Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni awamu ya 5 au 6?

Ninavyojua ni Awamu ya Sita, maana awamu inaenda na Rais mwenyewe japo awamu yake imeanzia njiani kumalizia alipoachia JPM, ni kama Zanizibar alivyofariki Karume Jumbe alkua Rais wa awamu ya pili na sio ile ie ya kwanza.
Mwongo mkubwa acha kudanganya umma bado ni awamu ya tano,awamu ni two terms miaka kumi!
So rais wa sita awamu ya tano!
 
Ufafanuzi Mheshimiwa Rais SSH ni Rais wa awamu ya sita. Awamu inaendana na rais kubadilika siyo Miaka aloongoza

Ufafanuzi wa Kwanza

Zanzibar alipofariki Karume, aliyefuata iliitwa awamu ya pili wala siyo ya Kwanza

Pili Wanaodhani awamu ni Miaka 10 je Nyerere aliyeongoza miaka 23 ameongoza awamu mbili? Ni moja

Ingetokea Lissu akawa Rais Mwaka 2020 serikali yake ni awamu ya sita so Kwamba anakamilisha Kumi ku combine na Magufuli ili iwe miaka 10 watengeneze awamu kamili

Pia Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya Sita,

Ufafanuzi wa Samia Suluhu kugombea

Anzia Ibara ya 37(2) inaeleza kuwa Makamu Endapo Rais akifa yeye anahapishwa kuwa rais, Ila anaruhusiwa kugombea awamu ya pili , yaan akimalizia kipindi cha aliyekufa anaweza gombea Mihula 2 kama Rais aliyekufa alikuwa ameshaongoza Zaid ya Miaka 2 hiyo haihesabiki , hakatazwi kugombea mara mbili mbeleni, lakin akichukua madaraka wakati Rais alokufa kashaongoza Chini ya Miaka 2 hapo anaruhusiwa kugombea term moja

Mfano
Magufuli angefariki 2023 hapo Samia angechukua madaraka na kumalizia na anaruhusiwa kugombea 2025 na 2030,

Lakin kwakuwa Magufuli ameaga dunia 2021, Samia ataruhusiwa kugombea mara moja tu ya 2025

Poleni CCM mliotegemea kugombea 2025,

Britannica
 
Ooh mara hii mmeshatoka JPM sasa ni SSH kweli kwenye maisha miaka 10 ni sawa na siku 1 maisha yanaenda kasi sana
 
Masuala ya awamu ni ya chama sie raia tunahesabu maraisi tu. Sasa huyu ni wa sita.
 
subirini ufafanuzi awamu moja haiwezi kushikwa na watu wawili mtu akiondoka awamu imeisha hakuna cha vipindi wala nini
Mkuu kumbe nawe kilaza sio!??
Awamu ni ya 5... Muda wa Ngosha haujatimia. Mama anamalizia..
 
Katiba haitambui kama Rais SSH anamalizia muhula wa hayati Magufuli!
Inatambua. Soma vizuri.

"Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano..."

Rais (wa awamu) ni yule aliyechaguliwa na wananchi.
 
6
Hiyo Ndiyo Awamu
Awamu Yenye Bahati Kiutendaji
Mambo Ni Bul Bul
 
Inatambua. Soma vizuri.

"Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano..."

Rais (wa awamu) ni yule aliyechaguliwa na wananchi.
Duh!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Naomba majibu Tafadhali ili kuwa na reference nzuri na ya uhakika humu jamvini.

Baada ya Rais SSH kuapishwa leo je anaendelea kuongoza serikali ya awamu ya 5 au tumeingia awamu mpya ya 6?

Naelewa kuwa ilani ya CCM inayotekelezwa ni ile ile.

Maendeleo hayana vyama!
Huyo ni Rais wa Pili wa Awamu ya Tano na lazima atekeleze Ilani ya Chama chake ila anaweza kuleta mbinu yake ya utekelezaji (Management Style), mfano: Mtangulizi alikuwa anazunguka na mabulungutu ya fedha za Serikali kuwasaidia wanyonge lakini kwenye Mkutano wa maelfu ya watu alikuwa anasaidia mmoja tu anayemfikia kumbe palepale kuna mamia ya wenye shida kama za aliyenufaika au wenye shida kubwa zaidi au kununua Jogoo Sh. Laki kumbe kuna Mkulima hapohapo ana Jogoo mkubwa zaidi lakini angetatua tatizo lake angempata mnunuzi wa kumpa Sh. 5'000 ampeleke mtoto wake shule. Mfano mzuri: Zanzibar wazee wote wa umri wa miaka 60 au zaidi wanalipwa Pensheni na Serikali haijalishi ulikuwa Mtumishi, Mkulima, Mvuvi, Mzururaji nk lakini Bara hata Watumishi wengi wanakufa wakidai Mafao yao ingawa kuna Sera na Wizara ya Wazee toka Awamu ya Tatu. Management Style ya Rais mzuri inaangalia Nchi nzimà na vilivyomo!
 
Back
Top Bottom