Wacha utahira watu wanaongezeka na huduma haziongezeki mpaka ziongezwe.
Kujengwa kwa madarasa 15,000/- kwa wakati mmoja hakumalizi tatizo la madarasa nchi nzima, bado yatahitajika tu ili mradi watu wanaendelea kuzaana, miundo mbinu ya barabara, maji, umeme, vituo vya afya hivyo hivyo.
Kama wewe una bahati ya kuishi sehemu yenye huduma zote, serikali inapambana kuhakikisha na ambao hawajabahatika kupata hizo huduma wanazipata, na wenye huduma duni wanaboreshewa.
As long as kodi na tozo zinasaidia watanzania wenzangu, nitalipa kodi kwa ufahari kabisa bila kinyongo.