Kuna video nyingi za watu October 29 policcm wakiua watu ziliweza kupatikana kwa ufanisi sababu ya CCTV.
Waligundua maeneo baadhi walitishiwa na kuambiwa wafute, wengine walivunjiwa camera zao na vifaa vyake kuchukuliwa hivyo sasa ni vita ya kuficha ukweli.
Ni nchi isiyojitambua ndio inataka ifahamu ulinzi binafsi wa mtu ameuweka wapi ili iweje?
Hapo wataambiwa watoe hadi ramani ya jengo ili wajue camera zitafungwa wapi ili kama wanakuja kumteka mtu wajue wanaanzia wapi, kama walivyofanya kwa Polepole baada ya kujua uelekeo na ramani ya nyumba kazi yao ya kwanza ilikua ni kuvunja camera na vifaa vyote vya ulinzi wa jengo.
Ni wakati wa watanganyika kupinga uhuni huu .