Serikali yafuta mradi wa Dege Eco Village

Tukumbuke,
Alieuanzisha huu mradi ni mchechu kipind akiwa director pale NHC,Na aliupambania sana mradi huu uweze kuanzishwa na kweli ukajengwa

KWASASA ndie paymaster WA gavoo pale ofsin Kwa mwigulu

Hofu yangu,
Kama kweli huu mradi anatafutwa mwekezaji,

yasije kua yake Yale manispaa na ushirika, watu wanajiuzia asset za serikali kwa Bei chee.

Kwa kisingizio Cha uchakavu au gharama Kubwa za uendeshaji mradi, Kwa mgongo wa mwekezaji mpya.
 
Unawaona matajiri ni waduwanzi kiasi hicho?

Wana kila aina ya 1.Finest business analysts unawajua wewe. 2.Financial advisors wa kila rangi (world class) 3. Investment advisors etc etc.

Hakuna mfanyabiashara timamu atanunua hilo li white-elephant project.

Huo mradi ima ununuliwe na fisadi, au na mtakatisha pesa.

Ulivyoieleza ni as if wafanyabishara wananunua vitu for the sake of kununua/kuwa navyo. Ulishawahi jiuliza kwanini kuna watu hawana nyumba na wana uwezo wa kuwa nazo au hawana magari na wana uwezo wa kuyamiliki? Ukifikiria hili utaelewa utofauti wa mimi na wewe na wafanyabiashara.
 
Utasikia kaununua mfanyabiashara fulani kwa pesa ya kutupa.... ni mazingira tu yanaandaliwa wakajiuzie we subiri.
 
Tuacheni kwanza sasa hivi tupo busy kuanzisha miradi mingine na kuuza prime areas kwa mgongo wa PPP's ili miaka ijayo pia tuje tuachane nayo hivyo kujiuzia sisi wenyewe real estate kwa bei ya kutupa.... (kwa mgongo wa kukomboa mradi)

Na since hakuna kuwajibika tutegemee hali kama hii kujirudia rudia kila baada ya miaka kadhaa..... Miradi ndio MIRADI (yaani pesa inapigwa kwenye miradi na sio returns kutoka kwenye miradi husika)
 
Kama NSSF wameshindwa kuendelea na mradi huu wapewe NHC wauendeleze kwa makubaliano ya kuwalipa NSSF kidogo kidogo kuliko kuutelekeza au kuuza kwa hasara.
 
Hongera Dau JK sasa Kizimkazi
 
Mradi ni wa Nssf. Mchechu alikuwa Nhc
 
hivi wakati wanaanzisha miradi kilometres nyingi sana kutoka kigamboni ferry. Walikuwa wanategemea watu watatoka nje kuishi?...

Sijawahi kuelewa kwa nini investment kubwa namna ile kupelekwa dege

Sometimes nahisi hata bei ya viwanja iliongezwa maana dege kwa miaka hiyo sidhani kama ilikuwa na thamani kubwa
 
So wanau write off kwemye vitabu vya NSSF au wanafanyeje sana.Yaani mradi ukiachwa na serikali unachikaje wakati tayari kuna uwekezaji.basi wafanye tuu hata iwe madrasa
 
Huu mradi utauzwa kwa bei ya kupa kwa wahuni, wataununua na within few months/years utamalizwa na kuwa na faida kubwa. Mark hii post utaniambia.
Mkuu nami nahisi hicho ndicho kinaenda kutokea.
 
Hakuna cha utoto wa mjini hapo zaidi ya upigaji
Haya serikali hayo maghofu watayafanyia nini!

Ova
 
Wewe umeongea ukweli usiopingika hawa viongozi ni matokeo ya akili zetu watanzania, viongozi wanatafuna kodi zetu na rasilimali na hatuna cha kuwafanya sababu ya ujinga wetu..!!
 
Kwani huu ni mradi wa national housing au wa nssf?
 
Tunapenda sana kujifananisha na Ulaya, wakati hata vyoo hatumudu kuviosha

Hizo hela wenyewe wanataabika na dhiki na msoto wa kila aina ila wao wanakuja na maamuzi mepesi

Si watuuzie hata sisi ki apartment kimoja kimoja kuliko kuacha popo waishi humo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…