Serikali yakiri kuwa zaidi ya 80% ya watalii wanaotembelea Tanzania huwa hawarudi tena

Nashauri tujifunze kwa nchi zinazofanya vizuri kama Dubai, Malaysia, Misiri, Hongkong n.k. hata ikiwezekana waje watufundishe kwa muda ili na sisi kufikia pale walipofikia.
Haina haja ya kuwaita watufnze....... Tuna watu hapa wana akili na wapo very smart, shida ya viongozi wa serikali ni kujiona smart brain na authority over everything and everyone.

Wao wakishapokea mishahara minono na kupita pita humu barabarani na mavx wanajiona wamemaliza kila kitu. Wasichojua ni kuwa wanatuchelewesha maisha na tunakosa pesa nyingi sana especially kipindi hiki cha covid 19 Tanzania ilikuwa ni chance yetu ya kuboom utalii sana.

Wazungu huko ulaya wamechoka sana na lock down... Wanataka kutoka warefresh akili. Sasa destination kama Tanzania kama tungeweka fair price na proper environment ya kuwapa hawa wageni hospitality at a very fair cost aaaaaaah walahi ntakwambia tungekuwa tunafunga hesabu ya trillion 10 kila mwezi kutokana na utalii tu hapo sekta nyingine zikiguswa na utalii pia.....
 
Urudi Tanzania kufanya Nini? Kwingine duniani nchi zinapunguza Kodi kubusti utalii, hapa kwetu tunaongeza Kodi kwa watalii kila uchao. Tayari Kuna jini jipya linaitwa bed levy linasubiri wageni wamiminike kwa wingi
Kuna mambo yanakera sana. Kwanza kujua tu kuna viongozi hawafanyi matakwa ya wenye inchi yetu tayari inajenga hasira sana......
 
Ufafanuzi mzuri
 
Hii kubwa sana..... Na sijui wanachaji nyingi hivyo ili iwaje?!
 
Mtaongea yote ila Tanzania Kodi Kodi Kodi ni nyingi mno.

Punguzeni Kodi otherwise tutabaki na masimba yetu
Its about time tuanze kuhoji hizi kodi zinatumikaje maana hazirudi kwakweli. Sioni mrejesho wa haya makusanyo.
 
Seronera ndio wapi huko mkuu?
 
Tatizo letu kubwa ni kujifanya tunajua Kila kitu au tunaweza Kila kitu kwa vile na sisi tuna certificate kama wao....!!

Ili kuinua quality tunahitaji kuruhusu a lot of expatriates in this sector.
Sheria za uhamiaji sio rafiki, zinawabana watu wenye mitaji na akili kubwa kuja kuwekeza nchini.
 
Tanzania Tourist Board wenyewe kucha kusafiri kwenda Ulaya na kula posho tu huku ubunifu ukiwa sifuri
Halafu bora usikie tu.... Aiseeee uwaone..... Yaaani ni wale sampuli ya watu waliosoma bush, mjini wamekuja miaka ya chuo na baada ya hapo ndio wamepata kazi.

Sasa majitu ya hivi huwa bado mashamba sana na hayana exposure na maisha ya kisasa ya mjini na ubunifu wao ni zero.

Unakuja kumpa mtu kama huyu ofisi ya utalii, unadhani atafanya nini zaidi ya kuwa busy kutoa ushamba wake tu kwa kufanya mambo ya kifala fala. Mifano ipo wazi, kigwangala.

Anapewa platform kubwa ya uwaziri wa utalii anaanza kutuhadithia shida akizopitia akiwa mtoto hadi maisha ya kuja kuwa kiongozi. Me ningekuwa raisi ile ni sababu tosha ya kumtoa nafasi ya uwaziri. Maana pale anakupa picha kuwa anaona tayari ameshatoboa maisha sasa kama sio ufala ni nini?!

Hizi nafasi wanawapa watu ambao sio sehemu yao hata kidogo.....
 
Ukiona mpaka serikali imekiri ujue basi kuna sehemu kuna shida

Kwa vyovyote vile watakuwa wamefanya reference na nchi mbalimbali duniani.

Kwa mfano sehemu km Dubai wanaweza kuwa wametoa ripoti, may be 60% ya watalii wanaoenda Dubai huwa wanarudi. Sasa hpo vyovyote km nchi lazima tujiulize shida ipo wapi!
 
Wahudumu wanasoma utalii college field matako bar, what do u expect??

Wafanyakazi Bongo wa hiyo sector, attitude yao kwa mteja ni 'kwani umeitwa si umekuja mwenyewe' wapo kupata mshahara hawafurahii wanachofanya.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Tatizo sisi raia hatupo serious katika kuhoji matumizi ya wazi ya hizo fedha wanakusanya. Hizi pesa hawa nguruwe wanafanya ndio mtaji wao na watoto wao kufanya maisha yao. Sisi wanatuletea ukanjanja sana mbwa hawa.
 
Nani aje Tanzania kwenye nchi ambayo (1) Haipimi wagonjwa kama wana COVID19 na (2) Haitoi takwimu kana kuna wagonjwa, waliokufa nanwaliopona.

Endeleeni kudanganywa na Magufuli
 
Yes issue ya bei kuwa wazi ni muhimu na hili jambo ni sehemu nyingi , hata hizi pub n.k
 
Ruaha kabla mtu hajafika anaanza kukata tamaa... ZILE KILOMITA NYINGI ZA BARABARA YA VUMBI TOKA MJINI HADI MBUGANI zinakata stimu na kutia uchovu kabla hata ya kufika geti la mbugani.. Ingawa kwa hospitality na good customer care jamaa wanajitahidi..
 
Safi sana. Serikali kandamizi hii yenye kufeli kila jambo!
 
Ukiona mpaka serikali imekubali kuwa kuna shida mahali, ujue walishafanya reference na nchi nyingine na kuona takwimu zao zinafanya. Vizuri zaidi yetu.
 
Tatizo kubwa si serikali kufanya biashara au mtu Binafsi, bali ni kuwa focused kwenye kutoa huduma kama ulivyosema huyo attendant alivyokuwa na labda utakuta Manager wasehemu hiyo anakosa ku link na staff wake na pia customers ilikujua changamoto zilizopo mapema, jingine ni kutotoa mishahara mizuri kwa staff , ambao mwisho wake ni kutengeneza michongo, kutokula vizuri, hivyo kukosa mvuto wa kumkaribisha mgeni.
La mwisho ni kukosa mngt skills na planning za kiuchumi kumuwezesha mfanyakazi kujiendeleza kibinafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…