Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Naunga mkono hoja. Ila pia mazingira ya siasa za Tanzania yamebadilika sana hiki kipindi cha miaka 9. Vyama vya upinzani vinapata tabu sana na kipindi kile vijana hasa wa vyuo walikuwa proud kuwa upinzani, ila sasa wote wamegeuka machawa kutafuta uteuzi au favor.
Hutazami mambo kwa usahihi..

Uchawa upo na umekuwepo miaka yote..

Na kwa taarifa yako, opposition ya sasa hivi/miaka hii is stronger than ya wakati ule..

Ushahidi ni matukio haya unayoyaona.

Mfano;

1. Iwapo opposition ni weak, unadhani John P. Magufuli na serikali/CCM yake kati ya 2016 - 2020 angefanya aliyofanya..?

✍️ Mathalani, alitumia rungu la dola kinyume cha katiba na sheria kupiga marufuku shughuli za kisiasa za vyama vingine ukiacha CCM..

✍️Alitumia siasa chafu kuhonga mapesa na vyeo vya kiserikali baadhi ya wapinzani wake waliokuwa tishio kwa sera na mipango yake..

✍️Kuchafua na kuharibu kwa makusudi uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 kwa sababu yeye na chama chake walijua watashindwa vibaya..

✍️Kuchafua na kuuharibu kwa makusudi uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa kuwa yeye na chama chake walikuwa wameshindwa vibaya sana. Mpaka leo hii hakuna matokeo rasmi ya kura za u - Rais. Unajua hilo..??

2. Haya yanayofanywa kibabe na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na CCM yake ni mwendelezo wa hofu na ubabe uleule wa kijinga toka enzi za marehemu Magufuli. Hii ni dalili ya hofu na woga wa kushindwa tu. Kama hakuna upinzani kama unavyofikiri, haya yasingekuwepo..!

Lakini unajua nini?

Kama hataki kuamini na kuelewa kuwa upinzani now is stronger than before, subiri utaona matokeo yake very soon..

Wenzio kwa sasa (Samia na CCM yake) wako so desperate kutafuta pesa hata kama zitatoka kwa shetani ili mradi wanadhani kuwa pesa hizo zitawasaidia na kuwakikishia kubaki madarakani dhidi ya wapinzani wao..

Mambo ya Ngorongoro na Loliondo ni mkakati wa CCM wa kujipatia pesa haramu toka kwa mabeberu wa kiarabu yanayoitaka ardhi hiyo na rasrimali zake zote..

Na tukizubaa tu, Serengeti National Park nayo itakwenda aidha kwa waarabu tena au kwa wachina...!!
 
Kwa hiyo ndiyo kusema hiyo Wilaya yote kwa sasa ni mali ya Waarabu!! Sasa kulikuwa na sababu gani ya kupigania Uhuru!!

Tungeendelea tu kutawaliwa basi, kama viongozi wenyewe wana tabia za akina Chifu Mangungo.
Kinachowasukuma viongozi wetu kufanya mambo ya ajabu bila kujali ni tamaa ya fedha!

Fedha ni fedheha! Na yote ni kwa ajili ya familia zao.

Je ni faida gani tunapata kwa kuuza wilaya nzima ya Ngorongoro? Kwa nini biashara hii haramu inafanywa kwa kificho?

Mpaka sasa serikali haijatueleza fedha zinazojenga vile vibanda vya Msomera zinatoka wapi na zimewekwa katika bajeti ya wizara gani?
 
Naililia nchi yangu Jamhuri ya Tanganyika.😡😡😡😡😡😡
 

Attachments

  • FB_IMG_1702085740919.jpg
    FB_IMG_1702085740919.jpg
    1.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1702085740919.jpg
    FB_IMG_1702085740919.jpg
    1.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1702085740919.jpg
    FB_IMG_1702085740919.jpg
    1.6 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1702085740919.jpg
    FB_IMG_1702085740919.jpg
    1.6 KB · Views: 1
Back
Top Bottom