Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Hatuendo popoto
1724162345462.jpg
 
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.View attachment 3074956
wananchi wa ngorongoro walishahamishiwa msomera huko Tanga kitambo sana na maisha yao ni mazuri kweli kweli...hakuna watu tena wanaoishi hifadhini ngorongoro....

wananchi wa msomera sasa sasahivi,
wanashiriki zoezi la kujiandikisha na uchaguzi wa serikali za mitaa na kujipanga na uchaguzi mkuu mwaka ujao....

nadhani Prof.Shuvji yuko nyuma kidogo kwenye uelewa na ufahamu wa hatua za kisheria zilizofikiwa kuhusu jambo hili muhumu sana. huko mbona tulishatoka kitambo sana ndrugu zangu?

na sasa tuko mbele sana kimaendeleo huko msomera. ukimbizi ni dhana tu labda ya prof. kutaka kuonyesha upande wake kwenye jambo hili, ambalo limekwisha kwa amani :pulpTRAVOLTA:
 
Wamebakia thimba fisi na tembo sio?
 
Serikali kupitia kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinachotoa ruhusa kwa mamlaka za Serikali kufanya mgawanyo wa Halmshauri za Wilaya;

Imetoa AMRI rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024; ili kufuta baadhi ya maeneo ya kiutawala kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27 Novemba, 2024.

Amri hii rasmi sasa inafuta Kata, Vijiji na Vitongoji katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo; Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo.

Katika Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro pekee, kupitia AMRI hii, Serikali imezifuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96.

Garatwa,
Dar es Salaam, Tanzania.
20 Agosti, 2024.
View attachment 3074791
Kwahiyo Sasa hivi nikitaka kuenda wilaya ya ngorongoro nisema nataka kuenda wapi Ili nieleweke naenda wapi?

Au niseme nataka kuenda vitalu vya Dubai?
 
Nilisema humu na bado naendelea kusema. Hii kasi aliyokuja nayo, iko siku itafika. Kila unapokanyaga unaambiwa hili eneo huruhusiwi kufika, ni la nchi/mtu fulani ndani ya TZ. Tuendelee kuwachekea tu, tutakuja kushtuka too late.
nchi iko salama wala usiwe na shaka ndugu..

ni maboresho tena yana nia njema kabisa nafikiri kikubwa ni elimu ndio iko chini juu ya hili swala
 
Back
Top Bottom