#COVID19 Serikali ya Saudia yasema "Mwaka huu ni wale Waislamu waliopata chanjo ya COVID-19 pekee ndiyo wataruhusiwa kuhiji Makka/Madina"

Msiwapingie watu namna ya kuishi, ile ni nchi huru hivyo na inajua ni kipi ni kizuri au kibaya kwa wananchi wake. Dini nyingi zina mambo ambayo yamepitwa na wakati au irrelevant. Hivyo pengine wameamua kuja njia ya kisasa zaidi ya kuabudu. Zaidi ni kuwa huo uislam umeanzia kwao na hivyo pengine wanaufahamu zaidi.
 
Mkuu suala la dini halina mambo ya kisasa wala zamani..

Dini ni sheria ambayo ilishapitishwa na Mungu.
 
Dhambi ya ubaguzi katika imani sijui imekaaje?
Mabohora, Sunni, Shia wote muda wa ibada yanatendeka yaleyale. Quran ni ileile.

Everyday is Saturday............................... 😎
 

Serikali ya Saudia kuwa na wahuni haibadilishi uhalali wa Makka kama sehemu ya Kuhiji. Swala ni kwamba mnaweza kwenda bila kupata chanjo? Kama hamuwezi kwenda mnafanya nini sasa?
 
Serikali ya Saudia kuwa na wahuni haibadilishi uhalali wa Makka kama sehemu ya Kuhiji. Swala ni kwamba mnaweza kwenda bila kupata chanjo? Kama hamuwezi kwenda mnafanya nini sasa?
Kitendo cha kuhalalisha kwenda hijja kwa chanjo ,,

Ni kuthibitisha uhuni wao..
 
Mkuu njoo kwenye harakati zetu wa ukombozi wa fikra. Sisi habari za dini tulichaachana nazo. Maana dini zililetwa ili kutugawa na kututawala. Sisi ni waumini wa uafrika wetu, na upendo kwa ndugu zetu wote, sio kisa wa dini moja ndio umpende, halfu wa dini nyingine umtenge.

Sisi ni pan afrika. Tunafurahia maisha, hatumaind tena majina ya waarabu wala wazungu. Tumeamua kuish kwa upendo na mshikamano
 
Unaposema Shia sio waislamu una maana gani mkuu??...
Sunni huamini mashia sio waislam bali Ni wachafuzi wa uislam
Hata hapa dar Kuna misikiti ya Shia na Sunni na ilitokea misikiti flan umepata ufadhili ujengwe na waarabu wa Saudi kulizuka mzozo hatari na inashindikana.
Kuuliza nkajibiwa wasaudi wasunni , sisi mashia watajaweka imam wa kissunni
 
Mwanamayu ndiyo ujue kuwa dini ni miradi ya watu kupatia pesa na kuwatawala wengine!
miye nilitegemea vatican,jerusalem na makka zisiguswe na korona kwani huko ndiko chimbuko la ukristo au uislamu!
Hujui dini, yohana alikatwaa kichwa, stephano aliuwawa.
Kuwa na dini haimaanishi kuondolewa majaribu.kama Yesu alijaribiwa sembuse marytina?
 
Kwani hao waasi wa Yemen walikuwa wakiwauwa wakristo?
Waasi mashia walitaka kumpindua rais msunni, Ni waislam vs waislam na kila mmoja akijiona mwislam zaidi
 
Hivi afrika tunatawaliwa na dini kweli? hebu elezea huo utawala wa dini tunao tawaliwa nao huku afrika ukoje?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…