Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Nadhani tunatangaza vitu tunavyoita vivutio lakini hata wenyewe sisi watz havituvutii......

Unajua ili uweze kumvuta mtalii ni vema ujue nae ni mwanadamu kama sisi, na anavutiwa na vile vitu tunavyoweza vutiwa navyo pia.

Inabidi tuongeze creativity ya kuweka vivutio ambavyo hata watu wa ndani pia wapo interested. Hebu tazama Malaysia kwa mfano, kule kuna wanawake wazuri, chakula kizuri, hoteli safi, culture profile ya kueleweka. Sasa mzungu anapokwenda kule inakuwa ni sehemu ya kutalii kweli kweli na kufurahia maisha.

Wazungu nao ni watu kama sisi, wanapokuja wanataja kuenjoy maisha ambayo sisi pia tuna enjoy sio kuwa igizia maisha ambayo hatuyaishi. Imagine mzungu anakuja unamuwekea ngoma za asili, hivi hizo ndizo ngoma unazosikiliza kila siku miaka hii?!

So hebu tutafiti kwa wenzetu Dubai na Malaysia........ Tujifunze then tuestablish.
Watanzania tunazidi kuwa wajinga kwa kila kitu mpaka tunatia aibu tunachojua ni kusifu, kusifiana na kupongezana kwa mambo ya kijinga kabisa. Miaka zaidi ya miwili iliyopita Waaustralia wengi sana walikuja kwa ndege zao lakini sidhani amerudi hata mmoja ingawa waliahidi kutangaza vivutio walivyovikuta na wao wenyewe kurudi tena. Wakaja Waczech toka Czech Republic wakafuata Warusi na Wachina wakingojewa lakini matokeo ya ujio huo yatakuwa yaleyale ya kutokomea. Viongozi wetu walitakiwa wajue kuwa hizi ni Promotional Tours ambazo zimeandaliwa na Tour Operators wa huko wenye uzoefu wa kupeleka Watalii kote duniani lakini wakiwa hapa wanapokelewa kwa ngoma za jadi lakini huduma mbovu. Kivutio nambari wani nchi yoyote ni wananchi wa nchi hiyo kwa Tanzania ndo ifuate Serengeti, big five, Ngorongoro, Kilimanjaro, Zanzibar nk kwa mfano dunia nzimà inajua Watanzania hawana furaha wapowapo tu.

Kenya ni nchi ndogo yenye vivutio vichache lakini wanaopata Watalii wengi zaidi kuliko Tanzania kuwa sababu wamewekeza sana kwenye miundombinu ya Utalii kama Hotels na Restaurant ambazo zinatumika na wenyeji pia maana wanajua lughà nyingi na wana furaha.

Mtalii yeyote atataka baada ya kutembelea vivutio ambayo nchini kwake havipo, akae na Mbongo wabadilishane mawazo lakini hapa kwetu Hotel aliyofikia ni wazungu tupu kama kule kwao labda watumishi wa Hotel ambao hata lughà hawajui.

Watalii wengi wanaokuja hapa ni wafanyabiashara ambao wangeweza kusaidia kuwainua wa kwetu au kuingia nao ubia au kuwafundisha mbinu bora za kufanya biashara lakini Mushi na Mangi wanakutana kwenye Bar ya Mrema kula nyamachoma na mtori.
 
Asante kwa kutupa feedback,ndio maana tunahitaji watalii wa ndani pia ili watusaidie kuboresha sekta ya utalii...
Binafsi sikuwahi kufikiria hili suala!
Nilitembelea Mikumi na Ruaha sijawahi fikira kurudi tena pande hizo ndani ya uhai wangu!

Ninadhani ni kwa sababu kama vile zina kuendesha kiasili wafanyakazi kipindi hicho wana tabasam tu ila wamechoka wana mawazo mengi kama vile wanadhulumiwa! Ila kwenye customer care uwongo bado tuna ka safari karefu!
Niombe Mungu anisaidie ni tamani kurudi tena mwaka huu maana ni miaka karibia ya 7 imepita!
 
hivi hawa watu wanafikiriaje? wakifanya dola 100 hapa kupanda mlima tutapata malaki na malaki ya watalii kwa mwaka hivyo bei kubwa sio kupata sana tuangalie na wingi wa watu pia
 
Unajua mzungu kutalii kurudia nchi moja mara mbili itachukua muda sana hawezi kuja mwaka huu na mwakan aje tena kwasababu wale huwa wanazunguka nchi nyingi kipindi cha likizo,

Kwa mfano wanaofanya kazi labda za kuajiriwa kwenye makampuni ndani ya mshahara wao huwa kuna kiasi ambacho wanakatwa na kampuni mfano kama unalipwa labda 1.5m kwa mwezi basi watakukata % kadhaa kwenye hiyo hela, kwanini wanakukata?

%Kubwa ya watalii wanaokuja kutalii baadhi ya nchi huwa wanasafirishwa na kampuni zao kwa zile % walizokiwa wanakatwa kila mwezi kwenye mshahara, japo hii sio lazma ukitaka wakukate ili baada ya likizo uchague nchi unayotaka kwenda kupumzika wakat wa likizo ila pia kama hutak basi hawakati chochote,

Sasa kutokana na hali hii huwa inapelekea wengi kuzunguka nchi mbalimbali hawawezi kurudia nchi moja mfululizo wachache sana huwa wanafanya hivo,

Lakin pia katika hili la gharama tz iko juu sana pamoja na kwamba ina mbuga nzuri lakin upande wa gharama iangaliwe maana wakat mwingine mtalii anakuja anataman arudi lakin akifikilia gharama na usumbufu uliozungumziwa hapo kuombwa pesa n.k huwa wanaona bora tuzungukie nchi zingine tu huko Tanzania tutajipanga tena,

Sasa wasitafte mchawi nani wachawi sisi wenyewe tu, unajikuta unalipia vitu vingi kwa gharama kubwa sana sijui kiingilio, chakula, malazi, usafiri, hapo hujakutana watakao kuomba pesa, simu, camera, yan mzungu akitoka hapo anajiuliza nimekuja kutalii au kutoa msaada? Hawezi kurudi kabisa huyo....
 
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena.

Maana yake ni kuwa sisi Tanzania kila mwaka tunategemea watalii wapya, hatuwezi kuwatuliza(keep) ama kuwahakikishia watalii wa zamani kurudi tena Tanzania kufurahia vivutio vyetu vya utalii.

Retention yetu ya watalii ni chini ya 20%. Maana yake ukuaji wa utalii wetu bado una changamoto kubwa sana.

Nikitoa my personal experience, nilitembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza, tukakutana na tour guide wa kike, wote tuliofika pale siku hiyo hatuwezi kutamani kurudi tena, mimi na wenzangu siku hiyo tulikuwa disappointed, siwezi kutamani hata kwa bunduki kutembelea tena hiyo hifadhi.

Nimewahi kwenda Serengeti National park mara 2, kwa pale niko tayari kurudi maana mategemeo yangu yalikamilika kwa zaidi ya 80%.

Je, unadhani ni kwanini watalii wa nje hawarudi tena baada ya kutembelea Tanzania.
Ni vema kutambua hao tunaowaita watalii zamani walijulikana kama Explorer ingawa sasa kuna tofauti kidogo. Kawaida mtalii/mzungu ktk miaka 3au4 anapanga nchi za kutembelea , hivyo basi akiisha tembelea eneo moja kati ya hayo 3 au 4 usitarajie atarudi kwako kabla ya kumaliza mzunguko wa maeneo aliyopanga kuyatembelea, hivyo ataendelea kuexplore sehemu nyingine ili notebook yake iweze kuonyesha ametembelea nchi au mabara mengi duniani.

Mkakati wa Tanzania ujielekeze ktk kuboresha huduma za utalii na kupunguza gharama za utalii ili wale wanaokuja wakirudi makwao wawambie wengine kuwa Tanzania Ni sehemu mzuri ya kutembelea.

Pia iwe Ni lazima kwa sehemu zinazohudumia watalii kuweka bango linaloonyesha bei ya huduma zao (price list). sasa hivi sehemu hizo muhudumu ana bei yake kwa mtalii, meneja na dereva nao wanazo bei zao na kampuni husika nayo bei yake, mwishowe sector ya utalii ndiyo inaumizwa!?
 
Juzi hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii alikutana na wafanyakazi wa wizara hiyo katika kujadili masuala ya utalii na changamoto zake alikiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudu tena, wakishakuja mara moja wengi wao huwa hawarudi tena.

Maana yake ni kuwa sisi Tanzania kila mwaka tunategemea watalii wapya, hatuwezi kuwatuliza(keep) ama kuwahakikishia watalii wa zamani kurudi tena Tanzania kufurahia vivutio vyetu vya utalii.

Retention yetu ya watalii ni chini ya 20%. Maana yake ukuaji wa utalii wetu bado una changamoto kubwa sana.

Nikitoa my personal experience, nilitembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza, tukakutana na tour guide wa kike, wote tuliofika pale siku hiyo hatuwezi kutamani kurudi tena, mimi na wenzangu siku hiyo tulikuwa disappointed, siwezi kutamani hata kwa bunduki kutembelea tena hiyo hifadhi.

Nimewahi kwenda Serengeti National park mara 2, kwa pale niko tayari kurudi maana mategemeo yangu yalikamilika kwa zaidi ya 80%.

Je, unadhani ni kwanini watalii wa nje hawarudi tena baada ya kutembelea Tanzania.
Watanzania ni wapole ila siyo wakarimu
 
Mimi niliwahi kuilalamikia hifadhi ya serengeti hapa!! Pale Nabi gate kwanza watumishi wanawadharau watanzania,ukiondoa madereva wa tours,mfano nilikuta pale watu wana tatizo la mfumo wa kulipia ada,kadi yao ya mastercard ilikuwa haisomi,sasa kuna askari mmoja yupo pale,ni mnene na mrefu,akawa anawagombeza wale watu kuwa waondoke eneo lile haraka kwa kuwa eti aliwaletea dalali wa kuwalipia kwa bei karibu mara mbili ya ile ya halali wakakataa,yule askari badala ya kuwatafutia suluhisho alikuwa akiwagombeza na kuwakejeli hadi nikaona huruma nikaingilia na kuwalipia kwa mkopo,angalau siku hizi nabi wanapokea Mpesa,ila kwenye geti la Laobare(ngorongoro) bado wanangangania Mastercard tu,hiyo inafanya iwe vigumu kwa watanzania wa kawaida ku enjoy mbuga zetu,hizi mbuga zetu hazina mvuto kwa wazawa kabisa,kwa kuwa mfumo ume wa favour wageni kwa asilimia zote
Hili limekuwa tatizo kubwa. Kuna hifadhi moja kubwa. Wageni wanakuja pesa kiasi fulan ila wanaishia getini na malalamiko kibao.

Embu tujaribu kushusha tozo ziko juu sana sana sana
 
Hapo suluhisho ni kuwauliza hao watalii kuwa kwanini hawarudi ? Wakisha taja sababu za kutokurudi then mamlaka husika kuzifanyia kazi .
 
Mimi niliwahi kuilalamikia hifadhi ya serengeti hapa!! Pale Nabi gate kwanza watumishi wanawadharau watanzania,ukiondoa madereva wa tours,mfano nilikuta pale watu wana tatizo la mfumo wa kulipia ada,kadi yao ya mastercard ilikuwa haisomi,sasa kuna askari mmoja yupo pale,ni mnene na mrefu,akawa anawagombeza wale watu kuwa waondoke eneo lile haraka kwa kuwa eti aliwaletea dalali wa kuwalipia kwa bei karibu mara mbili ya ile ya halali wakakataa,yule askari badala ya kuwatafutia suluhisho alikuwa akiwagombeza na kuwakejeli hadi nikaona huruma nikaingilia na kuwalipia kwa mkopo,angalau siku hizi nabi wanapokea Mpesa,ila kwenye geti la Laobare(ngorongoro) bado wanangangania Mastercard tu,hiyo inafanya iwe vigumu kwa watanzania wa kawaida ku enjoy mbuga zetu,hizi mbuga zetu hazina mvuto kwa wazawa kabisa,kwa kuwa mfumo ume wa favour wageni kwa asilimia zote
Yaan focus yao kubwa ni wageni wa nje. Maana ndio wanaleta pesa nyingi. Wanachoshindwa kufaham ni kuwa wageni wa nje ni so unriliable. Huwez sema next yr atarudi.
Badala ya kujiongeza. Watu wanakaa kimazoea.

Customer service ni mbovu. Yaaan mtu anakuwa na kiburi flani hivi.

Lazima wabadilike or utalii utadorora kwakweli.
 
Hakuna kitu kisichohitaji ubunifu na akili.

Kama huduma za utalii zingekuwa contracted, nina hakika sekta binafsi ingefanya vizuri maradufu ya jinsi mambo yalivyo leo.

Serikali yetu hakuna inachokiweza. Kwenye biashara na uchumi, ndiyo sifuri kabisa. Ushahidi upo, jinsi mashirika mbalimbali na viwanda namna vilivyokufa.

Na mahali ambapo Rais Magufuli amefeli kabisa, ni kufikiria Serikali, tena Serikali ya Tanzania inaweza kufanya biashara. Na akitaka aangamize kabisa uchumi mdogo uliopo aendelee kuweka shughuli za biashara kuwa controlled na Serikali.

Tanzania, pamoja na vivutio vyote tunavyotamba navyo, kwa mwaka mapato ni $3 billion. Misri mapiramidi yanaingiza $5 billion, Jiji la Paris $80 billion.

Serikali inafikiria utalii ni mikia tu ya fisi, pundamilia na tembo! Wanaofanya utalii, wanataka ku-enjoy na relaxation, sasa ukishaona mikia ya pundamilia, ndiyo basi. Hakuna cha ziada.

Tunazidiwa na nchi kama Thailand inayofanya sex tourism. Utajiri mkubwa hapa Duniani ni akili, siyo madini wala twiga na fisi. Ukiwa na akili halafu ukawa na madini, gas, wanyamapori, unapaa. Lakini hata ukapewa vyote hivyo, kama huna akili, utaendelea kudumu kwenye ndoa ya umaskini.

Nilienda Serengeti kwa kupitia lango la kule Magu, ni hovyo kabisa. Huyo anayeandikisha mnapoingia unadhani amesoma shule ya ngumbaru. Hata uwezo wa kuandika ni hoi. Mtu mwenyewe ni goigoi, hajua thamani ya muda na wala hajitambui. Pale langoni tu, unaanza kukatishwa tamaa.

Tuna wanyama na mbuga lakini hatuna watu wa kuvipa thamani vitu hivyo!!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo siyo kingine..
Ni gharama kubwa ya kutembelea mbuga zetu.
Ningeshauri wizara ya maliasili ipunguze gharama ya kuingia ngorongoro, Serengeti, lake manyara, tarangire, kilimanjaro na arusha national park cos ndio mbuga zinatembelewa sana bila kupunguza msitarajie mabadiliko yeyote.
 
Mkurugenzi wa Burudika Tourist Company, Erastus Lufungilo ametaja baadhi ya sababu zinazopelekea watalii kutorudi Tanzania mara baada ya kutembelea mara moja

Kwanza amesema hakuna ndege ya moja kwa moja kutoka Ulaya au Marekani kuja Tanzania hali inayofanya gharama kwa watalii hao kuongezeka. Hii ni sababu watalii wengi hutembelea Kenya au Afrika Kusini kwa kuwa kuna ndege za moja kwa moja

Kwa upande wa huduma kwa wateja amesema baadhi ya wanaoongoza watalii hupokea fedha za nyingi za watalii lakini hutoa huduma mbovu ikiwemo kutoenda Uwanja wa Ndege kuwapokea

Aidha masuala ya kodi za kila mara zimeripotiwa kuwa sababu pia na watu wa kada hiyo kukosa weledi

===
Owners of tourist firms and stakeholders of the tourism sector in Tanzania, including retired conservationists, have cited five major factors that make tourists visiting the country not to pay a second visit.

The sector contributes 17.5 percent of gross domestic product (GDP) and as well contributes 25 percent of forex earnings to the country, which is currently visited by 1.2 million tourists. The government targets that by 2025, the country should have receive at least some five million tourists to grow forex earnings to $6 billion from $2.5 billion per annum.

Talking to The Citizen recently, the stakeholders pointed out such factors as high costs incurred by tourists when visiting Tanzania, unsatisfying customer experience in the hands of hoteliers and other service providers.

According to them, poor infrastructure, a number of tourist companies that fail to meet the promises they give to their customers and lack of professionalism by workers, some of who, in a number of occasions, defraud tourist. Speaking to The Citizen, retired conservationist Erastus Lufungulo, who is now the director of Burudika Tourist Company, said tourists were forced to spend more because there were no direct flights from the source countries including Europe and the US to Tanzania.

“Our tourism is costly. This is because vising the country now is more expensive than vising Kenya or South Africa,” he revealed.

According to him, a multitude of tourist companies that lack the merits of operating the business and tour guiding lacks professional workers, causing problems.

“Some tour guides take money from tourists, but strangely you can’t find them at airports to receive the tourists. Even when they show up to receive tourists, who pay them a lot of money, they do not provide quality services to them,” Mr Lufungulo said.

For his part, Tanzania Tour Guides Association (TTGA) chairman Emmanuel Mollel said a multitude of taxes imposed on tourist companies and tour guides caused tourism costs to be unaffordable to most tourists, who fail to revisit the country.
“There are too many taxes as each passing day new taxes are introduced, forcing owners of tourist firms to hike costs so that they can make a profit,” said Mr Mollel. He questioned why some airlines were charging $500 more per ticket from Europe to Tanzania compared to when landing at other airports in neighbouring countries.

Tanzania Porters Organisation (TPO) secretary Loshiye Mollel said continued existence of tourist firms with unprofessional workers had been a problem to tourists.

“So far there are some tourist companies against which we have opened cases at police stations for using our members to guide tourists on the mountain and failing to pay them. For such a conduct, what sort of experience do they give to tourists visiting the country?” queried Mr Mollel.

Tanzania Association of Tour Operators (Tato) executive secretary Sirili Akko admitted that the tourism sector was facing a number of challenges that they have submitted to the government for action.

“I don’t want to speak too much on this issue. But I think our members will explain as to why their customers do not return after visiting the country,” said Mr Akko.
For his part, TLPO chairman Sammy Mdia said a multitude of over 20 taxes caused tourism to be costly in the country and that poor condition of infrastructure also was another tumbling block.

Opening the annual meeting for editors and senior reporters in the tourism industry, Natural Resources and Tourism permanent secretary Aloyce Nzuki called upon journalists to deliberate on why only 20 percent of tourists revisited the country.

Dr Nzuki also called upon media houses in the country to give the good image of the country before and after tourists visiting the country. Besides various proposals they gave in the meeting, journalists advised that a meeting of stakeholders of the tourism industry should be convened, under the Editors Forum, so as to freely discuss the challenges facing the sector.
 
Mimi niliwahi kuilalamikia hifadhi ya serengeti hapa!! Pale Nabi gate kwanza watumishi wanawadharau watanzania,ukiondoa madereva wa tours,mfano nilikuta pale watu wana tatizo la mfumo wa kulipia ada,kadi yao ya mastercard ilikuwa haisomi,sasa kuna askari mmoja yupo pale,ni mnene na mrefu,akawa anawagombeza wale watu kuwa waondoke eneo lile haraka kwa kuwa eti aliwaletea dalali wa kuwalipia kwa bei karibu mara mbili ya ile ya halali wakakataa,yule askari badala ya kuwatafutia suluhisho alikuwa akiwagombeza na kuwakejeli hadi nikaona huruma nikaingilia na kuwalipia kwa mkopo,angalau siku hizi nabi wanapokea Mpesa,ila kwenye geti la Laobare(ngorongoro) bado wanangangania Mastercard tu,hiyo inafanya iwe vigumu kwa watanzania wa kawaida ku enjoy mbuga zetu,hizi mbuga zetu hazina mvuto kwa wazawa kabisa,kwa kuwa mfumo ume wa favour wageni kwa asilimia zote
Chief...

Huo Uzi naukumbuka

Inahuzunisha mpaka leo mambo ni Yale Yale!.
 
Tatizo siyo kingine..
Ni gharama kubwa ya kutembelea mbuga zetu.
Ningeshauri wizara ya maliasili ipunguze gharama ya kuingia ngorongoro, Serengeti, lake manyara, tarangire, kilimanjaro na arusha national park cos ndio mbuga zinatembelewa sana bila kupunguza msitarajie mabadiliko yeyote.

Tanzania has the cheapest hakuna travel ingine africa ni cheap and adventourous kushinda tanzania, there may be other factors but not the price
 
Back
Top Bottom