Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 6,750
- 14,529
Possible ila kwa mfanyabiashara wa nje kununua huo mradi anachukua risk kubwa. Na ikitokea basi ajafanya housing ‘marketing research’ ya kina kwa mazingira ya Tanzania kama lengo ni kuuza units.Utasikia kaununua mfanyabiashara fulani kwa pesa ya kutupa.... ni mazingira tu yanaandaliwa wakajiuzie we subiri.
Mfanyabiashara wa ndani mpaka sasa hakuna hiyo kampuni yenye uwezo wa ku-manage such a large property portfolio kwa sasa. Wengi wao wana vigorofa viwili vitatu wanavyopangisha, hotel na malls.
Dege village ni mradi mkubwa inataka serious business kuuchukua iliyobobea kwenye maswala ya property either kwa lengo la kuuza hizo nyumba au kupangisha.
Na kama lengo ni kupangisha ndio kabisa hiyo sio biashara ya kuendeshea nyumbani kwako wewe na mdogo wako. Unahitaji ofisi nzima ya administration na upkeep ya majengo.
Serikali inapoteza muda tu, wamalizie mradi na kuwapa moja ya taasisi zake (not NHC) ku-manage as rentals au hata kwa kuuza units if possible.
Vinginevyo kwa mfanyabiashara wa ki Tanzania kujiingiza kwenye huo mradi ni kujitafutia pressure tu.
Kwa vyovyote vile atakae nunua huo mradi lazima afanye revaluation of costs ambazo NSSF wali-overestimate za ardhi, contracts na kadhalika. Kwa hivyo book value ya serikali waliyo nayo aina mantiki ni lazima uuzwe kwa bei ya chini tofauti na thamani iliyopo kwenye vitabu vya NSSF (ndio madhara ya ufisadi).
Ni hivi busara ni serikali kuuchukua mradi kumalizia na kuangalia kwa msingi wa kuchochea uchumi, low housing project kusaidia watumishi wa umma na vijana wengine wenye ajira na shida ya makazi kwa kuweka rent zinazofanana na eneo and life goes on.
Simuoni huyo mwekezaji wa ndani ambae ana experience ya ku-manage such a large portfolio, ata kama ni ufisadi utakuwa wa kijinga na sidhani kama kuna bank inaweza fund such a purchase Tanzania kwa mfanyabiashara it’s just too risky.