KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Kwa maana hiyo, wachina wanaukubali 'umaskini'?tunahitaji kuondoa fikra za kimasikini, kwa kuukataa umasikini hadharani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa maana hiyo, wachina wanaukubali 'umaskini'?tunahitaji kuondoa fikra za kimasikini, kwa kuukataa umasikini hadharani
Mkuu ungefuka kidogo hapo kumbe ni sisi tupo katika list hatari namna hioHata hizo takwimu za GDP ya Tanzania usiziamini. Katika awamu hii, takwimu nyingi ni za uwongo, ni za kupikwa.
Hiyo GDP ndiyo utajiri wenyewe. Kama tunawadanganya watu kuwa sisi ni matajiri, tunawadanganya kuwa uchumi unakua kwa 7.1% wakati ni 5% or less, ina maana hata GDP yetu inakuwa ni ya uwongo.
Kama GDP yetu ni ya uwongo, ina maana hata hiyo asilimia ya deni letu ni ya uwongo pia.
Usiulinganishe uchumi wa Kenya na Tanzania. Uchumi wa Kenya una predictability, wakati uchumi wa Tanzania hauna predictability. Haieleweki kwa namna tunavyoenda, tutaishia wapi. Unaweza kumkopesha mwenye deni ambaye unaelewa ana uhakika na anachofanya, kuliko asiye na deni ambaye haijulikani anafanya nini kwaajili ya kufika wapi.
Utawala huu umekosa maono. Wanadhani wakiwanyima watu uhuru wa kujua, watafanikiwa kwa kila jambo wanalolipanga. Ukweli ni kinyume. Anayekukopesha ili awe na uhakika, kuna wakati anahitaji taarifa toka kwa watu na taasisi huru. Kama wewe hutaki taasisi huru ziwe huru kufanya kazi, hata kama taarifa zako zitakuwa za kweli, wakati wote zitatiliwa mashaka.
Nilishangaa nilipokuwa ASEX (Australian Stock Exchange), Sydney; kuona Tanzania imekuwa listed kwenye nchi hatari kwa mitaji ya nje. Leo huwezi kupata fedha kwaajili ya kuja kuwekeza Tanzania.
Ni uwongo mkubwa kueleza kuwa tunashindwa kupata mikopo kwa sababu inakuwa na masharti tunayoyakataa. Ukiacha pesa MCC, ambaye ilihitaji kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na uhuru wa watu, hakuna msaada tuliowahi kuukataa kwa sababu ya masharti. Hata pesa ya MCC, hatukuikataa bali walitukatia watoaji baada kumnyang'anya ushindi wa wazi Maalim Seif kule Zanzibar.
Anahitajika afunguke zaidi ya hapaMkuu 'Inchaji' mbona hii unaifanya kuwa ngumu hivi kueleweka?
Ninahisi kama ni ujumbe mhimu unaouwasilisha hapa!
Mkuu kwa sasa kila mtanzania si karibu anadeni la $ 400+This is the right description.. hatukopesheki
Taasisi mbili tofauti zilitoa takwimu mbili todauti,
Hakuna sehemu Tanzania ilishutumiwa kupika uchumi wake,
Niletee link ya taasisi mojawapo kati ya hizo iliyoshutumu Tanzania kupika uchumi.
Taasisi zipi hizo zilizotoa takwimu mbili tofauti?Taasisi mbili tofauti zilitoa takwimu mbili todauti,
Hakuna sehemu Tanzania ilishutumiwa kupika uchumi wake,
Niletee link ya taasisi mojawapo kati ya hizo iliyoshutumu Tanzania kupika uchumi.
Nioneshe palipoandikwa kwenye hiyo link kuwa Tanzania inapika uchumi.![]()
World Bank contradicts Tanzania's economic growth estimates
Dar es Salaam. The World Bank today said Tanzania’s economy grew by 5.2 per cent in 2018, contradicting the 7 per cent growth figure announced by the government of Tanzania in June 2019. The...www.google.com
Nioneshe palipoandikwa kwenye hiyo link kuwa Tanzania inapika uchumi.
Yaani hiyo taasisi ilisema uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia kadhaa alafu wewe unasema eti uchumi unapikwa,Mtanzania mwenzangu uliishia darasa la ngapi? Mbona haya maneno yapo wazi na uhitaji akili ya PHD ili uweze kutambua kuwa wanapika takwimu? Unataka mpaka liandikwe neno takwimu zinapikwa?
[ World Bank contradicts Tanzania's economic growth estimates]
Basi nimeshindwa mimi. Jioni njemaNioneshe palipoandikwa kwenye hiyo link kuwa Tanzania inapika uchumi.
Tuna kizazi kiovu na kijinga sana awamu hii.Mtanzania mwenzangu uliishia darasa la ngapi? Mbona haya maneno yapo wazi na uhitaji akili ya PHD ili uweze kutambua kuwa wanapika takwimu? Unataka mpaka liandikwe neno takwimu zinapikwa?
[ World Bank contradicts Tanzania's economic growth estimates]
Hususan hichi kizazi ambacho kinaandika ujinga alafu Ukiwaambia wathibitishe hawawezi zaidi ya kuandika ujinga.Tuna kizazi kiovu na kijinga sana awamu hii.