#COVID19 Serikali ya Saudia yasema "Mwaka huu ni wale Waislamu waliopata chanjo ya COVID-19 pekee ndiyo wataruhusiwa kuhiji Makka/Madina"

#COVID19 Serikali ya Saudia yasema "Mwaka huu ni wale Waislamu waliopata chanjo ya COVID-19 pekee ndiyo wataruhusiwa kuhiji Makka/Madina"

Hivi chanjo inazuia aliyechanjwa kutoambukiza wengine?
Ndio hapo sasa, aliyechanjwa anakuwa amejikinga, lakini bado anaendelea kuambukiza wengine kama kawaida, sasa kwa maana hiyo katika suala la usambazaji virusi wote wako sawa, hili katazo halina mantiki
 
JPM akiipata hiyo

" Nimesikia ndugu zangu waislamu mmewekewa masharti kwamba mwaka huu hamuwezi kwenda kuhiji mpk uwe umechanjwa, Hao ndiyo viongozi wetu wa kiroho tulio nao leo yaani wanawazuia watu kutekeleza nguzo yao ya imani kisa ugonjwa, nilikuwa nachombeza na Mufti hapa kwani hatuwezi kujenga hiyo sehemu ya kuhiji kama ile ya Makka kule kisarawe kwa Mh Jafo ili na wao huko waje kuhiji hapa Tanzania kwa watani zangu wazaramo na fedha hizo zipo maana mambo mengine aah basi tu nisiendelee sana maana ni mambo ya imani ila ni mambo ya ajabu, ila wakiendelea kuwazuia leteni pendekezo tutajenga nasema tutajenga"
"Kwan nasema uongo ndugu zangu"
 
Umefupisha nini,mbona sijaona chochote ulichoeleza zaidi ya kusema shia sio waislamu?..
Nimekuuliza sabau ya kusema sio waislamu,unaniambia nikafanye uchunguzi.Wewe mwenye kujua ukweli umeshindwa hata kueleza kwa sentensi mbili kwanini unasema shia sio waislamu?
Nikisema hivi "Hakuna ibada hata moja tunayo fanya sisi Waislamu inafanana na ibada wanayo fanya Mashia".

Hapo uneelewa nini ?
 
Yanahusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu wa saudia.

Hawana uislam kitu..

Watalazimishaje mambo ya chanjo ambayo bado yamekuwa ni sintomfahamu ktk baadhi ya inchi ..

Kama unaona nakuumiza vaa chupi yako nenda..
Warembo wako wengi..
Hahahahahahahah, avae chupi aende? Duuuuh...., we jamaa wewe
 
Kila la Mtu ana uono wake mtazamo na maamuzi yake kulingana na utashi wake
Si sawa kulazimisha au kutaka serikari kua na mtizamo sawa na wengine wafanyavyo.
Issue ya Corona sio ya kukurupukia tu na kubugia chanjo kama tuonavyo.
Nashauri kuwepo na utulivu na utaratibu rafiki juu ya maamuzi yeyote ya hiyo chanjo.
N.b chanjo kwangu siafikiani nayo. Kufa nitakufa wakati wangu ukifika iwe Nina chanjo au sina. Nimechagua kutokua na chanjo
Nakuunga mkono
 
Uzuri sisi wazee wa "UKUU WA MWAFRIKA" maeneo yetu ya hija yapo afrika, hata kwa basi unaenda.

Kwann kuna shida gani mtu akipimwa na akawa neg- akaruhusiwa kusafiri. Kwan chanjo ni lazima?? Chanjo yenyewe wala haizuii maambukizi mapya.

Wanapozidi kukomaa nayo ndio maana waru wengi wanapata hofu juu ya ugonjwa huu

 
Mkuu serikali ya saudia ni genge la wahuni,,waliojivika joho la uislam..

Hii serikali ya kifalme hakuna inchi yeyote ya kiislam inayokubaliana nayo zaidi ya mataifa ya magharibi..

Hill genge la wahuni la saudia limekuwa likifanya mambo kadhaa ya kinyume na haki za binadamu kwa Yemeni kwa miaka kadhaa.

--Mfano kuendelea kushambulia Yemen,, haswa kwenye makazi ya raia na kuua watu wasio na hatia.

Bila kujali Wanawake na watoto.

Tena ikipata baraka zote za marekani,, kwa kuwauzia silaha za technology ya hali ya juu,,saudia iendelee kuipiga Yemen na kuikandamiza.

-- kuweka kambi za kijeshi kwnye bandari kadhaa kwenye mpaka kuzuia watu wa haki za binadamu kupeleka misaada Yemen..

Mkuu ukiona kwa macho wanayofanya saudia kwa Yemen,,yanasikitisha sana.

Tena waislam wenzao,,

Dini inasema ndugu wa muislam ni muislam mwenzie,,

Huo udugu upo wapi hapo?

Pasi na shaka huu utawala wa saudia ni genge la wahuni lililojivika joho la waislam.

Ukijumlisha na mauaji ya KASHOGI..

Hawafai hata kidogo..

Wanachokifanya wao ni kufata amri za mabwana zao marekani.

Na kuweka sheria za Mungu pembeni.

Wametoa mambo mengi ya kiislam na kuweka utamaduni wa kimagharibi..

Saudia ile inayopambwa kwenye vitabu vitakatifu. ,,sio hii iliyopo Leo..

Chochote kinachoendelea saudia kimepata baraka zote za mataifa ya magharibi..
Out of subject ...!!! Come to your senses please.
 
Hujajibu swali mkuu....NItajie nchi zenye/yenye uislamu kuliko saudi arabia..Simple tu
Mkuu uislam ni iman,,,

Saudia ni inchi takatifu iliyoshushwa qurain ,,

Na ni inchi aliyozaliwa mtume wetu Muhammad (S.A.W).
lakini haitoshi kusema kwamba family ya kifalme ndy inaharibu sifa za uislam mzima wa saudia.

Hivi jiulize wewe mtu ambaye hujawahi hata kuona kaburi l Mtume,Muhammad (S.A.W) ,,

au hata alama moja ya uislam,,
hujawahi kuiona kwa macho yako zaidi ya kusimuliwa.

Lakini unafata amri za Mungu,,
--unafunga.
-- unaswali.

Na kuogopa yale yaliyokatazwa ndani ya uislam..

Vipi hawa wasaudia ambao wanakila kumbukumbu ya alama za uislam,

- makaburi ya maswahaba yote yapo ,

- ushuhuda wa uislam wanaona hadi sasa.

Lakini wanafanya mambo tofauti na uislam.
Hii ni inchi takatifu lakini wapo watu hawaswali na wahuni kama kwengineko.

Zipo inchi zenye maadili ya kiislam kama Indonesia,Malaysia.iran
 
Yaani hata Ramadhani, haya mambo mbona yako wazi sana. Fatilia utaona, mambo mengine huwa yananoga ukishuhudia mwenyewe.
Kwenye ramadhani kuna tofauti zipi japo kwa uchache?
 
Saudi Arabia ni mke wa USA, yani katika mataifa ya kiislamu ni Iran pekee yake ndio mtetezi wa waislamu dhidi ha makucha ya beberu, wengi wote ni wachumba tu.

Haishangazi kuona Saudi ana toa boko kama hili maana ni kibaraka wa USA.
Nchi ni yao sasa wewe kinachokuuma nini? Very hopeless.
 
Nikisema hivi "Hakuna ibada hata moja tunayo fanya sisi Waislamu inafanana na ibada wanayo fanya Mashia".

Hapo uneelewa nini ?
Nikakuuliza unaweza toa mfano ni kwa jinsi gani wanafanya tofauti na nyie waislamu?..
 
Hii ni kwa mujibu wa tweet ya Zitto Kabwe.

Ameichagiza BAKWATA kuishikiniza serekali ya awamu ya 5 iruhusu chanjo kwa Watanzania ili waweze kutekeleza hii nguzo muhimu sana kwa Waislamu.

Hili ni la kwako mzee wetu Mufti Zuberi.....kabiliana na swahiba wako asiyetaka chanjo ili Mungu aendelee kukupa kibali cha kutumika katika nafasi nyeti uliyo nayo. Ama sivyo utakuwa umeuweka rehani utumishi wako ndani ya dini ya Mungu.

Acha ujinga wewe Mungu hana dini
 
Hii ni kwa mujibu wa tweet ya Zitto Kabwe.

Ameichagiza BAKWATA kuishikiniza serekali ya awamu ya 5 iruhusu chanjo kwa Watanzania ili waweze kutekeleza hii nguzo muhimu sana kwa Waislamu.

Hili ni la kwako mzee wetu Mufti Zuberi.....kabiliana na swahiba wako asiyetaka chanjo ili Mungu aendelee kukupa kibali cha kutumika katika nafasi nyeti uliyo nayo. Ama sivyo utakuwa umeuweka rehani utumishi wako ndani ya dini ya Mungu.

Enyi mawakala wa jokakuu mwovu na mharibifu mnafanya jitihada kubwa kuhakikisha lengo mnalitimiza ilio hasira za Mungu aliye hai awaangamize vizuri.

Kwa wadadisi ambao huwa hawafuati kelele za wanasiasa na mawakala wa maangamizi someni maandiko yafuatayo kisha tafakari:

The Mark of the Beast is Around the Corner

UFUNUO- 13:15-18
["..Let him that hath understanding count the number of the beast: for it is the number of a man; and his number is Six hundred threescore and six....]
 
Kwenye ramadhani kuna tofauti zipi japo kwa uchache?
1. Wao hawaruhusu mtu kuamka ukiwa na janaba ule muda wa alfajiri.
2. Hawaruhusu kupiga mswaki wala kuoga kipindi una swaum.
3. Wao huchelewa kufungua swaum
4. Kadhalika kwao haifai kufunga siku ya Ashura, wakati kwetu sisi funga hii ni sunnah
 
Nikakuuliza unaweza toa mfano ni kwa jinsi gani wanafanya tofauti na nyie waislamu?..
Sasa huo si mfano tosha na umejitosheleza ? Kwamba hatufanani nao kwa inada yoyote. Mathalani sala, kadhalika itikadi. Wao wanaamini Qur'aan tuliyo nayo haijakamilika iliyo kamilika anayo Mahd huko Pangoni. Mengi sana hatufanani nao Mashia.
 
Mkuu nimeshtuka sana wewe kusema mashia sio waislam.

Naomba utuelimishe muislam ni nani , na kwanini mashia sio waislamu , ni hilo tuu mkuu.
Wao wanaamini ya kuwa Mama Aisha alizini, kadhalika wanaamini ya kuwa baada ya Mtume kufariki maswahaba wote waliritadi isiokuwa wachache tu kina Abuu Dharri, Bilaal na wengine wachache yaani hawazidi kumi. Yaani maswahaba ambao Allah katika Qur'aan amewaridhia wao wanasema waliritadi.
 
Back
Top Bottom