Serikali yafuta shughuli za Nanenane mwaka 2021

Kama tukio la mwezi August tangazo limetoka leo, basi maana yake ni kwamba hakutakuwa na sherere yoyote ya kitaifa kwa mwaka huu.
 
Hivi ni nani huwa wanatunga sera hapa nchini? nahisi Kama vile hawajui uhalisia wa maisha ya Mtanzania!!

Mara muwabane wafanyabiashara Mara wafanyakazi muwapunje mishahara!
2 mara muwanyime sitahiki zao
3 mara hamna kupandisha watumishi madaraja kazini
4 Leo mumekuja kuwabana wafanyabiashara wadogo kwa kuzuia maonyosho ya 88!
Watunga sera mmtumwa na shetani??
 
Mpunga umekata tunafanya kuhamisha magoli tu.
Acha kuishi kinafiki mkuu muda utaendelea kuongeana kuwaumbua PESA HAKUNA[emoji23][emoji23]
 
Kwa sasa nawaelewa watu/ wafanyabiashara wanaohamisha mitaji/ biashara zao nje ya nchi.

Kuwekeza Tanzania ni kama 'kubet', mda wowote 'mkeka' unachanika!
 
Kwani taarifa inadai kuajiri maafisa ughani, mbona unaropoka tu, tengeneza hoja?
 
Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Waziri wa kilimo Profesa Mkenda katika mahojiano na ITV leo.

MY TAKE:
Naipongeza kauli hii kama ina nia dhabiti. Kwani maonesho ya nane nane hayajawahi kuleta tija kwa mkulima wa jembe na mfugaji mdogo kule vijijini ambao ndio walio wengi
 
sio mbaya Japo ,kilimo kinahitaji Sana haya maonyesho.
 
Tuseme tu serikali haina pesa, lakini kiuhalisia maonyesho ya Nanenane ndio sehemu pekee ambapo mkulima alipaswa kwenda kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya kilimo.

Angeweza kujua masuala ya utafiti mpya wa kilimo, mbegu bora, masuala ya mbolea, pembejeo za kilimo, viatilifu na mambo kama hayo. Pia kuonyesha aina mbalimbali za mazao yatokanayo na kilimo na ufugaji.

Ilipaswa kuwa fursa nzuri kwa mkulima kujifunza na kubadilishana uzoefu na wenzake. Lakini kibaya ni kwamba baadhi ya maofisa wa serikali wakageuza kuwa fursa ya kwenda kupiga pesa na kugawana posho!
 
Kwasababu ya chadema ndo mana mishahara ya watumishi wa umma haijaongezwa kwa miaka yote mitano unadhani nchi ipo vitand
 
Hii habari mbaya Sana kwangu, Nina kanga 700 nategemea nanenane kuwa nao 1500 ili niwauze, nimekuwa nikifaidika na maonesha haya,navuna mpunga wangu sasa hawa jamaa wamenikata kichwa kabisa, Aise hawa binadamu walioshiba wanakula viyoyozi maofisini na kulipana per diem hivi hawajui kabisa kama kuna watu tunahangaika siku kwa siku tupate mlo? Mungu anawaona , Malipo ni hapa hapa duniani, kuna siku yatawapata Magumu yanamna ,poa tu ngoja tusukume gurudumu hili la Maisha lakini safari bado ndefu tutaonana huko mbele
 
Wewe nawe ni kima tu...ebu tupe mradi wa umwagiliaji chini ya Pombe?
 
Pumbavu kabisa wewe kwani fedha za sherehe zinatosha kuajiri mtu?
 
Pesa ya maonyesho itaajiri wangapi? Kuna mambo haya make any sense ndiyo maana watu wanahoji...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…