Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(DARUSO) waomba radhi

Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(DARUSO) waomba radhi

Enzi zetu leo hii nazani Pale Mlimani pangekuwa hapatoshi kabisa, siku huzi wanasoma watoto wadogo bado wanamaziwa vifuani mwao.Haiwezekani viongozi wanao watetea wasimamishe masomo na nyie mpompo tu. Huu ni ujinga na uoga wa kijinga pia.

Haki haiombwi hutafutwa, pambaneni Historia itawakumbuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hii barua imeandikwa na mwanafunzi wa chuo kikuu tuna tatizo kubwa kwenye mfumo wetu wa elimu. Mwanafunzi mwenye udhaifu wa kiwango hiki katika uandishi anafikaje chuo kikuu? Soma tu hiyo aya ya kwanza uniambie ulichoelewa.
badala ya wanafunzi kaandika wananfunzi

sijui hawakufanya editing baada ya kumalizA kuandika
 
Enzi zeno viongozi wa nchi walikua waelewa wana diplomasia na wanaheshimu democrasia na haki za wanafunzi, walikua nauchungu na wananchi.......sasa hivi uthubutu utapata majibu kamiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😆😆😆😆😆 hii nchi ina vituko
 
Hiyo iliandikwa na Joyce mutu ya Congo. Viongozi waliosimamishwa waligoma kusaini.
 
Kula na mbabe hakikisha ukitoza tonge kandamizia na finyango ya nyama kabisa kabisa maana ukizubaa utaambulia mchuzi mtupu.
Teh teh. Hizo finyango za kufichwa kwa tonge la ugali zinakuwa na mkato wa ukubwa gani?
Yote kwa yote, hii barua ya kuomba radhi imetolewa huku hao viongozi wa wanafunzi wameshafukuzika au namna gani?
Maana sasa habari hizi zinanichanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hii barua imeandikwa na mwanafunzi wa chuo kikuu tuna tatizo kubwa kwenye mfumo wetu wa elimu. Mwanafunzi mwenye udhaifu wa kiwango hiki katika uandishi anafikaje chuo kikuu? Soma tu hiyo aya ya kwanza uniambie ulichoelewa.
Kaandika huku akilia na kusahau ku re edit kabla haja print.

Kamwaga capitals kila mwanzo wa neno na makosa mengine kibao tu ya kiufundi kwenye uandishi wa barua yake hiyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia Mh Ndalichako asimalizie ghadhabu zake kwa wanafunzi tu, hapo chuoni kwenye utawala kuna tatizo pia apamulike.

Lazima kuna makandokando yaliyopelekea wanafunzi kusara.

Auwe nyani bila ya kuwaangalia usoni.

Hao staff wanaohusika na mikopo ya wanafunzi, wamulikwe kwa kurunzi ya spotlight, walishazoea kukandamiza haki za wanafunzi na kusababisha migomo ya kipumbafu inayoipaka matope serikali!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom