Omba mungu wewe sio mfanyabiashara unaezunguka mikoani na gari lako vinginevyo mikeka yote mliotandikiwa barabarani Mwigulu anafikiria kuiwekea toll charge.
Utatia akili
Kodi ni muhimu lakini tozo hapana.
Jukumu la waziri wa fedha ni kukuza uchumi, kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza furaha kwa wananchi.
Sio Mwigulu yaani ana hakikisha people are worst of today kuliko jana yao; yeye anawaza tozo tu.
Halafu wizara zingine hizo tozo wanazichezea kwa matumizi ya ovyo. Watu wametenga 500 million ya kununua majiko ya gas kwa madai ya promotion ya kubadili tabia.
Majiko yenyewe yananunuliwa kupitia kampuni moja mwenye biashara ana historia ya ufisadi na rafiki wa karibu wa godfather na baba yake waziri. Kibaya zaidi majiko yanachapa ya muuzaji sasa hiyo ni promotion ya wizara au taifa gas.
Kuna sababu wenzenu wanampenda ‘bi tozo’ kila muhuni anaangalia lake, wenyeviti wa mkoa na wilaya CCM wanaangalia kutafuna hela za miradi na vitega uchumi vya chama, mawaziri wanaangalia deals, civil servants kutafuna hela za miradi ya serikali, OC na rushwa, wafanyabiashara kukwepa kodi and so forth kila mtu na urahisi wa kupata asali iliyo mbele yake.
Mzigo wa kuendesha hiyo serikali anabebeshwa mtanzania maskini tozo kila kukicha, wengine kati yao wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku.
Hizi ndio kodi za ku support kweli.