Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Mwaka juzi nilifanya utalii wa ndani mbuga ya Saadani, ilikuwa shida kuwaona wanyama! Wanyama ni wachache sana.

Kingine kinachokwaza utalii ni tabia ya company za utalii kutumia local tour guide ili mradi anajua kuongea tu kiingereza kibovu na ujanja ujanja anaenda na mtalii.. akigingwa na swali kuhusu nature hajui, aina za miti na scintif name hajui, anajua kuelezea wanyama tu huku scientic name zake hajui. Kwa mtalii ana boreka.
 
Pamoja na gharama za viingilio, hizi zipo rasmi na mtalii huwa amejiandaa navyo... lakini pia kwa raia 'uchawa' ni mwingi na kero kubwa.

Tunawaombaomba sana, tukiona mzungu tu ni fursa... hata embe tu tutamuuzia 5000/- lengo ni kumpiga tu.

Wale vijana wa kupandisha watalii mlimani ni hatari tupu, mzungu ananyonyolewa kila kona na hana cha kufanya.
 
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena..

Hata kama sijui hapana aisee , kupanda mlima milioni 300 huu utakuwa ni uongo brother

unashangaa mil 300, the latest i know even hio ela ni ndogo saaahv!

mskilize aliepanda mlima mwenyewe, be sure that hio hela saaahv ni more than mil 300 atleast 400M for now or 500M
 
Kuna mengi mkuu, ila natumaini Dr Ndumbaro atatumia ule umakini wake kutatua changamoto za hii sekta.

Inabidi kuweza kuongeza thamani ya vivutio vyetu bila kuharibu/kupoteza/kufifisha uhalisia wake (authenticity). Magoroto Forest Estate, ni mfano mzuri wa kuongeza thamani bila kuharibu uhalisia. Wamefanya kazi nzuri sana pale.

sawa sawa kabisa
 
Kama kawaida Mabongoman hawana ufahamu mwingi>>Mtalii siyo mtu tajiri kama mnavyofikiri. Watalii wengi wanafunzi na wafanyakazi wa kawaida sana ili wao wafike huku wamejidunduliza vidola kwa kusave hata miaka miwili sasa Mabongoman wakiwaona watalii wanawaona matajiri kweli wakizani jamaa wanamipesa ,huwa inatokea kama Abramovich, Will smith mara chache kuja kutalii

ubunifu,ubunifu ubunifu Mabongoman hata bonus hakuna
 
yes na lengo lisiwe kurudisha watalii waliokwishakuja.

bali kuongeza wengine zaidi.
Tunaweza pia kuwarudisha kwa kuwaonyesha bado kuna vivutio vingine hawajatembelea, au kuwapa motisha ya kuongeza muda wa kuwa nchini. Kila siku wanayoongeza wanafanya matumizi nchini. Unatakiwa uwape motisha ya kuendelea kufanya matumizi, aidha kwa kulipia huduma au kufanya manunuzi.
 
yah,maana ukiishaboresha kila kitu ni wao ndio watahitaji kubaki au kurudi kwa mara nyingine.
 
Mimi nafikiri tungetoa unafuu kwa vifaa hivi ili kusudi wajasiriamali wengi wajitokeze wanunue yale macamping equipment. Magari ili utalii wa ndani ukue

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwetu sio hivyo hao wageni ndio walikuepo kwenye hiyo biashara wanashinikiza mazingira magumu kwa wanaoanza ili wabaki wenyewe kwenye soko hawajui kuwa ubora na ufanisi wa kazi unakua kwa kiwango cha chini mno...
 
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena.

Maana yake ni kuwa sisi Tanzania kila mwaka tunategemea watalii wapya, hatuwezi kuwatuliza(keep) ama kuwahakikishia watalii wa zamani kurudi tena Tanzania kufurahia vivutio vyetu vya utalii.

Retention yetu ya watalii ni chini ya 20%. Maana yake ukuaji wa utalii wetu bado una changamoto kubwa sana.

Nikitoa my personal experience, nilitembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza, tukakutana na tour guide wa kike, wote tuliofika pale siku hiyo hatuwezi kutamani kurudi tena, mimi na wenzangu siku hiyo tulikuwa disappointed, siwezi kutamani hata kwa bunduki kutembelea tena hiyo hifadhi.

Nimewahi kwenda Serengeti National park mara 2, kwa pale niko tayari kurudi maana mategemeo yangu yalikamilika kwa zaidi ya 80%.

Je, unadhani ni kwanini watalii wa nje hawarudi tena baada ya kutembelea Tanzania.

=============

ARUSHA
Wamiliki wa makampuni ya watalii, wadau ya sekta ya utalii nchini Tanzania ikiwemo wahifadhi wastaafu wameelezea sababu tano zinazowafanya watalii waliotembelea nchini wasirudi kwa mara ya pili.

Sekta ya utalii inachangia asilimia 17.5 ya pato la Taifa pia asilimia 25 ya mapato ya fedha zote za kigeni nchini ambapo kwa sasa inatembelewa na watalii milioni 1.2. Serikali inalenga mpaka 2025, Tanzania inatakiwa kupokea angalau watalii milioni tano na kukuza mapato ya fedha za kigeni kutokana na utalii mpaka dola bilioni 6 kutoka dola bilioni 2.5 kwa mwaka.

Wakiongea na gazeti la Citizen, washika dau wameainisha sababu kama gharama kubwa ambazo watalii wanaingia wakitembelea Tanzania, huduma kwa wateja isiyoridhisha kwenye mahoteli na watoa huduma wengine.

Kulingana na wao, miundombinu mibovu, makampuni ya watalii yanayoshindwa kutimiza ahadi zao walizowapa wateja na wafanyakazi kukosa uadilifu ikiwemo kuwalangua watalii. Akiongea na Citizen, mhifadhi mstaafu, Erastus Lufungilo ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Burudika amesema watalii walilazimika kutumia fedha zaidi kutokana na kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kutoka kwenye nchi zao ikiwemo Ulaya na Marekani kuja Tanzania. "Utalii ni gharama, hii ni kwasababu kutembelea Tanzania kwasasa ni gharama kuliko kutembelea Kenya au Afrika kusini" Alieleza.

Kulingana na yeye, makampuni mengi ya utalii yana mapungufu katika kuendesha biashara na kuongoza watalii kunakosababishwa na upungufu wa wafanyakazi wataalam na kusababisha matatizo.

"Baadhi ya waongoza watalii wanachukua hela kutoka kwa watalii lakini chaajabu huwezi kuwakuta uwanja wa ndege kuwapokea watalii. Hata wakijitokeza kuwapokea ambao wanalipwa hela nyingi, hawatoi huduma bora" Alisema Lufungilo

Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha waongoza watalii(TTGA) amesema wingi wa kodi zinazotozwa kwa makampuni ya watalii na waongoza watalii imesababisha watalii kutomudu gharama kwa watalii wengi ambao wanashindwa kuitembelea tena Tanzania.

"Kuna kodi nyingi sana na kila siku kodi mpya zinatangazwa na kuwalazimu wamiliki kupandisha gharama ili kupata faida. Alisema ndugu Mollel. Alihoji kwanini baadhi ya mashrika ya ndege kuchaji dola 500 zaidi kwa tiketi safari kutoka Ulaya kuja Tanzania ikilinganishwa na viwanja vingine vya ndege kwenye nchi za jirani.

Akifungua mkutano wa mwaka kwa wahariri na waandishi waandamizi kwenye sekta ya utalii, katibu mkuu wizara ya Utalii na maliasili, Aloyce Nzuki amewataka wanahabari wafikiri kwa makini kwanini asilimia 20 pekee ya watalii wanaitembelea tena Tanzania.

Dr. Nzuki amevitaka vyombo vya habari nchini kutoa taswira nzuri ya nchi kabla na baada ya watalii kutembelea Tanzania

View attachment 1666303
NGOJA KWANZA WATUMISHI WA WIZARA WAMALIZE KUKARIRI KURASA 260 ZA ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA HA MAPINDUZI KISHA TUTAANGALIA NAMNA YA KUTATUA TATIZO
 
"..Nikitoa my personal experience, nilitembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza, tukakutana na tour guide wa kike, wote tuliofika pale siku hiyo hatuwezi kutamani kurudi tena, mimi na wenzangu siku hiyo tulikuwa disappointed, siwezi kutamani hata kwa bunduki kutembelea tena hiyo hifadhi..."

Mkuu hujatufafanulia hapa kulikuwa na tatizo gani au ni huyu tour guide wa kike ndo alikuwa tatizo au alikuwa peke yake tu hifadhi nzima au ilikuwa vipi hasa??!!
 
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena.

Maana yake ni kuwa sisi Tanzania kila mwaka tunategemea watalii wapya, hatuwezi kuwatuliza(keep) ama kuwahakikishia watalii wa zamani kurudi tena Tanzania kufurahia vivutio vyetu vya utalii.

Retention yetu ya watalii ni chini ya 20%. Maana yake ukuaji wa utalii wetu bado una changamoto kubwa sana.

Nikitoa my personal experience, nilitembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza, tukakutana na tour guide wa kike, wote tuliofika pale siku hiyo hatuwezi kutamani kurudi tena, mimi na wenzangu siku hiyo tulikuwa disappointed, siwezi kutamani hata kwa bunduki kutembelea tena hiyo hifadhi.

Nimewahi kwenda Serengeti National park mara 2, kwa pale niko tayari kurudi maana mategemeo yangu yalikamilika kwa zaidi ya 80%.

Je, unadhani ni kwanini watalii wa nje hawarudi tena baada ya kutembelea Tanzania.

=============

ARUSHA
Wamiliki wa makampuni ya watalii, wadau ya sekta ya utalii nchini Tanzania ikiwemo wahifadhi wastaafu wameelezea sababu tano zinazowafanya watalii waliotembelea nchini wasirudi kwa mara ya pili.

Sekta ya utalii inachangia asilimia 17.5 ya pato la Taifa pia asilimia 25 ya mapato ya fedha zote za kigeni nchini ambapo kwa sasa inatembelewa na watalii milioni 1.2. Serikali inalenga mpaka 2025, Tanzania inatakiwa kupokea angalau watalii milioni tano na kukuza mapato ya fedha za kigeni kutokana na utalii mpaka dola bilioni 6 kutoka dola bilioni 2.5 kwa mwaka.

Wakiongea na gazeti la Citizen, washika dau wameainisha sababu kama gharama kubwa ambazo watalii wanaingia wakitembelea Tanzania, huduma kwa wateja isiyoridhisha kwenye mahoteli na watoa huduma wengine.

Kulingana na wao, miundombinu mibovu, makampuni ya watalii yanayoshindwa kutimiza ahadi zao walizowapa wateja na wafanyakazi kukosa uadilifu ikiwemo kuwalangua watalii. Akiongea na Citizen, mhifadhi mstaafu, Erastus Lufungilo ambae kwa sasa ni mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Burudika amesema watalii walilazimika kutumia fedha zaidi kutokana na kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kutoka kwenye nchi zao ikiwemo Ulaya na Marekani kuja Tanzania. "Utalii ni gharama, hii ni kwasababu kutembelea Tanzania kwasasa ni gharama kuliko kutembelea Kenya au Afrika kusini" Alieleza.

Kulingana na yeye, makampuni mengi ya utalii yana mapungufu katika kuendesha biashara na kuongoza watalii kunakosababishwa na upungufu wa wafanyakazi wataalam na kusababisha matatizo.

"Baadhi ya waongoza watalii wanachukua hela kutoka kwa watalii lakini chaajabu huwezi kuwakuta uwanja wa ndege kuwapokea watalii. Hata wakijitokeza kuwapokea ambao wanalipwa hela nyingi, hawatoi huduma bora" Alisema Lufungilo

Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha waongoza watalii(TTGA) amesema wingi wa kodi zinazotozwa kwa makampuni ya watalii na waongoza watalii imesababisha watalii kutomudu gharama kwa watalii wengi ambao wanashindwa kuitembelea tena Tanzania.

"Kuna kodi nyingi sana na kila siku kodi mpya zinatangazwa na kuwalazimu wamiliki kupandisha gharama ili kupata faida. Alisema ndugu Mollel. Alihoji kwanini baadhi ya mashrika ya ndege kuchaji dola 500 zaidi kwa tiketi safari kutoka Ulaya kuja Tanzania ikilinganishwa na viwanja vingine vya ndege kwenye nchi za jirani.

Akifungua mkutano wa mwaka kwa wahariri na waandishi waandamizi kwenye sekta ya utalii, katibu mkuu wizara ya Utalii na maliasili, Aloyce Nzuki amewataka wanahabari wafikiri kwa makini kwanini asilimia 20 pekee ya watalii wanaitembelea tena Tanzania.

Dr. Nzuki amevitaka vyombo vya habari nchini kutoa taswira nzuri ya nchi kabla na baada ya watalii kutembelea Tanzania

View attachment 1666303
Huduma mbovu zinazotegemea maelekezo kutoka juu ni chanzo kikubwa cha kupoteza watalii.
 
Nashauri tujifunze kwa nchi zinazofanya vizuri kama Dubai, Malaysia, Misiri, Hongkong n.k. hata ikiwezekana waje watufundishe kwa muda ili na sisi kufikia pale walipofikia.
Hivi kweli matatizo hamuyajui? Gharama kubwa, standards za chini, huduma mbovu, barabara mbovu, waongozaji lugha gongana; kiwango chetu kiko chini sana, ukilinganisha hata na Kenya tu hapa jirani! Wahusika wawe na elimu ya kutosha, wapeleke nje waone wenzao wanafanyaje; punguza uswahili uswahili! Simpo!
 
yes na lengo lisiwe kurudisha watalii waliokwishakuja.

bali kuongeza wengine zaidi.
Wewe unaonekana bado una elimu ndogo juu ya biashara. Nakufunza jambo, nalo ni, katika biashara yoyote unafanya, wekeza akili yako, ufahamu wako, jitihada zako, na mbinu nyingi kwa mteja ambaye umeshamuhudumia sababu huyu atakupa mrejesho wa biashara yako na wapi unapowaya. Ila ukianza tabia ya kuwapuuza wateja wa awali sababu unatarajia wapya, hapo ndipo unaharibu biashara na kufeli mapema.
 
utalii sio duka la mchele mangi.

leo hii tuna mpango wa kuweka cable za kupandia kilimanjaro,unadhani target ni wale ambao wameshakuja tayari kwamba warudi!!!!sio hivyo.ndio maana tunatangaza pia utalii na mandege yananunuliwa,haina haja ya yote haya kama mtu aliishafika bongo na anapajua.

mtalii kurudi,inaweza changiwa na huduma na maandalizi ya mwenyeji,lakini bado kurudi kwake liko mikononi mwake zaidi yako wewe.
 
ili kuvutia watalii wa kigeni zaidi, nadhani tozo za kuingia hifadhi ingepunguzwa ili wengi wao waweze kumudu na kuongeza mapato ya nchi.
The lower the price at good service level, the higher the number of customers joining the service.
 
Back
Top Bottom