Serikali yafuta shughuli za Nanenane mwaka 2021

Serikali yafuta shughuli za Nanenane mwaka 2021

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Tanzania, Profesa Adolf Mkenda ametangaza kusitisha shughuli zote za maonyesho ya Nanenane zilizokuwa zifanyike mwaka huu.

Akizungumza leo Jumatano Februari 10 2021 bungeni Jijini Dodoma, Profesa Mkenda amesema fedha zote za umma bila kujali ni za wizara gani, zisitumike kwenye shughuli hizo.

“Lakini nawasiliana na wizara nyingine na wadau kwamba fedha hizo tuzielekeze katika kuendeleza shughuli za ugani,” amesema waziri huyo.

Amesema hivi karibuni walikuwa na kikao na maofisa kilimo wa mikoa, walijadiliana kwa kiasi kikubwa kuhusu changamoto ambazo baadhi zinahitaji wawezeshwe kifedha ili wazitatue.

“Tuna maofisa tumewaajiri hadi ngazi ya kata kwa ajili ya kilimo, lakini changamoto tulizozizungumza wakati ule zinahitaji na sisi kuwawezesha vilevile, kwa sababu hatuna haja ya kuweka ofisa kule lakini hatujatengeneza wao kuwasaidia watu,” amesema.

Amesema wako wakulima wanasema hawajui wanapataje huduma za ugani hivyo anawasiliana na wizara nyingine ambazo ni wadau kwenye shughuli hizo kwamba fedha yote iliyokuwa itumike kwa ajili ya shughuli za Nanenane mwaka huu ipelekwe katika shughuli za kuimarisha ugani.
 
Na Sabasaba? Hakutakuwa na maonesho? Au kwa sababu hii "inaingiza" haina shida? By the way, badala Sabasaba kuwa kituonesho ya maonesho ya ubunifu wa products mbalimbali imegeuka kuwa gulio kuuubwa.
 
Maflgufuki akisema pesa zote ziende kujenga miundo mbinu mfano ya umwagiliaji asiajiri mnalalamika akisema basi tuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya kilimo maafisa ugani ili pesa iliyokuwa iende kujenga miundombinu ya umwgiliaji wasikose ajira mnalakamika hivi nyie ngedere mnataka nini?

amAsante Mu gu kuwapiga pepo Chadema chini uchaguzi mkuu
Deni la Taifa ni Tsh 59 Tilion,
Miradi yote tunajenga kwa fedha zetu.
 
Haya ni matokeo ya uwizi mkubwa wa fedha za umma kuhalalisha uchafuzi wa 28/10/2020. Deni la taifa pekee toka Oktoba 2020 limekuwa kwa asilimia 7 na hivi kufikia trilioni 59. Na bado, mengi yatafuata. Kunapokuwa watawala dhalimu, taifa huugua.
 
Magufuli akisema pesa zote ziende kujenga miundo mbinu mfano ya umwagiliaji asiajiri mnalalamika akisema basi tuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya kilimo maafisa ugani ili pesa iliyokuwa iende kujenga miundombinu ya umwgiliaji wasikose ajira mnalakamika hivi nyie ngedere mnataka nini?

Asante Mungu kuwapiga pepo Chadema chini uchaguzi mkuu
Wacha kelele, utafanyaje maonesho na hiki kirusi kipya cha Corona kinavinjari mitaa yetu?
 
Magufuli akisema pesa zote ziende kujenga miundo mbinu mfano ya umwagiliaji asiajiri mnalalamika akisema basi tuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya kilimo maafisa ugani ili pesa iliyokuwa iende kujenga miundombinu ya umwgiliaji wasikose ajira mnalakamika hivi nyie ngedere mnataka nini?

Asante Mungu kuwapiga pepo Chadema chini uchaguzi mkuu
Waliomtangulia waliweza kufanya vyote, ajira zilikuwepo, barabara zilijengwa na Sherehe za kitaifa ziliazimishwa kama kawaida
 
Duuuh! Hili ni pigo kubwa kwangu!! nilikuwa natarajia kuingia nane nane na kuku elfu moja! mara kwa mara sera za Tanzania zimekuwa zikinikwamisha na kunirudisha nyuma kiuchumi!! miaka Kama minne. Serikali ilikuja na sera ya leseni ya kitaifa kwasisi wafanyabiashara ya ng'ombe!

Watu tulifilisiwa na hii sera, ngombe zetu zilizuiliwa minadani na machinjioni!! Watu tulikata mitaji!!

Leo tema mmekuja na kuzuia n 88.

Nikama vile serikali mmekuwa mnatumika na shetani kunididimiza kiuchimi!! Sera za Tanzania sio rafiki kwangu!
 
Magufuli akisema pesa zote ziende kujenga miundo mbinu mfano ya umwagiliaji asiajiri mnalalamika akisema basi tuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya kilimo maafisa ugani ili pesa iliyokuwa iende kujenga miundombinu ya umwgiliaji wasikose ajira mnalakamika hivi nyie ngedere mnataka nini?

Asante Mungu kuwapiga pepo Chadema chini uchaguzi mkuu
Mwambie apunguze na zile posho za kikao cha chama a.k.a bunge la vigeregere kodi zinapotea bure kule.
 
Sasa ifike muda vyama vya wakulima na waendeshe shughuli hizi kwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka wizara husika. Serikali haina shamba na si mfanyabiashara wa mazao ya kilimo!!

Serikali kutotumia fedha zake kwenye maonesho haya isiwe ndio kukwama kwa yeyote mwingine!! Kwani serikali ikishindwa kuongezea wafanyakazi wake mshahara, mtu binafsi nae asiongeze?? (Nawaza kwa sauti).
 
Hi sio sawa!! Serikali ingeounguza matumizi yake. Ili na sisi wanannchi wa kawaida tupate!! pesa yote imebaki serikalini 88 ndio imekuwa ikibust kidogo biashara za watu!! sasa mnazuia maonyosho hayo!!
 
Magufuli akisema pesa zote ziende kujenga miundo mbinu mfano ya umwagiliaji asiajiri mnalalamika akisema basi tuajiri vijana waliomaliza mafunzo ya kilimo maafisa ugani ili pesa iliyokuwa iende kujenga miundombinu ya umwgiliaji wasikose ajira mnalakamika hivi nyie ngedere mnataka nini?

Asante Mungu kuwapiga pepo Chadema chini uchaguzi mkuu
Nchi hii haina utaratibu wala mipango. Hata kesho hatujui kitasemwa au kufanywa nini. Ni Magufulu akisema ..............

What a failed state. Nchi ya watu 60M😭😭😭😭😭😭😭
 
Nilikua nimetega projects zangu za promotions nasubiria mpunga tu kumbe miamba iko majalala.
 
Back
Top Bottom