Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

wananchi wa ngorongoro walishahamishiwa msomera huko Tanga kitambo sana na maisha yao ni mazuri kweli kweli...hakuna watu tena wanaoishi hifadhini ngorongoro....

wananchi wa msomera sasa sasahivi,
wanashiriki zoezi la kujiandikisha na uchaguzi wa serikali za mitaa na kujipanga na uchaguzi mkuu mwaka ujao....

nadhani Prof.Shuvji yuko nyuma kidogo kwenye uelewa na ufahamu wa hatua za kisheria zilizofikiwa kuhusu jambo hili muhumu sana. huko mbona tulishatoka kitambo sana ndrugu zangu?

na sasa tuko mbele sana kimaendeleo huko msomera. ukimbizi ni dhana tu labda ya prof. kutaka kuonyesha upande wake kwenye jambo hili, ambalo limekwisha kwa amani
 
Wamebakia thimba fisi na tembo sio?
 
Ni wakoloni wapya wa zama hizi.Wanaigawa nchi upya kimipaka kama mwaka 1886 kule Berlin/scramble for Ngorongoro.
Hayana akili hayo

Yanapigwa lawsuits za ajabu....

Na kizuri Wamasai wote wamegoma...hata wakimwaga askari,hakuna la maana watafanya
 
Kwahiyo Sasa hivi nikitaka kuenda wilaya ya ngorongoro nisema nataka kuenda wapi Ili nieleweke naenda wapi?

Au niseme nataka kuenda vitalu vya Dubai?
 
Nilisema humu na bado naendelea kusema. Hii kasi aliyokuja nayo, iko siku itafika. Kila unapokanyaga unaambiwa hili eneo huruhusiwi kufika, ni la nchi/mtu fulani ndani ya TZ. Tuendelee kuwachekea tu, tutakuja kushtuka too late.
nchi iko salama wala usiwe na shaka ndugu..

ni maboresho tena yana nia njema kabisa nafikiri kikubwa ni elimu ndio iko chini juu ya hili swala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…