Sijaona maaujanja ya huyo dogo ila iwapo kufanya yaliyo mbele ndio kipaji maalum hata mimi nilistahili sema tu sikupigiwa chapuo.
Stori yangu,
Hii nikweli na kweli tupu:
Wakati tukiwa darasa la Sita enzi hizo, Shule yetu ilipata mkasa wa kuwa na madarasa pungufu katika kipindi fulani hali iliyolazimisha darasa la saba na la sita kuwekwa katika chumba kimoja kikubwa tukipangiliwa katika hali ya kila darasa likiwa limepeana mgongo na lingine.
Ghafla tu siku moja, mwalimu wa Hisabati wa darasa la saba ambae pia alikuwa akitufundisha Hisabati darasa la Sita (Sisi) alitoa Jaribio kwa Darasa la saba.
Tukiwa tumetulia tuli,
Mwalimu yule wa Darasa alituamuru mimi na Mkali mwenzangu wa Darasa la sita kuwa tuunganae na La Saba tufanye Jaribio hilo,
Amini usiamini, tuliwakimbiza wale mafala shule nzima haikuamini.
Zingekuwa zama hizi si ajabu ningeonyeshwa kwenye TV.
Najua atatokea mwehu mmoja atasema hii Chai😕