Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Serikali yakwama ujenzi Mji mpya wa NSSF Dege Eco Village Kigamboni, yatangaza kuuza mradi

Kwa hiyo alishindwa kuwashughulikia kwa miaka 5 yote.
Majengo yalitelekezwa hadi nilipokuwa nikipita nashangaa inakuaje mradi umeshatumia mamilion ya pesa umefika pale halafu majumba yanaachwa tu yaoze
Kuwashughulikia mafisadi kunahitaji muda mrefu
 
Kwa hiyo alishindwa kuwashughulikia kwa miaka 5 yote.
Majengo yalitelekezwa hadi nilipokuwa nikipita nashangaa inakuaje mradi umeshatumia mamilion ya pesa umefika pale halafu majumba yanaachwa tu yaoze
Sio tu kutekelezwa, yaani vifaa vyote mule kama magari, sijui vifaa vya ujenzi nk vimeibiwa karibia vyote
 
Roho mbaya, visasi na chuki vya JPM ndio vilisababisha mradi kusimama.
Nambie kimewashinda kipindi kuendeleza?
Miradi wa kifisadi from the beginning unaweza kuwa na matokeo chanya?
Akili zako ndogo hufikirii kwa nini miradi mingi ya majengo ya kibiashara hazina wapangaji?
Hayo magorofa unayoyaona hapo Dar gorofa za juu haina wangaji miaka nenda rudi!
Walikuwa wanaazisha miradi ya kifisadi wapige ten percent lakini wewe juha umekazania kumlaumu JPM!
Juzi hapa mlisema mmeshafungua nchi! What's wrong going on?
 
Hizi pesa za wafanyakazi ni za kuchangia wajanja wachache wafanye miradi ya ujanja ujanja kama hii kwa malengo ya kujitajirisha huku wastaafu wakisota kupata mafao yao na kubanwa na kikokotoo......nchi ya kindezi sana hii.
 
View attachment 2398070

Baada ya kusuasua kukamilika kwa mradi wa Dege Eco Village kwa thamani ya dola 653 milioni za Marekani (zaidi ya Sh1.3 trilioni), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililokuwa linautekeleza limetangaza kuuza kwa mwekezaji mwingine atakeyevutiwa nao.

Ujenzi wa mradi huo wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ulioanzishwa na NSSF mwaka 2014 ulisimama tangu Januari 2016 ukidaiwa kufisidi zaidi ya Sh179 bilioni hivyo kutokamilika kwa nyumba za kifahari, hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na kusambazwa Jumanne Oktoba 25 imetangaza kutafutwa kwa mzabuni atakayeuendeleza mradi huo.

“NSSF inakusudia kuuza mradi mzima wa Dege Eco Village, shirika halitowajibika tena baada ya mauzo haya. NSSF inakaribisha zabuni zilizofungwa kuununua mradi huu kwa viwango vya kimataifa vilivyoainishwa kwenye Kanuni za Ununuzi wa Umma zilizochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 446,” inasomeka sehemu ya taarifa ya NSSF.

Kwa wawekezaji watakaovutiwa kuuendeleza mradi huo uliosimama kwa miaka saba sasa, NSSF imesema wanaweza kuutembelea huko Rasi ya Dege iliyopo Kigamboni jijini hapa ili kuukagua na kujiridhisha na mandhari yake kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana wa Novemba 3.

Zabuni zote, shirika hilo limesema zinapaswa kuwasilishwa mpaka Novemba 14, saa 9:00 alasiri kabla hazijafunguliwa mbele ya waombaji wote watakaokuwa wamejitokeza kwenye ukumbi wake uliopo ghorofa ya saba katika Jengo la Benjamin William Mkapa.

View attachment 2398094

Pia, soma=> Dar: Mradi wa Dege Eco village uliotelekezwa Kigamboni
Ni wakati wetu kumiliki majengo makubwa baada ya fitina ya muda mrefu.....
 
Muda mrefu huku majengo yanaoza na kushuka thamani? Muda mrefu kiasi gani? Maana hata aliunda mahakama lakink hakuna fisadi lolote tuliwahi kusikia limepelekwa huko kwa miaka yote 5.
Kila alipojitahidi kuwakamata mnadai hawapendi matajiri anakinyongo nao,akina Manji wote walifirisi NSSF kwa kukopa, lakini Magufuli alivyoanza kumshugulikia makelele kibao,akina Lugemalira wa IPTL walipigiwa kelele na akina Lissu bungeni, lakini Magufuli alivyoanza kuwashugulikia mkaanza kusema wanaonewa, Watanganyika kwa unafiki hawajambo.
 
Ni awamu ya mwendazake sio hii
mwendazake ndiye aliyeupiga chini huo mradi.mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.mwenye huu mradi anajulikana tena wakati huo kuna nsomile mmoja aliupigia promo sana huo mradi.
 
Kila alipojitahidi kuwakamata mnadai hawapendi matajiri anakinyongo nao,akina Manji wote walifirisi NSSF kwa kukopa, lakini Magufuli alivyoanza kumshugulikia makelele kibao,akina Lugemalira wa IPTL walipigiwa kelele na akina Lissu bungeni, lakini Magufuli alivyoanza kuwashugulikia mkaanza kusema wanaonewa, Watanganyika kwa unafiki hawajambo.
Embu niambie Manji alikopaje NSSF?!
 
Duh...!. Bonge la fursa hili!.
Hapa Mchechu hawezi kuacha hii opportunity!.
Hapa matajiri watauwana!.
Huu ni wakati sasa wa PPR kuachana na media business na kuingia kwenye real estate na property!.
P
🤣🤣🤣kaka Pascal PPR itaweza hiyo ligi kweli?hapo tayari wakubwa washapangana,DG anakamilisha tu maandalizi ya mchezo.PPR jikite kwenye low cost housing,maeneo ya Kibaha,Kimara Bonyokwa,Kirungure,Mkuranga,Vianzi.nk.
 
Back
Top Bottom