Serikali yaagiza Mtoto Charles Mathias arushwe Darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada

Serikali yaagiza Mtoto Charles Mathias arushwe Darasa kutoka Chekechea hadi Primary, Babu Tale aahidi kumlipia ada

Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza baada ya kuonyesha kipaji kikubwa kwenye somo la Hisabati.

Afisa tawala wa mkoa bwana Kobehelo amesema agizo hilo lianze kutekelezwa mara moja.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale ameahidi kugharamia elimu ya mtoto huyo hapo kijijini.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Anagharimia elimu ya huyo mtoto hapo kijijini? Elimu si bure?labda angesema amhamishe shule then amgharamie hapo sawa
 
Chekechea nayo Si ina kama stage tatu ?
Stage tatu za kiwiziwizi tu. Ukitaka kuikwepa hiyo kama mwanao yupo vizuri sana na umri umeenda, akimaliza stage one (the so called baby class), mhamishie shule nyingine akafanye interview ya stage ya tatu (pre unit) au ya darasa la kwanza kabisa
 
Babu Tale amchukue huyo Dogo Charles amlete Mikocheni pale kwake Kisha ampeleke Bunge au Olympio primary School shule za serikali za English Medium.
 
Hao wanavuta bangi Yaani chekechea to primary ndio kurushwa darasa

Kwa iq ya yule mtoto alipaswa kurushwa mpaka darasa la 3 huko
 
Wewe nawe hauoni hata aibu yaani unatoa ushuhuda wa kupinga uwezo wa yule dogo wakati yule dogo kuonyesha uwezo wa kukokotoa hesabu zile akiwa na umri wa miaka 6 tu Tena akiwa ana Soma darasa la awali ' halafu unajitolea mfano wewe ambaye ulikuwa umeshafika darasa la 6 tayari una experience ya kutosha tu shuleni [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Wonders shall never ends
 
Kurusha darasa hakusaidii,kitu.Watoto wenye vipaji inatakiwa Serikali iwaendeleze katika vipaji vyao.iwasomeshe kwa gharama zake .Hawa watu nchi zilizoendelea wanawatafuta Sana,Ni wachache Sana duniani wa aina hiyo.kumsomesha mtoto wa aina hiyo Ni uwekezaji utakaolipa maradufu mbeleni. Naiomba Serikali iwaalee Hawa wanasayansi wa miaka ijayo.Ndio akina Einstein Hawa.
 
Nakumbuka kuliwahi kuweko shule za watoto wenye vipaji. Ila ziliishia viongozi kujaza watoto wao wasio na vipaji.Tusirejee Zama hizo.
 
ampeleke mchepuo wa kiingereza kama kweli ana maanisha kumsaidia lakini siyo kumnunulia sare na kidumu cha maji pamoja na fagio
Uwaga wanapotea.. wazazi watazunguhswa kupewa ada. Yaani watachomesha tu. Bora dogo abaki hapo hapo ambapo wazazi wake wana weza.. hao wanasiasa hawana dogo wao wanachojali ni publicity.
 
Uwaga wanapotea.. wazazi watazunguhswa kupewa ada. Yaani watachomesha tu. Bora dogo abaki hapo hapo ambapo wazazi wake wana weza.. hao wanasiasa hawana dogo wao wanachojali ni publicity.
Dogo anaweza kuzibiwa riziki kizembe, akapelekwa elimu bure wakati kulikuwa na nafasi ya kupelekwa shule ya maana, hao wazazi wajiridhishe chap kwamba Babu tale atamsomesha wapi na kwa level ipi waandikishiane, kama ni magumashi wakatae ofa yake mapema wafadhili wa maana wapo wengi maana dogo anao uwezo
 
mi nilianza darasa la kwanza nikiwa na miaka 6, sasa huyo cha ajabu ni nini? viongozi wenu hawana kazi kwa kweli siku hizi, si kwa kushadadia upu*** huo.
 
Hichi kichwa kitapotelea kwenye mashule ya kata!

Ataenda kuharibiwa tu.
Shule yenyewe anayosoma haina madarasa wanaosomea kwenye pagala, halina madawati wanakaa kwenye mawe.

Halafu mbunge wao anasema atamgharamia masomo wakati hata kuboresha shule ameshindwa.

Hebu jiulize kuna magenius wangapi wanapotelea kwenye hayo mapagala yanayoitwa shule huko mikoani ?
 
Mi nilijua babu tale anamchukua anamtafutia shule nzuri za English Medium! Sasa anamwacha hapohapo kijijini wamroge afe?!
 
Serikali mkoani Morogoro imeagiza mtoto Charles Mathias mwenye umri wa miaka 6 arushwe darasa kutoka Chekechea hadi darasa la kwanza
Mbona kwa umri wake alitakiwa kuwa darasa la pili huyo, kwa muda mrefu watoto wamekuwa wanaanza darasa la kwana wakiwa na miaka mitano
 
Back
Top Bottom