Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
Nimeipenda hii theory.The lower the price at good service level, the higher the number of customers joining the service.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeipenda hii theory.The lower the price at good service level, the higher the number of customers joining the service.
Haina haja ya kuwaita watufnze....... Tuna watu hapa wana akili na wapo very smart, shida ya viongozi wa serikali ni kujiona smart brain na authority over everything and everyone.Nashauri tujifunze kwa nchi zinazofanya vizuri kama Dubai, Malaysia, Misiri, Hongkong n.k. hata ikiwezekana waje watufundishe kwa muda ili na sisi kufikia pale walipofikia.
Kuna mambo yanakera sana. Kwanza kujua tu kuna viongozi hawafanyi matakwa ya wenye inchi yetu tayari inajenga hasira sana......Urudi Tanzania kufanya Nini? Kwingine duniani nchi zinapunguza Kodi kubusti utalii, hapa kwetu tunaongeza Kodi kwa watalii kila uchao. Tayari Kuna jini jipya linaitwa bed levy linasubiri wageni wamiminike kwa wingi
Ufafanuzi mzuriWatalii hawarudi kwa sababu zifuatazo:-
1. Gharama za utalii sio rafiki mfano kupanda mlima Kilimanjaro mtalii mmoja ni usd 1000 . Bila malazi ya hoteli alikoshukia na chakula na unakuja kila mtalii anapanda mlima kea gharama tofauti mwisho watalii wakikutana na kujadiliana wanaomba watanzania ni watu wasio waaminifu.
2. Utalii umeingiliwa na watu na makampuni yasiojua utalii ni nini mwisho hawapati customer care kwa wageni.
3. Ubovu wa miundombinu mfano barabara zilizopo ngorongoro crater na serengeti national park. Mgeni akirudi safari anakwenda kuugua kwanza.
4. Wageni wengi ni watalii na ni wapiga picha mbugani. Hivyo unakuja anaingia mbugani kwa dola chache ,anapika picha. Nyingi kwa gharama ile ile na picha anakwenda kuziuza kwa bei kubwa na Hana haha ya kurudi tena.
Hii kubwa sana..... Na sijui wanachaji nyingi hivyo ili iwaje?!Mwaka jana nilipanda mlima Kilimanjaro na huko niliongea na baadhi ya watalii wakutoka nje. Wengi wanalilimikia ukubwa wa kodi. Kwa mtu mmoja kodi ilikuwa dola 800 kwa mujibu wa maelezo yao. Hiki ni kiwango kikubwa sana kwa mtu wa kawaida.
Serikali ipunguze kodi na iongeze promo.
Its about time tuanze kuhoji hizi kodi zinatumikaje maana hazirudi kwakweli. Sioni mrejesho wa haya makusanyo.Mtaongea yote ila Tanzania Kodi Kodi Kodi ni nyingi mno.
Punguzeni Kodi otherwise tutabaki na masimba yetu
Kuna fala m'moja tu ameona huo ni ubunifu...... Hili taifa lina viongozi mapopoma..... MUNGU atusaidie.....Na kodi ya kitanda imeshazinduliwa,wanadhani watalii ni wajinga
Seronera ndio wapi huko mkuu?You are quite right, Sir. Kwenda kutalii si sawa na Simba na Yanga, inahitaji matayairisho. As you say, ukishaenda Ngorongoro mwaka huu, kwa nini uende tena? Ila kuna usemi Tanzania Unforgettable, kuna namna ya kutumia nafasi hii vizuri: wote waliokuja mara moja watarudi tu tena, maybe 3 or 4 times kabla hawajazeeka mno, na watakuja na familia.
Mie ni mfano mzuri. Tulienda mara ya kwanza Seronera tukiwa Form IV (Shy Bush, bure, tulilala sehemu za wanafunzi tukitumia malori ya Bwiru, Headmasters are very smart). Nikapenda sana. Hii ni lazima tuifanyie kazi Shule zote F2, F4 na F6 waende, kila mtoto aende walau mara moja. Hata kama tutamlipia au tutakula "hasara" inakupa addiction ni lazima tu utarudi tena na tena.
Next nikaenda after 8 years nishaajiriwa. Nikaenda tena 5 years later baada nilipooa, then after 3 nikiwa na familia nzima. Yote ilikuwa ni Seronera, ila ujanjani na kipato kupanda niliongeza Ngorongoro na Lobo.
Mtalii wa kweli atarudi every 4 or years, siyo kila mwaka.
Sheria za uhamiaji sio rafiki, zinawabana watu wenye mitaji na akili kubwa kuja kuwekeza nchini.Tatizo letu kubwa ni kujifanya tunajua Kila kitu au tunaweza Kila kitu kwa vile na sisi tuna certificate kama wao....!!
Ili kuinua quality tunahitaji kuruhusu a lot of expatriates in this sector.
Halafu bora usikie tu.... Aiseeee uwaone..... Yaaani ni wale sampuli ya watu waliosoma bush, mjini wamekuja miaka ya chuo na baada ya hapo ndio wamepata kazi.Tanzania Tourist Board wenyewe kucha kusafiri kwenda Ulaya na kula posho tu huku ubunifu ukiwa sifuri
Ukiona mpaka serikali imekiri ujue basi kuna sehemu kuna shidaKwanza nitoe kheri za mwaka mpya kwa wana jamvi. Pili nilitaka kidogo kutoa maoni yangu kutokana na habari hii :
Nikubaliane na hoja kuwa kuna eneo la maboresho katika sekta ya utalii. Hii ni general rule kama kila kitu lazima kiboreshwe, maana kwangu naamini ukiona hakuna maboresho basi ujue kitu kinakufa! Lakini si kwa hoja hizi za kuwa kuna wizi ndio maana watalii hawarudi!
Nadhani tunatafuta mchawi, hii ni tabia ya kawaida kwa mtalii kila siku kutafuta nchi ambazo hajawahi kufikia na kwenda huko. Ni mara chache sana kumuona mtalii anarudia nchi ambayo alishakwenda. Nayasema haya sio kama napotosha, binafsi nikichagua nchi ya kwenda kutembea basi kila mwaka nachagua nyengine. Sio kama nimekosewa wala!
Tanzania nachagua kila baada ya miaka 3-5 kurudia matembezi, lakini hii inakuwa ni special treatment kutokana na kuwa nina kwetu nataka kutembelea na wazee, ndugu, marafiki n.k. Sitashangaa kumuona mtalii aliekuwa na mahusiano na mtanzania kumuona anarudia matembezi yake Tanzania kwa sababu hii ambayo inafanana na hio ya kwangu hapo juu.
Nadhani tujikite kuboresha utalii lakini sio kunyosheana vidole na kuanza kumtafuta mchawi. Kama suala la usafiri wa anga ni kweli Tanzania haina connection nzuri, sina uhakika tatizo ni nini. Hili linanisumbua hadi leo kufahamu, tena miaka ya hivi karibuni ndio kumeiprove kidogo. Zamani ilikuwa ticket za TZ ni ghali zaidi kutokana na uhaba wa airlines zinatua. Tutazame vizuri kama taifa jinsi ya kufanya partnerships na airlines na mataifa yenye watalii ili kuwe na urahisi wa haswa ticket za ndege.
Maasalaam
Tatizo sisi raia hatupo serious katika kuhoji matumizi ya wazi ya hizo fedha wanakusanya. Hizi pesa hawa nguruwe wanafanya ndio mtaji wao na watoto wao kufanya maisha yao. Sisi wanatuletea ukanjanja sana mbwa hawa.Kwa maoni ya wadau hapa, inaonyesha kodi kubwa ndio changamoto kubwa.
Ninachojiuliza ni kuwa mbona suala la kodi bongo ni kaa la moto?
Kwenye biashara kodi kubwa, viwandani kodi kubwa, kwenye kilimo tozo kibao, kuagiza bidhaa nje e.g. magari ndio balaa kabisa. Kumbe kwenye utalii nako hali nin gumu pia?
Ilitakiwa tuwe mbali sana kiuchumi kwa kodi hizi.
Nani aje Tanzania kwenye nchi ambayo (1) Haipimi wagonjwa kama wana COVID19 na (2) Haitoi takwimu kana kuna wagonjwa, waliokufa nanwaliopona.Haina haja ya kuwaita watufnze....... Tuna watu hapa wana akili na wapo very smart, shida ya viongozi wa serikali ni kujiona smart brain na authority over everything and everyone.
Wao wakishapokea mishahara minono na kupita pita humu barabarani na mavx wanajiona wamemaliza kila kitu. Wasichojua ni kuwa wanatuchelewesha maisha na tunakosa pesa nyingi sana especially kipindi hiki cha covid 19 Tanzania ilikuwa ni chance yetu ya kuboom utalii sana.
Wazungu huko ulaya wamechoka sana na lock down... Wanataka kutoka warefresh akili. Sasa destination kama Tanzania kama tungeweka fair price na proper environment ya kuwapa hawa wageni hospitality at a very fair cost aaaaaaah walahi ntakwambia tungekuwa tunafunga hesabu ya trillion 10 kila mwezi kutokana na utalii tu hapo sekta nyingine zikiguswa na utalii pia.....
Yes issue ya bei kuwa wazi ni muhimu na hili jambo ni sehemu nyingi , hata hizi pub n.kNi vema kutambua hao tunaowaita watalii zamani walijulikana kama Explorer ingawa sasa kuna tofauti kidogo. Kawaida mtalii/mzungu ktk miaka 3au4 anapanga nchi za kutembelea , hivyo basi akiisha tembelea eneo moja kati ya hayo 3 au 4 usitarajie atarudi kwako kabla ya kumaliza mzunguko wa maeneo aliyopanga kuyatembelea, hivyo ataendelea kuexplore sehemu nyingine ili notebook yake iweze kuonyesha ametembelea nchi au mabara mengi duniani.
Mkakati wa Tanzania ujielekeze ktk kuboresha huduma za utalii na kupunguza gharama za utalii ili wale wanaokuja wakirudi makwao wawambie wengine kuwa Tanzania Ni sehemu mzuri ya kutembelea.
Pia iwe Ni lazima kwa sehemu zinazohudumia watalii kuweka bango linaloonyesha bei ya huduma zao (price list). sasa hivi sehemu hizo muhudumu ana bei yake kwa mtalii, meneja na dereva nao wanazo bei zao na kampuni husika nayo bei yake, mwishowe sector ya utalii ndiyo inaumizwa!?
Ubabaishaji kila kona, wageni wanapigwa kila kona, no standard servicewatalii wa nje hawarudi tena baada ya kutembelea Tanzania
Ruaha kabla mtu hajafika anaanza kukata tamaa... ZILE KILOMITA NYINGI ZA BARABARA YA VUMBI TOKA MJINI HADI MBUGANI zinakata stimu na kutia uchovu kabla hata ya kufika geti la mbugani.. Ingawa kwa hospitality na good customer care jamaa wanajitahidi..Mm nimetembelea mbuga nying sn ila serenget sijawah fika kinachofanya watalii wasirud ni management mbovu mfano ukienda ruaha mapokez ni pa kiswahili vyoo ni vya kiswahili refreshment ndio kabisa uswahili swahili tu afu mbuga kubwa wanyama wachache yaan mnatafuta wanyama kwa mbinde chui, simba ndio balaa hawapatikan kuna haja ya kujenga good management wagen wasipate usumbufu mbuga pekee ambayo angalau niliifurahia ni manyara ipo poa sn japo na penyewe pana changamoto yake ilaa kwa serenget naamin ipo juu maana ndio best of all in africa
Ukiona mpaka serikali imekubali kuwa kuna shida mahali, ujue walishafanya reference na nchi nyingine na kuona takwimu zao zinafanya. Vizuri zaidi yetu.Kuna watu mnaleta siasa kila sehemu.
Yaani ni kama mmeamua kwenda kinyume tu na wale wanaoabudu na kusifu.
Hivi kwa akili za kawaida kabisa unakuja kupanda kilimanjaro 2021,utarudi tena kupanda mlima lini?
Mwingine analalamikia gharama,sijui anadhani mzungu ni sawa na mchaga wa uru anayerudi kuhesabiwa dec kwao moshi!!!wale wanajiandaa miaka hata 7 au 19 kabisa kwa ajiri ya kutengeneza kumbu kumbu maishani mwake.
kama kandaa sehemu 5 atembee duniania baada ya kujipanga,anarudije tz!!!
Tatizo kubwa si serikali kufanya biashara au mtu Binafsi, bali ni kuwa focused kwenye kutoa huduma kama ulivyosema huyo attendant alivyokuwa na labda utakuta Manager wasehemu hiyo anakosa ku link na staff wake na pia customers ilikujua changamoto zilizopo mapema, jingine ni kutotoa mishahara mizuri kwa staff , ambao mwisho wake ni kutengeneza michongo, kutokula vizuri, hivyo kukosa mvuto wa kumkaribisha mgeni.Hakuna kitu kisichohitaji ubunifu na akili.
Kama huduma za utalii zingekuwa contracted, nina hakika sekta binafsi ingefanya vizuri maradufu ya jinsi mambo yalivyo leo.
Serikali yetu hakuna inachokiweza. Kwenye biashara na uchumi, ndiyo sifuri kabisa. Ushahidi upo, jinsi mashirika mbalimbali na viwanda namna vilivyokufa.
Na mahali ambapo Rais Magufuli amefeli kabisa, ni kufikiria Serikali, tena Serikali ya Tanzania inaweza kufanya biashara. Na akitaka aangamize kabisa uchumi mdogo uliopo aendelee kuweka shughuli za biashara kuwa controlled na Serikali.
Tanzania, pamoja na vivutio vyote tunavyotamba navyo, kwa mwaka mapato ni $3 billion. Misri mapiramidi yanaingiza $5 billion, Jiji la Paris $80 billion.
Serikali inafikiria utalii ni mikia tu ya fisi, pundamilia na tembo! Wanaofanya utalii, wanataka ku-enjoy na relaxation, sasa ukishaona mikia ya pundamilia, ndiyo basi. Hakuna cha ziada.
Tunazidiwa na nchi kama Thailand inayofanya sex tourism. Utajiri mkubwa hapa Duniani ni akili, siyo madini wala twiga na fisi. Ukiwa na akili halafu ukawa na madini, gas, wanyamapori, unapaa. Lakini hata ukapewa vyote hivyo, kama huna akili, utaendelea kudumu kwenye ndoa ya umaskini.
Nilienda Serengeti kwa kupitia lango la kule Magu, ni hovyo kabisa. Huyo anayeandikisha mnapoingia unadhani amesoma shule ya ngumbaru. Hata uwezo wa kuandika ni hoi. Mtu mwenyewe ni goigoi, hajua thamani ya muda na wala hajitambui. Pale langoni tu, unaanza kukatishwa tamaa.
Tuna wanyama na mbuga lakini hatuna watu wa kuvipa thamani vitu hivyo!!
Sent using Jamii Forums mobile app