Serikali ya Tanzania imeshindwa kutafsiri dhana ya Burkina Faso?

Yep..wenzetu tuliowaamini watuongoze na kutuonyesha njia ndio kwanza wanapakua minyama yote..tunaachiwa vimifupa.

Nimependa usikivu wa Ruto, japo imekuja kwa gharama
Ooh Okay, haijalishi tupo namba ipi, muhimu ni magari yepi na kwanini?
 
Leo ajuza nimekupa like angu japo umeshindwa kusema ukweli kwamba lazima tubadili katiba, watu waanze kuomba kazi kuanzia Mkuu wa Idara mpk Waziri nafasi zitangazwe zisiwe za machawa na ndugu wa Rais, pia lazima tubadili muundo wa elimu tuachane na hii elimu ya kijinga ya kukaririshana twende mbele zaidi.
 
FaizaFoxy umesema vyema. Ni dharau katika nchi ambayo bado tunajitafuta ila matumizi yetu ni ya kufa mtu. Serikali inaenda kununua gari thamani million Mia tatu(300 millions. Ukiunganisha gharama za mafuta, service na ununuzi wa vipuri ndani ya miaka miwili huenda likafika 1 billion.

Mfano wa pili;Serikali inalipa Madaktari Bingwa kuzunguka kila Mkoa/Wilaya wanalipwa per diem(150,000-170,000/=) huu ni mwezi wa Tatu lakini ukiangalia sehemu wanazoenda sio kwamba hakuna Daktari Bingwa la hasha wapo. Serikalini ni kutengeneza madili tu na political mileage. Hapo kwenye kampeni 2025 itakuwa tulitembeza Madaktari Bingwa nchi nzima na tuliwafikia watu kadhaaaa basi Tu ionekanae kama political credit

ITOSHE KUSEMA SERIKALI INA MATUMIZI YA ANASANA SANA AMBAYO HAYAENDANI NA UHALISIA WA MAISHA YETU.​
 
Hususan kwa watendaji, washauri wa Rais na vyombo vyetu vya intelijensia.

Nchi ndogo za magahribi ya Afrika zimeonesha jinsi Afrika inavyohitaji mabadiliko ya namna tunavyoongoza nchi na kusimamia serikali.

Tanzania ni wakati umefika itazame uhalisia. Ya nchi hizo ndogo ni mfano mzuri sana, na tusidhani hayajafika Afrika Mashariki, yameshafika. Yanasambaa kama moto wa makumbi.

Leo tunashuhudia Kenya hata Polisi na jeshi hawataki kuhusishwa na siasa na uongozi mbovu.

Tutakopa mpaka lini? Tutaendelea na kila kitu cha uongozi kukifanya siasa mpaka lini?

Tumeshuhudia watu kama Makonda wanaondokana na siasa za kulindana na kuingia kwenye uhalisia wa kumtumikia mwananchi. Naona mawaziri wachache sana wameliona hilo, lakini hawaonekani vilivyo na hawatumii media kuonesha dhahiri shahiri kuwa sasa siyo wakati wa siasa, ni wakati wa vitendo.

Tunataka tuone mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wakiondokana na dhanna ya kujitetea na kutetea ujinga, tunataka tuwaone wakitumikia wananchi muda wote.

Serikali iwachane kabisa na anasa za kijinga za magari ya kifahari kwa kila mkuu wa idara mpaka wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya. Hiyo ni dharau kubwa kwa wananchi wanyonge.

Kuna mengi sana ya kurekebisha na waziri wa fedha leo hii anakuja na bajeti ambayo haitekelezeki kwa jinsi fungu kubwa linavyokwenda kwenye matumiazi ya anasa. Anasa ya kwanza inayojionesha wazi wazi ni kwa Mtanzania wa kawaida, ni wakuu wote, kuaniza wa idara mpaka mawaziri kutembelea magari ya anasa ambayo ni mzigo mkubwa kwa nchi ya kimasikini.

Serikali ijirekebishe, tusifikiri sisi ni kisiwa, sisi ni nchi inayopakana na nchi nyingi Afrika. mabadiliko ya mama anayoyataka kwenye R zake nne yawekwe wazi, siyo kutangaza mabadiliko wakati naamini hata mawaziri hawaelewi ni mabadiliko yepi.

Naamini katika watendaji na idara zote za serikali waliyoelewa dhanna ya R nne ni wachache sana. Ofisi ya Rais inayohusika na habari inatakiwa itowe elimu kubwa kwa serikali na wananchi ili wote tuelewe ni kupi, kupatana, kustahamili, kubadilika na kujenga upya kuliko kusudiwa na falsafa ya R nne za mama Samia.

Ukifatilia habari za Burkina Faso kwa sasa, utaona kuwa wanaziishi R nne za mama Samia bila kuwa nazo.
S isi tulionazo tunashindwa kuziishi.
Hili bandiko lako nimeielewa mno, umeandika kama mwana mageuzi Leo
 
Moto ukiwaka ndo watashtuka. Kifupi watu wamemchoka Samia na serikali yake
 
Leo upo kwenye siku zako za heri.
Hongera kwa bandiko zuri madam ajuza.
 
Unang'ata na kupuliza cyo. Usilete mind game apa we ni wale wale tu.
 
Maajabu leo faiza umeongea ukweli,maana always ulikuwa mtu wa kuitetea serikali hata kwenye uozo.

Naona malaika wa Bwana amekushukia,safi na hongera kuona hili.
 
Back
Top Bottom