Serikali yalipa bilioni 212 kwa ajili ya ndege 5

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kuwa serikali imefanya malipo ya awali ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombardier ndogo 1, pamoja na malipo ya bilioni 50 kwa ajili mradi wa kufua umeme wa katika bwawa la Julius Nyerere.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 4, 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma pamoja na kupokea na kujibu maswali ya wananchi waliokuwa wakipiga simu.

"Serikali imefanya malipo ya awali ya ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombadier ndogo 1, pia serikali imefanya malipo ya bilioni 50 kwenye mradi wa reli na bilioni 50 kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere," amesema Msigwa.
 
Bwana Analogia Malenga , serikali ya nchi yako Ni kichwa Cha mwendawazimu kwa kweli, huku wanalalamika ATCL linaendeshwa kwa hasara, huku wanaendelea kuleta midege mingine!.
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kuwa serikali imefanya malipo ya awali ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombardier ndogo 1, pamoja na malipo ya bilioni 50 kwa ajili mradi wa kufua umeme wa katika bwawa la Julius Nyerere.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 4, 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma pamoja na kupokea na kujibu maswali ya wananchi waliokuwa wakipiga simu.

"Serikali imefanya malipo ya awali ya ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombadier ndogo 1, pia serikali imefanya malipo ya bilioni 50 kwenye mradi wa reli na bilioni 50 kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere," amesema Msigwa.
Hayo mabilioni ya ndege mnaudhi mungemalizana na Bwawa la Umeme ndio mengine ya ndege yafuate
 
Afu tujesikia ndege hazifiki kwetu Ruvuma, ingefaa serikali ikawekeza kwenye miundo mbinu ikavutia wawekezaji wakawekeza kwenye safari za ndani. Wakachapa kodi sasa

Iwe mtu ukiwa Dodoma huwazi kufika Mtwara
 
😁😁😁
2656558_102011131.jpg
 
Kweli hii serikali ni jeuri.
Ni kweli matatizo ya wananchi yatatatuliwa kwa midege hiyo?
Kila mwaka hasara, halafu wanaendelea kuyanunua!!
Hivi vichaa ni viongozi au wananchi?
 
ku…………………….[emoji35][emoji2962][emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959][emoji2959]

yani kuna sehemu hata dawa wala huduma za jamii ni tatizo.alafu wanaenda kutukoroga kufanya haya.
kuna mtu hata kuwa na faida kwenye udalali
 
Safii. Na Zanzibar tupewe mgao wetu (50%-50%)
Hakuna mgao wa Zanzibar fanyeni kazi sio mnashinda virabarazani mnakunywa alkasusu mnategemea wanaume toka Mainland tupambane nyie mlee
 
Ni jambo zuri Serikali kuweza kukamilisha malipo hayo tena kwa kutumia fedha za ndani.

Wasiwasi wangu ni kama tumeweza kushughulikia dosari zilizoainishwa kwenye ripoti ya CAG kuona namna bora ya kuliendesha na kulifufua Shirika letu la Ndege.

Binafsi nilidhani Serikali ingejikita kwenye kuboresha miundombinu na mazingira wezeshi ya biashara ya ndege ili akina Precision Air na akina FastJet warudi kufanya biashara na sisi kama Serikali tubaki kukusanya kodi.

Hizo Bilioni tungeendelea kuboresha mtandao wa barabara, kuna Wilaya hazina hata kilomita 1 ya Lami kuunganisha na Mikoa. Maji Vijijini bado yanachangamoto, tungeweza kuboresha ili kufikia 85% ya Ilani ya Uchaguzi kuelekea 2025
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema kuwa serikali imefanya malipo ya awali ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombardier ndogo 1, pamoja na malipo ya bilioni 50 kwa ajili mradi wa kufua umeme wa katika bwawa la Julius Nyerere.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 4, 2021, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma pamoja na kupokea na kujibu maswali ya wananchi waliokuwa wakipiga simu.

"Serikali imefanya malipo ya awali ya ya shilingi bilioni 212.95 kwa ajili ya Ndege 5, Ndege kubwa 2, za masafa ya kati 2 na Bombadier ndogo 1, pia serikali imefanya malipo ya bilioni 50 kwenye mradi wa reli na bilioni 50 kwenye mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere," amesema Msigwa.
Tulikwisha sema kuwa mkataba ulishasainiwa siku nyingi. Sasa ni utekelezaji tu. Tulijifunga wenyewe na hivyo kwa kuogopa fidia ya kuvunja hiyo mikataba tunaendelea kulipia hadi ndege zote zifike hapa.
 
Back
Top Bottom