Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Kuna baadhi ya vitu lazima tuweke black and white....ingawaje ukweli unauma sometimes... maendeleo hayana chama
 
Mkuu, swala siyo gharama tu, swala ni thamani ya gharama anazolipa. Ukiacha vivutio kama hifadhi za Serengeti, Ngorongoro, Gombe na Mlima Kilimanjaro, au visiwa vya Zanzibar, Mafia, nk...vivutio vingine huduma zake ni za chini sana...
Atleast this can be the reason, nlikua nataka kuskia watu wanaolilia bei
 
Sasa hizo kodi kubwa wanazotoza pesa hizo huwa wanazipeleka wapi, mbona kila siku afadhali ya jana maisha hayajulikani?
 
atleast this can be the reason, nlikua nataka kuskia watu wanaolilia bei
Kuna mengi mkuu, ila natumaini Dr Ndumbaro atatumia ule umakini wake kutatua changamoto za hii sekta.

Inabidi kuweza kuongeza thamani ya vivutio vyetu bila kuharibu/kupoteza/kufifisha uhalisia wake (authenticity). Magoroto Forest Estate, ni mfano mzuri wa kuongeza thamani bila kuharibu uhalisia. Wamefanya kazi nzuri sana pale.
 
Siku zote nasemaga waTZ hawajui jinsi gani ilivyo expensive kwa mzungu kuja kutalii. Na wazungu wana kitu wanaita bucket list na mara nyingi uwa hawarudii sehemu unless wale wanofanya vitu kama uwindaji au michezo flani flani.

Wengi inawachukua miaka kadhaa kukusanya pesa za kuja kutalii halafu utegemee aje kila mwaka, no way.
 
Nashauri tujifunze kwa nchi zinazofanya vizuri kama Dubai, Malaysia, Misiri, Hongkong n.k. hata ikiwezekana waje watufundishe kwa muda ili na sisi kufikia pale walipofikia.
Dubai na Egypt zinafanya vizuri kwa sababu zipo karibu sana na nchi za Ulaya hivyo ni cheap na mtu hahitaji kuchukua likizo ndefu kwenda Dubai/Egypt au Morocco.

Niliwahi ishi nchi fulani EU, wafanya kazi wenzangu walikuwaga wanenda weekend mara Dubai mara Morocco na J3 wanaamkia kazini, ni kama kwenda Spain au Portugal, ndege ni rahisi, hotels bei rahisi na inachukua kama masaa ma2 au ma3 kufika.
 
Watalii hawarudi kwa sababu zifuatazo:-
1. Gharama za utalii sio rafiki mfano kupanda mlima Kilimanjaro mtalii mmoja ni usd 1000 . Bila malazi ya hoteli alikoshukia na chakula na unakuja kila mtalii anapanda mlima kea gharama tofauti mwisho watalii wakikutana na kujadiliana wanaomba watanzania ni watu wasio waaminifu..
Sekta ya utalii imejaa wababaishaji sana na matapeli. Mtu analipia trip akifika bongo anaambiwa mara kuna iki hujalipia mara kile kimepanda bei so mzungu ni mtu anaishi kwa buget na sio kubahatisha hivyo akiondoka anaondoka na sura mbaya ya sekta ya utalii na taifa. Wangeingia online wasome malalamiko ya watalii na wayafanyie kazi kwanza ndio waje walalamike
 
Watalii hawarudi kwa sababu zifuatazo:-
1. Gharama za utalii sio rafiki mfano kupanda mlima Kilimanjaro mtalii mmoja ni usd 1000 . Bila malazi ya hoteli alikoshukia na chakula na unakuja kila mtalii anapanda mlima kea gharama tofauti mwisho watalii wakikutana na kujadiliana wanaomba watanzania ni watu wasio waaminifu...
Kutokana na hoja namba 4, tunapaswa kuongeza kodi zaidi kwa watalii hawa?
 
ili kuvutia watalii wa kigeni zaidi, nadhani tozo za kuingia hifadhi ingepunguzwa ili wengi wao waweze kumudu na kuongeza mapato ya nchi.
Ukishusha tozo idadi ya watalii makapuku itaongezeka, sisi tunataka watalii viwango ambao kwao pesa siyo Shida
 
Good observation: sehemu kubwa ya matatizo yapo kwenye (a) huduma mbovu na (b) tozo kubwa

Makampuni mengi yanayohudumia watalii huwa hayatoi huduma nzuri kwa watalii. Wanatumia tour guides vijana ambao hawakutayarishwa kujua tabia za watalii, badala yake wao wanawachukulia watalii kama watu wenzao wa kijiweni ilihali wao wametokea mataifa tofauti yenye tamaduni tofauti. Tour guide mzuri ni yule anayeza tour kwa kutwawelewa atenja wake kwa kuwaliza wametoka wapi, ni nini kilichowavutia kuja kuangalia Tanzania. Inatakwa serikali ianzishe mafunzo ya mtu kupata leseni ya kuwa tour guide.

Mahoteli, makampuni ya tours na serikali huweka tozo kubwa sana kwa watalii kama vile watalii hao wana kisima cha pesa. Kuna watalii ambao hubana matumizi ili waweze kutunza pesa za kutosha kuja kutembelea mbuga zetu. Kuwachaji pesa nyingi bila kipimo hadi kufikia wao kuishiwa kabisa huwakatisha tamaa wasipende kurudi Tanzania tena.
 
No one reason ni gharama
Kodi kubwa
hakuna anayeelewa,mtalii anajichanga haswa kuja huko kutalii almost mishahara yake miwili au mitatu anateketeza akishakuja arudi tena kufanya nini?hawana utajiri wowote wengi wao wabangaizaji tu,wachache sana matajiri
 
Hapo kwenye Ruaha naamini wapo hovyo kabisa ! ni mbuga ambyo kweli hawana wanyama
Mm nimetembelea mbuga nying sn ila serenget sijawah fika kinachofanya watalii wasirud ni management mbovu mfano ukienda ruaha mapokez ni pa kiswahili vyoo ni vya kiswahili refreshment ndio kabisa uswahili swahili tu afu mbuga kubwa wanyama wachache yaan mnatafuta wanyama kwa mbinde chui .simba ndio balaa hawapatikan kuna haja ya kujenga good management wagen wasipate usumbufu mbuga pekee ambayo angalau niliifurahia ni manyara ipo poa sn japo na penyewe pana changamoto yake ilaa kwa serenget naamin ipo juu maana ndio best of all in africa
 
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena...
Customer Service.
 
1. most places ukishaenda mara moja ukirudi mara mbili inakua sio adventure tena, hata kama ni dubai ukishaenda mara moja ukienda the second time it doesnt add up...
Hata kama sijui hapana aisee , kupanda mlima milioni 300 huu utakuwa ni uongo brother
 
wapelekeni buguruni karibu na kimboka kuna SGR inajengwa inavutia sana na yale mavyuma ya blue.
 
Nilienda pia saadani Pangani aisee sitamani kule mana nilikuwa naoneshwa kwa mbali sana mfano simba yule ila Ngorongoro ni best kwa kweli serengeti sijafika
 
Back
Top Bottom