Serikali yaanza kugwaya kwa 'utajiri' walioutangazia ulimwengu, Tanzania kukosa mikopo nafuu na misaada

Serikali yaanza kugwaya kwa 'utajiri' walioutangazia ulimwengu, Tanzania kukosa mikopo nafuu na misaada

Hata hizo takwimu za GDP ya Tanzania usiziamini. Katika awamu hii, takwimu nyingi ni za uwongo, ni za kupikwa.

Hiyo GDP ndiyo utajiri wenyewe. Kama tunawadanganya watu kuwa sisi ni matajiri, tunawadanganya kuwa uchumi unakua kwa 7.1% wakati ni 5% or less, ina maana hata GDP yetu inakuwa ni ya uwongo.

Kama GDP yetu ni ya uwongo, ina maana hata hiyo asilimia ya deni letu ni ya uwongo pia.

Usiulinganishe uchumi wa Kenya na Tanzania. Uchumi wa Kenya una predictability, wakati uchumi wa Tanzania hauna predictability. Haieleweki kwa namna tunavyoenda, tutaishia wapi. Unaweza kumkopesha mwenye deni ambaye unaelewa ana uhakika na anachofanya, kuliko asiye na deni ambaye haijulikani anafanya nini kwaajili ya kufika wapi.

Utawala huu umekosa maono. Wanadhani wakiwanyima watu uhuru wa kujua, watafanikiwa kwa kila jambo wanalolipanga. Ukweli ni kinyume. Anayekukopesha ili awe na uhakika, kuna wakati anahitaji taarifa toka kwa watu na taasisi huru. Kama wewe hutaki taasisi huru ziwe huru kufanya kazi, hata kama taarifa zako zitakuwa za kweli, wakati wote zitatiliwa mashaka.

Nilishangaa nilipokuwa ASEX (Australian Stock Exchange), Sydney; kuona Tanzania imekuwa listed kwenye nchi hatari kwa mitaji ya nje. Leo huwezi kupata fedha kwaajili ya kuja kuwekeza Tanzania.

Ni uwongo mkubwa kueleza kuwa tunashindwa kupata mikopo kwa sababu inakuwa na masharti tunayoyakataa. Ukiacha pesa MCC, ambaye ilihitaji kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na uhuru wa watu, hakuna msaada tuliowahi kuukataa kwa sababu ya masharti. Hata pesa ya MCC, hatukuikataa bali walitukatia watoaji baada kumnyang'anya ushindi wa wazi Maalim Seif kule Zanzibar.
Mkuu ungefuka kidogo hapo kumbe ni sisi tupo katika list hatari namna hio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fyatueni watoto, nchi hii tajiri

August 12 2016 Rais wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli alikutana na wakazi wa Dar es salaam na kuzungumza nao kuhusu maendeleo ya nchi lakini hakuacha kukumbushia lengo lake kuu la kuruhusu elimu bure kwa kila mwanafunzi.
 
Taasisi mbili tofauti zilitoa takwimu mbili todauti,
Hakuna sehemu Tanzania ilishutumiwa kupika uchumi wake,
Niletee link ya taasisi mojawapo kati ya hizo iliyoshutumu Tanzania kupika uchumi.
 
Taasisi mbili tofauti zilitoa takwimu mbili todauti,
Hakuna sehemu Tanzania ilishutumiwa kupika uchumi wake,
Niletee link ya taasisi mojawapo kati ya hizo iliyoshutumu Tanzania kupika uchumi.
Taasisi zipi hizo zilizotoa takwimu mbili tofauti?
 
Mtanzania mwenzangu uliishia darasa la ngapi? Mbona haya maneno yapo wazi na uhitaji akili ya PHD ili uweze kutambua kuwa wanapika takwimu? Unataka mpaka liandikwe neno takwimu zinapikwa?

[ World Bank contradicts Tanzania's economic growth estimates]

Nioneshe palipoandikwa kwenye hiyo link kuwa Tanzania inapika uchumi.
 
Mtanzania mwenzangu uliishia darasa la ngapi? Mbona haya maneno yapo wazi na uhitaji akili ya PHD ili uweze kutambua kuwa wanapika takwimu? Unataka mpaka liandikwe neno takwimu zinapikwa?

[ World Bank contradicts Tanzania's economic growth estimates]
Yaani hiyo taasisi ilisema uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia kadhaa alafu wewe unasema eti uchumi unapikwa,
Hizo takwimu si hizo taasisi ndio zilitoa zenyewe au,
Niletee link inayoishutumu eti kuwa Tanzania inapika uchumi sio link za makisio ya ukuaji wa uchumi.
 
Mtanzania mwenzangu uliishia darasa la ngapi? Mbona haya maneno yapo wazi na uhitaji akili ya PHD ili uweze kutambua kuwa wanapika takwimu? Unataka mpaka liandikwe neno takwimu zinapikwa?

[ World Bank contradicts Tanzania's economic growth estimates]
Tuna kizazi kiovu na kijinga sana awamu hii.
 
Back
Top Bottom