makes sense!
 
Hakuna haja ya kubishana mkuu.Na mbona mwenyewe umekiri kwamba sio mwanasheria.This proves that you don't know.

Anyway,nimesema tafuta mwanasheria unayemuanini wewe kama unataka kupata ukweli.

Sidhani kama TBC1 wanaweza kumualika mwanasheria kihiyo kiasi hicho asiyejua hata kitu kidogo kama hiki.Jamani ubishi mwingine hauna maana.Hapa shida kubwa ni matumizi ya neno awamu na muhula/ mihula.

Narudia tena, Mama Samia anaanza awamu ya sita muhula wa kwanza.
 
Back
Top Bottom