Hakuna kitu kisichohitaji ubunifu na akili.
Kama huduma za utalii zingekuwa contracted, nina hakika sekta binafsi ingefanya vizuri maradufu ya jinsi mambo yalivyo leo.
Serikali yetu hakuna inachokiweza. Kwenye biashara na uchumi, ndiyo sifuri kabisa. Ushahidi upo, jinsi mashirika mbalimbali na viwanda namna vilivyokufa.
Na mahali ambapo Rais Magufuli amefeli kabisa, ni kufikiria Serikali, tena Serikali ya Tanzania inaweza kufanya biashara. Na akitaka aangamize kabisa uchumi mdogo uliopo aendelee kuweka shughuli za biashara kuwa controlled na Serikali.
Tanzania, pamoja na vivutio vyote tinavyotamba navyo, kwa mwaka mapato ni $3 billion. Misri mapiramidi yanaingiza $5 billion, Jiji la Paris $80 billion.
Serikali inafikiria utalii ni mikia tu ya fisi, pundamilia na tembo! Wanaofanya utalii, wanataka ku-enjoy na relaxation, sasa ukishaona mikia ya pundamilia, ndiyo basi. Hakuna cha ziada.
Tunazidiwa na nchi kama Thailand inayofanya sex tourism. Utajiri mkubwa hapa Duniani ni akili, siyo madini wala twiga na fisi. Ukiwa na akili halafu ukawa na madini, gas, wanyamapori, unapaa. Lakini hata ukapewa vyote hivyo, kama huna akili, utaendelea kudumu kwenye ndoa ya umaskini.
Nilienda Serengeti kwa kupitia lango la kule Magu, ni hovyo kabisa. Hiyo anayeandikisha mnapoingia unadhani amesoma shule ya ngumbaru. Hata ywezo wa kuandika ni hoi. Mtu mwenyewe ni goigoi, hajua thamani ya muda na wala hajitambui. Pale langoni tu, unaanza kukatishwa tamaa.
Tuna wanyama na mbuga lakini hatuna watu wa kuvipa thamani vitu hivyo!!
Sent using
Jamii Forums mobile app