Serikali yafufua mchakato ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Serikali yafufua mchakato ujenzi Bandari ya Bagamoyo

Ni kweli 10% ni ndogo kwenye maproject ya ndani kama ya kilimo ila 10% zisitusumbue sana tuna vidhibiti vyake ni kuviimarisha tu. Kuhusu bandari tuna tatizo la ukubwa wa kina kuruhusu meli kubwa pia business zone ambayo wafanyabiashara wakubwa wanaweza kuja na kukaa hata miezi 6 wakifanya mambo yao.

Sasa kuamua tuboreshe zilizopo au tujenge mpya ni suala la sisi kuangalia cost analysis, RIO na uwezo wa bandari husika kufanya kazi huku ikifanyiwa marekebisho.

Kwa sasa hatuna uwezo wa Kujenga Mpya

Karibu 23-24 Trilion zinahitajika kujenga mpya Hii ni Karibu makusanyo yetu kwa mwaka mzima ( Tukubali hatuwezi kuliko kuiuza nchi kirahisi ) Hakuna Mtu atakuja hapa akupe masharti mepesi

Cha Kufanyika kwa miaka 10 Ijayo Tujikite kwenye Chumi zalishi za Kilimo na Viwanda Vya Kuchakata mazao ( hii itatusaidia kuwa na vyakula vya kutosha na kuuza nchi jirani)


Angalia Sgr inavyotutesa kwenye bajeti hiyo ni projecy ya 13 Trilion na tuna phase 5-6 nadhani

kukubali kusubiri ni Busara mkuu Sir lanka waliona ujanja kuwahi ila now?

Tanga Iwe Bandari Pacha na Dsm Tutumie Vyema bahati hii ya kuwa na bandari pacha reli ipo TRC Klalala tu usingizi wa Porn..
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
View attachment 2315050
China (CMHI) na Oman (OIA) wamejitoa kwenye mazungumzo ya uwekezaji wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Sababu za wawekezaji hao kujitoa katika mradi huo ambao ungegharimu Tsh 23.3 trilioni hazijawekwa bayana hadi sasa. Serikali inatafuta mwekezaji mpya.

Chanzo: The Guardian
MAGUFULI na UKATILI wake kwa RAIA Wake Aliupinga MRADI HUU
 
View attachment 2315050
China (CMHI) na Oman (OIA) wamejitoa kwenye mazungumzo ya uwekezaji wa mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Sababu za wawekezaji hao kujitoa katika mradi huo ambao ungegharimu Tsh 23.3 trilioni hazijawekwa bayana hadi sasa. Serikali inatafuta mwekezaji mpya.

Chanzo: The Guardian
The African Report walishatoa uchambuzi wao makini tangu mwaka jana kwa jinsi gani itakuwa vigumu kumshawishi mchina kujenga hii bandari kipindi hiki

Kwa wafuatilaji wa mambo hili tulilitegemea
 
Tanzania: Why Bagamoyo Port deal with China is an uphill battle
 
SERIKALI imeanza mchakato wa kutafuta mwekezaji mpya kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo baada ya mazungumzo na mwekezaji wa awali kutokufikiwa mwafaka na hatimaye kujitoa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, alisema hayo jana alipoulizwa swali na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ambayo serikali imefikia katika mpango wake wa kuanza ujenzi wa bandari hiyo.

“Bandari ya Bangamoyo ni kweli muda mrefu tumeizungumza na tulikuwa tunaenda vizuri na baadhi ya watu lakini sasa hivi inaonekana yale mazungumzo hayakwenda vizuri. Mwenyewe ameamua hatoendelea kuwekeza huko,” alisema Prof. Mbarawa.

Pia alisema hata baada ya mazungumzo na mwekezaji wa awali kuvunjika, nia ya serikali ya kujenga bandari hiyo iko pale pale.

“Nia ya serikali iko pale pale kwa sababu tunajua bandari hii ya Dar es Salaam inaanza kufika mahali inashindwa uwezo wake na bandari itakayotuokoa ni hii ya Bagamoyo. Kwa hiyo hilo la serikali tunalijua na tutahakikisha tunalisimamia ili tuijenge haraka iwezekanavyo.

“Katika mpango huu, naamini tutapata wawekezaji wengine wazuri na wenye uwezo wa kujenga bandari hii ya Bagamoyo,” alisema Mbarawa.

Wakati wa Bunge la Bajeti lililomalizika Juni 30, mwaka huu, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka 2022/23, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, alisema katika kipindi cha mwaka 2021/22, serikali ilifufua majadiliano ya mradi wa Bandari na Kanda Maalum ya Bagamoyo (BSEZ) uliosimama tangu mwaka 2018.

Alisem wizara yake ndiyo ilikuwa inaratibu uendelezaji wa BSEZ unaolenga kuendana na ushindani wa biashara za usafiri wa majini pamoja na kuunganisha shughuli zingine za kiuchumi ikiwamo viwanda na utalii.

Dk. Kijaji alisema wizara hiyo ilifufua majadiliano na wawekezaji ambao ni Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) ya China na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman (OIA) ambayo awali ilikuwa inaitwa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (SGRF).

Kwa mujibu wa Kijaji, majadiliano hayo yalihusu eneo dogo la mradi wa BSEZ kwa kuendeleza eneo la hekta 3,087 kati ya hekta 9,887 ambapo unahusisha ujenzi wa bandari.

Pia alisema mpango huo ulihusisha ujenzi wa kituo cha usafirishaji kwenye eneo la hekta 887 na uendelezaji wa eneo maalum la viwanda kwenye eneo la hekta 2,200
Hatuwezi kujenga bandari,lakini tunaweza kununua magari kibao kwa ajiri ya msafara wa Raisi,wizara,mikoa,wilaya,na zingine tunashindwa kuzisimamia,zinaibwa,escrow,Richmond,pesa iliyopigwa ingeweza kujenga hii bandar
 
We jamaa huwa unashabikia ujinga tu kila mara.

Angalia hata maswali yako yasivyokuwa busara.
Jibu swali unaipanua Bandari ya Dar kuelekea wapi? kusini kuna daraja la kigamboni, mashariki kuna kambi ya navy Kigamboni, magharibi posta na hadi feri ikulu

Sasa tuambie unaipanua Bandari ya Dar kuelekea wapi?
 
60yrs after independence ilibidi tuwe na uwezo wa kusimamia shoo sisi wwnyewe. Hapo naona kuna watu wamegomewa ten pasenti zao wameamua kuvuruga mchakato.

Uwekezaji mkubwa kama huo kwanini usielekezwe kwenye bandari iliyopo ili ku utilize kiingiacho kwa 100% ili faida itakayo patikana ielekezwe huko bwagamoyo kuijenga kwa phase ...
Sidhani kama issue ni 10%. Mkataba ulikuwa na masharti magumu.
 
Ila mambo mengi ambayo mama anayawekaga hadharani kabla ya kuiva, yanabuma jamani. Hadi huruma yani. Mama aache kuweka hadharani vitu kabla hawajamaliza humo ndani. Usiri utawale.
Hata hizi reforms anazotamani ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama hasa polisi, mabadiliko ya katiba na mazingira ya kidemokrasia, sijui kama yatafika material stage.
 
Jibu swali unaipanua Bandari ya Dar kuelekea wapi? kusini kuna daraja la kigamboni, mashariki kuna kambi ya navy Kigamboni, magharibi posta na hadi feri ikulu

Sasa tuambie unaipanua Bandari ya Dar kuelekea wapi?

Maanake Kigamboni isingepaswa kuwa Makazi kama wangeangalia Miaka 1000 mbele.

Kigamboni ingekua Economic Special Zonal ya Viwanda, Jeshi, Airport, Bandari , Tafiti mbali mbali ,

Eneo Hili Sijui kwanini Tuliruhusu Makazi
 
Back
Top Bottom