Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Sheria ni mpya na imekuja kuwaumiza zaidi wale wanaofanya transactions za viwango vya chini.

Kutoka kwenye lile jedwali, nimeona watakaoumia ni wale watakaotuma au kutoa kuanzia shilingi 5000/= mpaka 30,000/=

Mfano, kutoka shilingi 10,000/= mpaka 14,999/= wanakata.

Lakini pia, kutoka shilingi 15,000/= mpaka 19,999/= napo wanakata, wamefanya hivi makusudi wakijua watanzania wengi hivi ndivyo viwango vyao vya kutoa na kupokea pesa.

Hali ni tofauti kwa yule atakayetoa mfano kuanzia 100,000 -200,000/= huyu atakatwa mara moja pekee, wamefanya hivi wakijua hawa ni wachache na wanaojiweza.
 
Unapopewa mshahara wako serikali inakukata kodi benki inakukata tozo na serikali inakurudia tena inakukata kodi! dalili serikali imefilisika.
 
Ndio wameshindwa . . . Kama hali isingekuwa hivyo haya matozo usingeyaona wala kuyasikia.
Kweli Nchemba ni failure
 
Mimi nishaanza hilo zoezi
 
Wenzetu hamna akili?
Atm ukitoa pesa unakatwa na bank, sasa hivi serikali pia itaweka makato yake. Sasa hapo inapunguwaje?

NB
Pia Kodi na tozo ni lazima
Serikali lazima ipate mapato, hata kwa kutumia nguvu
Bhanyaning'we
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…