Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Kodi zina utaratibu wake wewe kibwengo. Huo utaratibu unaitwa KANUNI ZA UTOZAJI WA KODI.

Kwa kikerewe wanaita PRINCIPLES OF TAXATION.

Na mojawapo ya kanuni ni zuio la kutoza kodi mara mbili kwenye pato lile lile.

Lakini naamini wewe haya huyajui kwa sababu elimu huna.

Unachoweza ni kuwaabudu wafalme ili upate chochote kitu ukale na wanao.

Ajira ngumu.
Huna unachoweza kunifundisha kwenye uchumi,mimi mwenyewe ni mchumi..

Kwenye Taifa lenye informal sector kubwa kama Tanzania takribani 80% staili hii ndio inatakiwa..

Kwanza Kodi ni ndogo Sana hizo ,huko kwenye formal sector Kodi zinafika karibu 30% ya kipato cha mtu..

Wewe hapo unauziana mali hamlioo Kodi,unaenda mgahawani unakula bila risiti,unamiliki ardhi hulipii harafu unaongea upumbavu..
 
Siamini kama Lameck na timu yake wameshindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato isipokuwa kuwabamiza wanyonge kwa gia ya tozo za miamala!

Am sure deposit kwa bank zitapungua lkn pia kbl ya sheria hiyo kuanzia pesa nyingi zitachotwa kurudi kuhifadhiwa kwenye magodoro!!
Makato benki kabla ya haya matozo yalikuwa makubwa sana na niliwahi lalamika humu.

Kwenye simu walisababisha watu wapunguze kutuma pesa, huku napo wanataka watu tuache


Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Yaani mfano umelipwa mshahara na hio hio serikali ukaingia benki halafu unaenda benki au atm kutoa hela serikali tena wanakukata TOZO(Hapo kama bank nao huwa wanatoza unaliwa huku na huku)
Maana zamani charges za bank zilikuwa 800 ATM, ghafla wakaweka VAT, ghafla benki zote kwa kushirikiana zikaongeza hadi 1100+VAT inafika kama 1300+

Tena Benki zikaweka kiwango tofauti na zamani ukitoa 400,000 makato yalikuwa sawa na ukitoa 50000

Leo tena serikali inaongeza tozo maana yake kutoa 400000 makato tu yatakuwa 3000

Kuna wale ambao mshahara anautoa mara 4 makato anakatwa hadi asilimia 5 ya mshahara wake

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Siamini kama Lameck na timu yake wameshindwa kubuni vyanzo vingine vya mapato isipokuwa kuwabamiza wanyonge kwa gia ya tozo za miamala!

Am sure deposit kwa bank zitapungua lkn pia kbl ya sheria hiyo kuanzia pesa nyingi zitachotwa kurudi kuhifadhiwa kwenye magodoro!!
mnyonge anaweka pesa kwenye kibubu
 
Definition ya kodi sasa imekosa maana kabisa, watu wataacha kuweka pesa zao Bank na Mabenki yataishia kukosa wateja na kuanguka, hii kodi ni ya kuua uchumi , huyu mpuuzi Mwigulu sijui walimtoa wapi? anatumia makalio yake kufikiria, wanatufanyia uhuni hawa mabozo haikubaliki kodi zimezidi, inaonekana tunafanyia kazi V8 za hawa mafisadi, itabidi kuingia mtani boss wa kweli ajulikane sasa wananchi au hawa mafisadi
 
Wanashindwa ubunifu kwenye kukusanya kodi wanakamua walipa kodi wale wale , kwa mfano maduka mengi ya mitaani hayalipi kodi kwa sababu kodi zaidi rafiki .

Na kwa sababu TRA wanapitaga mwezi wa saba tu maduka ufungwa mchana TRA wakipita maduka yanafunguliwa .

Issue hapo ni kufanya centralization kuanzia serikali ya mitaa kusajili wauza maduka kupitia afisa biashara wa kata husika . Pia kodi iwe rafiki hata ikibidi iwe flat rate kwa mfano (200,000/-) kwa mwaka kila quarter 50k . Wakiwa centralized unatumia control namba analipa moja kwa moja .


Maana kuwakwepa TRA ni kufunga duka siku za msako lakini wakifanya kutoa elimu na kuweka kodi rafiki watakusanya sana .
Hujui bila kodi mishahara hailipiki?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ko sisi wafanya biashara ndo inakula kwetu, Dah! hii nchi hii
 
Lipa Kodi wewe..

Hii sheria ilikuwa ianze mwaka wa Fedha uliopita sanjali na miamala ya simu ila mechanism zake ndio hazikuwekwa sawa..

Kwamba unaona kukatwa elfu 3 kwenye 800k au elfu 4 kwenye million 3 utapata hasara Sana si ndio?

Acheni ujinga na utoto..Tozo za miamala tumeona zilivyoleta mageuzi kwenye sekta ya Afya, barabara,maji na elimu.
Na hapo wamelenga kuwaadhibu wafanyakazi wote maana mishahara hupitia benki, hivyo hawawezi kwepa kukatwa.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hii ni Kodi Mara mbili kwa wafanyakazi kwasababu, mfanyakzinakiwekewa mshahahra, hukatwa Kodi asilimi 18, Sasa kila takapoutoa huo mshahahra akatwe Tena Kodi, huu ni UNYONYAJI wa waziwazi, I abidi tuupinge huu uamuzi.. Hawa viongizi wafikiri zaidi ili kupata vyanzo vingine vya mapato..
 
Na hapo wamelenga kuwaadhibu wafanyakazi wote maana mishahara hupitia benki, hivyo hawawezi kwepa kukatwa.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hizo ni rate mpya na infact zimepunguzwa,kwani hujui kwamba transactions zimepunguzwa kwa 43%?

Tatizo lenu Mnakurupukia mkijua ni Kodi mpya wakati ilikuwepo toka mwaka Jana.
 
How how how
Kwani pesa zetu kukaa bank hazikatwi service charges?
Tozo ya nini kwa raia wenye kipato duni?

Mzigo wa kodi na bado zinatungwa sheria kukwapua kidogo unachobakinacho. State bulgary
 
Back
Top Bottom