Serikali yafuta mradi wa Dege Eco Village

Serikali yafuta mradi wa Dege Eco Village

Tukumbuke,
Alieuanzisha huu mradi ni mchechu kipind akiwa director pale NHC,Na aliupambania sana mradi huu uweze kuanzishwa na kweli ukajengwa

KWASASA ndie paymaster WA gavoo pale ofsin Kwa mwigulu

Hofu yangu,
Kama kweli huu mradi anatafutwa mwekezaji,

yasije kua yake Yale manispaa na ushirika, watu wanajiuzia asset za serikali kwa Bei chee.

Kwa kisingizio Cha uchakavu au gharama Kubwa za uendeshaji mradi, Kwa mgongo wa mwekezaji mpya.
 
Mama anaposafiri, ajaribu kuuza huu mradi kwa ma celebrity wa Hollywood huko.

Anapokutana na watu kama kina Mel Gibson, kina elon, isiwe tu stori za kawaida.

Mama ukikutana na mtu kama Elon mwambie aje state House ya Tanzania, mwambie njoo nina mazungumzo makubwa ya kibiashara na wewe.

Ukifanikiwa kuongea na macelebrity 50 kuna watakao potezea lakini wengine wanaweza wakaelewa.

Imagine Elon Musk amekubali kuja bongo.

Akija prezidaa mwenyewe unampokea mapokezi yenye hadhi ya ikulu, mixer matarumbeta. Mpaka ikulu, makamera kama yooote, BBC, cnn, itv macho yoote kwake(wanapenda sana sifa hawa nguruwe)

Kesho yake chukua helicopter, kisha mpe ride dege beach yooote, muonyeshe mijengo kwanza kwa juu apagawe halafu unamrudisha ikulu, unamwambia "let's talk the business now"(hapo mnaongea ukiwa unamuonyesha wale tausi na swala wa ikulu maana lazima aje na kile kitoto chake)

Wakati anawaza kuhusu deal, unamtoa mpaka kwenye pantoni(hakikisha kwenye pantoni kuna watu wachache wanaojielewa, wasije kupanda wauza madafu mwishowe wafosi kumuuzia Elon madafu)

Anavuka anakutana na chuma zinamsubiri, akipanda ni bakora mpaka dege, unamuonyesha mijengo tena, akimaliza kukagua mijengo yote unampeleka Beach.

Mkifika Beach mnakuta boti zinawasubiri, mnapanda haooo mnapepea(kama namuona vile na anavyopendaga kuvaa masuti muda wote kama mnyasa 😄 ) straight to state House ikulu, mkifika ikulu unamwambia unaona umbali kutoka ikulu mpaka mijengo ilipo, njia zote zinapitika muda wote

Nitakupa ulinzi straight kutoka jumba jeupe, halafu nitakuruhusu ujenge na kibandari kidogo dogo, kwa ajili ya kupitishia mizigo yako.

Deal done, baada ya mwaka tesla zinakua zinazalishwa kigamboni hapo.

Imagine tesla inatengenezwa Kigamboni, unashindwa vipi kumiliki gari?
Unawaona matajiri ni waduwanzi kiasi hicho?

Wana kila aina ya 1.Finest business analysts unawajua wewe. 2.Financial advisors wa kila rangi (world class) 3. Investment advisors etc etc.

Hakuna mfanyabiashara timamu atanunua hilo li white-elephant project.

Huo mradi ima ununuliwe na fisadi, au na mtakatisha pesa.

Ulivyoieleza ni as if wafanyabishara wananunua vitu for the sake of kununua/kuwa navyo. Ulishawahi jiuliza kwanini kuna watu hawana nyumba na wana uwezo wa kuwa nazo au hawana magari na wana uwezo wa kuyamiliki? Ukifikiria hili utaelewa utofauti wa mimi na wewe na wafanyabiashara.
 
Kwa hivyo zile billion 30 alizoomba na kupewa Riz1 akiwa wizara ya ardhi na makazi kwa lengo la kumalizia mradi jamaa washatafuna.

Dege village ni loss, lakini ujinga zaidi ni kuuacha, either way serikali ita cover tu bad investment iliyofanywa na NSSF.

Sasa badała ya kuacha already a large housing project ‘elements of nature’ uuchukue bure bure. Bora Samia na yeye ajichie legacy kwa kuumalizia tu, kuna faida kuliko hasara kwa kufanya hivyo.

Besides kilichobaki ni cosmetic tu, sasa sijui kwanini serikali aitaki kumalizia na kuwapa watu makazi kwa business model nyingine.
Utasikia kaununua mfanyabiashara fulani kwa pesa ya kutupa.... ni mazingira tu yanaandaliwa wakajiuzie we subiri.
 
Tuacheni kwanza sasa hivi tupo busy kuanzisha miradi mingine na kuuza prime areas kwa mgongo wa PPP's ili miaka ijayo pia tuje tuachane nayo hivyo kujiuzia sisi wenyewe real estate kwa bei ya kutupa.... (kwa mgongo wa kukomboa mradi)

Na since hakuna kuwajibika tutegemee hali kama hii kujirudia rudia kila baada ya miaka kadhaa..... Miradi ndio MIRADI (yaani pesa inapigwa kwenye miradi na sio returns kutoka kwenye miradi husika)
 
Kama NSSF wameshindwa kuendelea na mradi huu wapewe NHC wauendeleze kwa makubaliano ya kuwalipa NSSF kidogo kidogo kuliko kuutelekeza au kuuza kwa hasara.
 
Serikali imefuta ndoto ya kuendeleza mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kujiridhisha kuwa itakuwa hasara kuendelea nao.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Juni 26, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mariam Kisangi.

Mradi wa Dege Eco Village ulinzishwa kwa lengo la kuwekeza fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF, ambao ulilenga kuwa na faida zaidi kutokana na uwekezaji wake.

Mradi huo ulisimamishwa na Serikali na umekuwa na maswali mengi kutoka kwa wabunge na wananchi ikiwa inakaribia miaka tisa sasa tangu usimamishwe.

Serikali imekuwa ikielekeza kuwa inatafuta mwekezaji wa kuununua mradi huo ambao hadi mwishoni mwa 2023 ulikuwa na thamani ya Dola za Marekani 220 milioni (Sh501 bilioni).
Hongera Dau JK sasa Kizimkazi
 
Tukumbuke,
Alieuanzisha huu mradi ni mchechu kipind akiwa director pale NHC,Na aliupambania sana mradi huu uweze kuanzishwa na kweli ukajengwa

KWASASA ndie paymaster WA gavoo pale ofsin Kwa mwigulu

Hofu yangu,
Kama kweli huu mradi anatafutwa mwekezaji,

yasije kua yake Yale manispaa na ushirika, watu wanajiuzia asset za serikali kwa Bei chee.

Kwa kisingizio Cha uchakavu au gharama Kubwa za uendeshaji mradi, Kwa mgongo wa mwekezaji mpya.
Mradi ni wa Nssf. Mchechu alikuwa Nhc
 
hivi wakati wanaanzisha miradi kilometres nyingi sana kutoka kigamboni ferry. Walikuwa wanategemea watu watatoka nje kuishi?...

Sijawahi kuelewa kwa nini investment kubwa namna ile kupelekwa dege

Sometimes nahisi hata bei ya viwanja iliongezwa maana dege kwa miaka hiyo sidhani kama ilikuwa na thamani kubwa
 
Kwa hivyo zile billion 30 alizoomba na kupewa Riz1 akiwa wizara ya ardhi na makazi kwa lengo la kumalizia mradi jamaa washatafuna.

Dege village ni loss, lakini ujinga zaidi ni kuuacha, either way serikali ita cover tu bad investment iliyofanywa na NSSF.

Sasa badała ya kuacha already a large housing project ‘elements of nature’ uuchukue bure bure. Bora Samia na yeye ajichie legacy kwa kuumalizia tu, kuna faida kuliko hasara kwa kufanya hivyo.

Besides kilichobaki ni cosmetic tu, sasa sijui kwanini serikali aitaki kumalizia na kuwapa watu makazi kwa business model nyingine.
So wanau write off kwemye vitabu vya NSSF au wanafanyeje sana.Yaani mradi ukiachwa na serikali unachikaje wakati tayari kuna uwekezaji.basi wafanye tuu hata iwe madrasa
 
Huu mradi utauzwa kwa bei ya kupa kwa wahuni, wataununua na within few months/years utamalizwa na kuwa na faida kubwa. Mark hii post utaniambia.
Mkuu nami nahisi hicho ndicho kinaenda kutokea.
 
Location ya mradi huu ilikuwa ni maamuzi yasiyo sahihi.

Laiti kama mradi huu ungekuwa upo Kawe , Africana, Kunduchi n.k location kaskazini ya jiji karibu na bahari hata Bagamoyo mradi huko mwekezaji mpya angejitokeza fasta sana.

Nashangaa watoto wa mjini Jakaya Kikwete, Dr. Ramadhani Dau n.k waliweza vipi kupotea maboya wakapeleka mradi Kigamboni wa dizaini hiyo.
Hakuna cha utoto wa mjini hapo zaidi ya upigaji
Haya serikali hayo maghofu watayafanyia nini!

Ova
 
nakumbuka walikuwa wanasema eti usa anakuja kujenga mji kigamboni yaani usa miji yao kama detroit inaangamia halafu waje kujenga mji tanzagiza? hii nchi tunaongozwa na really low iq stupid people labda na sisi (wananchi) tuko hivyo pia kwa maana wanasema every country gets the leaders it deserves …
Wewe umeongea ukweli usiopingika hawa viongozi ni matokeo ya akili zetu watanzania, viongozi wanatafuna kodi zetu na rasilimali na hatuna cha kuwafanya sababu ya ujinga wetu..!!
 
Kati ya miradi ya ovyo iliyo anzishwa wakati wa Jakaya Mrisho Kikwete.
Mambo ya akina Day, Mchechu, na wenzao...
Prof. Anna Tibaijuka anasemaje kuhusu hili?
Nikimsikia anauoigia debe wakati akiwa Waziri wa Ardhi.
Mi naona busara waendeleze kuliko kuacha majengo yaoze.
Kwani huu ni mradi wa national housing au wa nssf?
 
Tunapenda sana kujifananisha na Ulaya, wakati hata vyoo hatumudu kuviosha

Hizo hela wenyewe wanataabika na dhiki na msoto wa kila aina ila wao wanakuja na maamuzi mepesi

Si watuuzie hata sisi ki apartment kimoja kimoja kuliko kuacha popo waishi humo
 
Back
Top Bottom