Serikali yafuta mradi wa Dege Eco Village

Utasikia kaununua mfanyabiashara fulani kwa pesa ya kutupa.... ni mazingira tu yanaandaliwa wakajiuzie we subiri.
Possible ila kwa mfanyabiashara wa nje kununua huo mradi anachukua risk kubwa. Na ikitokea basi ajafanya housing ‘marketing research’ ya kina kwa mazingira ya Tanzania kama lengo ni kuuza units.

Mfanyabiashara wa ndani mpaka sasa hakuna hiyo kampuni yenye uwezo wa ku-manage such a large property portfolio kwa sasa. Wengi wao wana vigorofa viwili vitatu wanavyopangisha, hotel na malls.

Dege village ni mradi mkubwa inataka serious business kuuchukua iliyobobea kwenye maswala ya property either kwa lengo la kuuza hizo nyumba au kupangisha.

Na kama lengo ni kupangisha ndio kabisa hiyo sio biashara ya kuendeshea nyumbani kwako wewe na mdogo wako. Unahitaji ofisi nzima ya administration na upkeep ya majengo.

Serikali inapoteza muda tu, wamalizie mradi na kuwapa moja ya taasisi zake (not NHC) ku-manage as rentals au hata kwa kuuza units if possible.

Vinginevyo kwa mfanyabiashara wa ki Tanzania kujiingiza kwenye huo mradi ni kujitafutia pressure tu.

Kwa vyovyote vile atakae nunua huo mradi lazima afanye revaluation of costs ambazo NSSF wali-overestimate za ardhi, contracts na kadhalika. Kwa hivyo book value ya serikali waliyo nayo aina mantiki ni lazima uuzwe kwa bei ya chini tofauti na thamani iliyopo kwenye vitabu vya NSSF (ndio madhara ya ufisadi).

Ni hivi busara ni serikali kuuchukua mradi kumalizia na kuangalia kwa msingi wa kuchochea uchumi, low housing project kusaidia watumishi wa umma na vijana wengine wenye ajira na shida ya makazi kwa kuweka rent zinazofanana na eneo and life goes on.

Simuoni huyo mwekezaji wa ndani ambae ana experience ya ku-manage such a large portfolio, ata kama ni ufisadi utakuwa wa kijinga na sidhani kama kuna bank inaweza fund such a purchase Tanzania kwa mfanyabiashara it’s just too risky.
 
Wapuz sana hawa

Ova
 
So wanau write off kwemye vitabu vya NSSF au wanafanyeje sana.Yaani mradi ukiachwa na serikali unachikaje wakati tayari kuna uwekezaji.basi wafanye tuu hata iwe madrasa
I am not suggesting that.

Muhimu kwanza ni kufanya ‘revaluation’ ya hiyo asset kwenye vitabu vya NSSF na mmbia wake wote wachukue equal losses kwa walichowekeza.

Serikali imalizie mradi na kuchukua share based na gharama ya hela zake ilizoweka.

Mradi ukiisha ipewe taasisi ya serikali ku-manage sio kuanzisha taasisi mpya tena.

Faida ya mwisho wa mwaka inagawanywa by shares, that way NSSF inakuwa na income na huyo mmbia wake mwingine analipwa kama ulikuwa mkopo au anapata shares yake.

Kuliko kuwa na asset ambayo ipo kwenye vitabu tu aizalishi as intended na kuongeza risk za short term solvency kwa NSSF.

I am not saying that’s the only solution, ila something as to be done, maana upuuzi zaidi ni kuacha hali iendelee kama ilivyo.
 
Kuacha njiani mradi wa ujenzi ambao upo zaidi ya asilimia 50 ni hasara mara mbili.

Ushauri wangu
1. Mradi umalizwe lakini ufanywe kuwa low cost housing project kutoka kwente ''luxurious residential apartment/houseing scheme''.
Wanaweza kufanya hivi kwa kufanya mabadiliko ya kimahitaji hasa kwenye finishings works.

2. Mradi uuzwe kwa kampuni ama mtu anayeweza kuuendeleza.

Hela za mafao hizo.
 
Aseeh mara ya kwanza nilipita hapo ghorofa ni nyingi nikamuuliza mtu nilikuwa naye tulibaki kuduwaa Ila pale ni mabillion yamepotea

Na jamaa anajibu kirahisi tuu haoni haja daah,
Ccm oyeeeeee
Nimemaliza kusoma kitabu kinaitwa " I am the state" mimi ni dola
 
Utetezi wa ajabu kwenye hela na maisha ya watu , kwanza mradi ulifeli kabla ya watu kuhamia huko dodoma leo kuhamia dodoma unataka iwe sababu ya mhimu mradi kufeli
 
Nashauri wamalize mradi na wafanye kiwe chuo kikuu kama ilivyo MIT.. yale majengo yatumiwe kama hostel sawa wajenge majengo ya kusomea na maabara za kisasa. Kiwe world class university
 
Aseeh mara ya kwanza nilipita hapo ghorofa ni nyingi nikamuuliza mtu nilikuwa naye tulibaki kuduwaa Ila pale ni mabillion yamepotea

Na jamaa anajibu kirahisi tuu haoni haja daah,
Hapo hakuna hela iliyopotea katika angle ya uchumi.
 
Tatizo lilishatokea, njia ya kunusuru huo upotevu kwa sasa ni upi?
 
Hii nchi huwa inachezewa sana halafu bado wanakwambia hawana Hela!
 
Hivi kule dege walitegemea ataenda kukaa nani

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…