Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Yaani mfano umelipwa mshahara na hio hio serikali ukaingia benki halafu unaenda benki au atm kutoa hela serikali tena wanakukata TOZO(Hapo kama bank nao huwa wanatoza unaliwa huku na huku)

Mshahara wenyewe umepigwa Kodi kabla ya kuja benki.

Naukishaitoa hiyo pesa ukamtumia mtu Kwa simu, unapigwa Tena tozo.

Ukikaa nnchale, ukichimama nnchale njomba.

Kinachoniuma zaidi hizi pesa hua hatuambiwi makusanyo Yako kiasi Gani na zinafanya Nini. Ukihoni unaambiwa hamia Burundi
 
Siamini kama Lameck na timu yake wameshindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato isipokuwa kuwabamiza wanyonge kwa gia ya tozo za miamala!

Am sure deposit kwa bank zitapungua lkn pia kbl ya sheria hiyo kuanzia pesa nyingi zitachotwa kurudi kuhifadhiwa kwenye magodoro!!
Convenience ni kama madawa ya kulevya... ngumu kuacha. Watu watavumilia tu, na baadae wataona sawa.
 
Yaani mfano umelipwa mshahara na hio hio serikali ukaingia benki halafu unaenda benki au atm kutoa hela serikali tena wanakukata TOZO(Hapo kama bank nao huwa wanatoza unaliwa huku na huku)
Na wakati huo tayari wameshakata madeni yao kwenye huo mshahara halafu wanakata na kakipande kengine ka ziada moja kwa moja kutoka bank daaahh....
 
Elimu elimu elimu! Miamala kabla ya hii ilikuwa inatozwa service charges amabzo serikali ilikuwa inapokea kodi. Sasa services charges zinaendelea na serikali itapkea huko kodi na Pia tumeongezewa tozo mpya ya serikali. Kwa hiyo kwenye muamala wako mmoja, serikali anapokea pesa mara mbili. Tuendelee, maisha nchi hii bado ni mepesi sana. Yakitushinda tutahamia Burundi.
Kwa maana hiyo ni tozo mpya au ni zilizokuwepo zimeongezwa au zimepunguzwa?kwania sudhani kama Kuna miamala yeyote iliyokuwa Haina gharama.Na kichekesho kikubwa zaidi no pale mitandao ya simu ilivyoamua kama umejiunga na huduma za kibenki hata kama una billions kwenye account Yako kama huna Salio la kutosha sms huwezi kuipata pesa Yako hata uwe na shida Gani,hata hiyo kuongeza Salio kwenye simu.Hapa ndio ninapo waona watanzania wote sisi ni wajinga.Na tutabakia kuwa maskini Kwa ujinga wetu.Kwani kufanya haya tunajihujimu wenyewe.Kisa tunalazimisha manufaa binafsi na kuzuia manufaa ya umma wa watanzania ambao kupitia Kwa ndio maendeleo ya Taifa.[emoji848]
 
Tungekuwa na elimu ya kutosha tungeandamana na kuwatoa mafisadi madarakani
chadema kwa miaka kadhaa sasa, wamejaribu sana kutoa elimu ya uraia ili wananchi wajitambue, wamejaribu sana kuitisha maandamo yanayohusu masuala mbalimbali yenye maslai mapana kwa umma ikiwemo suala la katiba mpya.

mwisho wa siku chadema haohao wanaishia kubezwa, kupuuzwa, kuzomewa, kutukanwa, kudhihakiwa, kutengenezewa propaganda nk. na haya yote yanafanywa na wananchi maskini.

acha tuisome namba, labda ipo siku akili zitatukaa sawa.
 
Back
Top Bottom