Serikali yapiga marufuku mazao ya uhandisijeni(GMOs) nchini

Serikali yapiga marufuku mazao ya uhandisijeni(GMOs) nchini

Mkuu sidhani kama uko sahihi sana (utanisamehe kama nakosea). Kuna hybrids (chotara) na hizo GMOs. Hybrids ndo zimeenea sana hapa nchini. Hizi ukipanda zinaota vizuri sema sifa husika (kuvumilia ukame, magonjwa, uzaaji nk) hupungua kadri unavyorudia kupanda

GMOs kwa sasa zilikuwa zinafanyiwa utafiti makutupola pale. Hizi huwa zinatengenezwa mahsusi kwa kuzaa sana au kuvumilia/kukinzana na magonjwa au wadudu fulani. Na wengine wanazifanya tegemezi kwa kitu fulani ili wapate faida zaidi kwa kukuuzia more products. Kwa mfano.

1. Mbegu inaweza ikatengenezwa ma ikafanywa tegemezi kwa kiuatilifu fulani ndo izae sana. Hapa utauziwa mbegu na kulazimishwa kununua hicho kiuatilifu ili upate majibu mazuri. Hapa utaambiwa ili izae vizuri inabidi utumie hii kitu shambani kwako katika kupalilia etc


2. Inaondolewa uwezo wa kuwa mbegu baada ya kuvuna. Hili linafanyika ili urudi kwa mtengenezaji kila ukitaka kulima.

Naomba kuwasilisha
You may be right, ila from what I know Monsanto wana kampuni Arusha, sijui kama wameshaanza kuuza au bado, but we are on the way there.
 
Sandpiper, do not only look at the superficial benefits you have been told by Monsanto.Please think of the dark side of GMOs.I do not have to go to the details of the side effects of GMOs because they are everywhere.But how for Gods sake can we believe Monsanto to have anything to do with what we eat,it is such an evil company.Please go through the following to have a glimpse at the history of the company,it is so horrific.

The Complete History of Monsanto, The World's Most Evil Corporation
The issue here is GMO, forget about MONSANTO , so is it o.k for other companies . Think about SASSO chicken . I believe that we are overreacting here . We need to be able to feed our people if we fail then in food aid we will not a choice what kind of seeds were used. Others have moved forward in Genetic engineering it o.k to use their knowledge to our advantage.
According to the U.S. Department of Agriculture (USDA), GM seeds are used to plant more than 90 percent of corn, soybeans, and cotton grown in the United States. Unless you consciously avoid them, GM foods likely find their way into many of your snacks and meals.
 
Ingekuwa kwa wenzetu wangeweka wazi majina ya wabunge waliotaka kutuletea GMO,ili tuwafahamu.
 
The issue here is GMO, forget about MONSANTO , so is it o.k for other companies . Think about SASSO chicken . I believe that we are overreacting here . We need to be able to feed our people if we fail then in food aid we will not a choice what kind of seeds were used. Others have moved forward in Genetic engineering it o.k to use their knowledge to our advantage.
According to the U.S. Department of Agriculture (USDA), GM seeds are used to plant more than 90 percent of corn, soybeans, and cotton grown in the United States. Unless you consciously avoid them, GM foods likely find their way into many of your snacks and meals.
Hivi unaijua US Department of Agriculture wewe na unaijua Monsanto na GMO companies wewe.Do you really know what they stand for.Kama ni scientist basi you are either a very young scientist so you do not really know what is going on.Halafu inaelekea unachumia tumbo,so you do not really care what happens to the unsuspecting and ignorant Tanzanians.
Very sad.

Finally sina haja ya kukuambia the dark side of GMOs,kama unataka kweli kujua, the internet has many sites which has the right information.Kwa kuanzia hata hivyo you can read this scholarly article.
This is a scholarly article of three GM corn on rats.The effects are very well documented in the conclusions.

A Comparison of the Effects of Three GM Corn Varieties on Mammalian Health

And finally please be informed that Monsanto has a stake in all GMO companies,it is infact the mother company.I would infact call it the "mother of harlots." This means that you cannot separate Monsanto from the other smaller GMO companies.They are one.Knowing the evil nature of Monsanto and therefore other companies, it would be suicide to allow Monsanto or any othet GMO company for that matter to have anything to do with our food.To really appreciate the evil nature of Monsanto,please go through the following article.It tells it all!

The Complete History of Monsanto, The World's Most Evil Corporation
 
The issue here is GMO, forget about MONSANTO , so is it o.k for other companies . Think about SASSO chicken . I believe that we are overreacting here . We need to be able to feed our people if we fail then in food aid we will not a choice what kind of seeds were used. Others have moved forward in Genetic engineering it o.k to use their knowledge to our advantage.
According to the U.S. Department of Agriculture (USDA), GM seeds are used to plant more than 90 percent of corn, soybeans, and cotton grown in the United States. Unless you consciously avoid them, GM foods likely find their way into many of your snacks and meals.
Mkuu, je ni kweli pamoja na ardhi yote hii na rasilimali maji na watu tunahitaji GMO? Hybrid zinatosha sana na tunaweza zalisha na kuuzia nchi zingine nyingi za Africa. Unajua hayo mazao wanayolima kwa GMO USA si kwa lengo la chakula cha binadamu kwa asilimia kubwa, pia wanazo sheria kali na uchunguzi wa mara kwa mara wa hivyo vyakula. Ni lazima label ionyeshe kuwa ni GMO na wengi hawatumii kabisa.
 
Hawa waliingia tangu wakati wa JK, ikaleta mvutano then wakapata mahala nadhani huko Dodoma kwa ajili ya majaribio na utafiti. Na cha ajabu wanapigiwa upatu na bahadhi ya watafiti wetu pengine kwa sababu wanatoa sana mpunga. Tanzania ina eneo kubwa sana ni suala tu la kumechanise kilimo na hatutakuwa na haja ya GMO. Tuachane na jembe la mkono, tufanye kilimo cha umwagiliaji na mfumo wa masoko uwe mzuri. Tunao uwezo mkubwa sana wa kuzalisha ziada ya kutosha kabisa
Nilimuona katika TV mtaalamu wetu wenyewe akipongeza sana utafiti huo wa GMO. Sikushangaa kwa vile naelewa anamtumikia shetani ili apate mradi wake, sasa afanyeje?
 
Acha hasira, mchumia tumbo!!!? jieleze kwa hoja
kwenye hiyo experiment
A Comparison of the Effects of Three GM Corn Varieties on Mammalian Health
kwenye discussion kinasema hivi ;The experiments clearly need to be repeated preferably with more than one species of animal. Secondly, the length of feeding was at most only three months, and thus only relatively acute and medium-term effects can be observed if any similar to what can be derived in a process such as carcinogenesis or after endocrine disruption in adults 21. Proof of toxicity is hard to decide on the basis of these conditions. Longer-term (up to 2 years) feeding experiments are clearly justified and indeed necessary. This requirement is supported by the fact that cancer, nervous and immune system diseases, and even reproductive disorders for examples can become apparent only after one or two years of a given intervention treatment under investigation, but they will not be evident in all cases after three months of administration when first signs of toxicity may be observed .
The bottom line these experiments were not conclusive enough to indicate the effects of GM . Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa tunahitaji kuwa na solution katika kilimo chetu . Waliojaribu kulima wanajua hasara zilivyowapata pale mvua zilipokata ghafla au ugonjwa wa mazao ukitokea . Mkulima amekuwa mtu wa kubahatisha . Tutabaki kuletewa mchele wa msaada kutoka India na kuendelea kuagiza vyakula kutoka nje ambavyo madhara yake hata hatujui , Umesahau mahindi ya njano , unga wa yanga? . Toa solution tufanye nini basi kama wewe ni Mwanasayansi uliokomaa. Tuna wasomi wenye PHD na Maprofesa lakini sijaona lini walikuja na suluhisho la matatizo ya Watanzania kwenye sekta mbalimbali. Negative People have a problem for every solution !!!!
 
Nisaidieni tofauti ya mbegu za hybrid na GMO,nielimishe tafadhali kuna mambo nataka kuelewa katika hayo,
pia tofauti ya hybrid na organic farming,au hybrid inaweza kutumika kwenye organic farming!
 
Uelewa wako wewe kwenye maswala ya GMO ni mdogo sana. Nakushauri kaa kimya tu wakufundishe wanaojua. Si lazima kuchangia hata kama hujui.
Kweli kabisa mkuu Mimi sio mtalam wa maswala ya mimea Ila kwa kusoma tu sehemu tofauti tofauti hawajamaa wanataka kuja kututeka wakisha maliza mbegu zetu wanaanza kutuwekea vikwazo hamtaki kuowana wanaume kwa wanaume hatuwapi tena mbegu!
Tukisema turudi kwenye mbegu zetu za asili hazitaota tena na hazita kubali tena ata tukiwa tumezihifadhi hili ni janga kubwa kuliko majanga yote!
 
Nov 21, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AITAKA TARI KUSITISHA MAJARIBIO YA GMO

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo tarehe 21 Novemba 2018 ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kusitisha mara moja utafiti na majaribio ya uhandisijeni (Genetic Modified Organism-GMO) yanayofanyika kwenye vituo vyake vya utafiti.

Aidha, Katibu Mkuu ameilekeza Taasisi hiyo ya TARI kuwa mabaki yote ya majaribio ya Uhandisijeni yateketezwe mara moja.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Taasisi hiyo kuanza kutoa matokeo ya utafiti bila kupata idhini ya serikali.

Siku za hivi karibuni Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha Makutupora imekuwa inaalika watu mbalimbali kwenda kuona matokeo ya utafiti wakati serikali haijaruhusu matumizi ya uhandisijeni nchini.

For the English Audience
The Tanzanian government has ordered The Agricultural Research Institute(TARI) to stop all Genetic Engineering (Genetic Modified Organisms-GMO) research and testing on all its centers.

This is to be followed by destroying all of what remains of the GMO testing materials.

Recently the Institute without the consent of the Government had started to disseminate and exhibit research results at one of its centers.


Zaidi, soma >> Nimeona wabunge wakishangilia ujio wa mbegu za GMO. Je, hawajui madhara yake kwa binadamu? - JamiiForums


Kwa wale wageni kwenye swala la GMOs,mada ifuatayo itasaidia kuongeza ufahamu.
Barua ya wazi kwa Rais Joseph Pombe Magufuli kuhusu GMOs.

Areafiftyone
JF-Expert Member

Nov 5, 2018
Genetically modified foods au organisms ni janga la dunia,pamoja na sisi tulioko JamiiForums.
Mwenzetu Dr Richard Mbunda ambaye anakerwa na GMOs, amemuandikia Rais barua ya wazi akieleza kwa kina ubaya wa GMOs na kueleza wazi kwa nini anaamini GMOs kama zitaruhusiwa kulimwa nchini,zitaleta adhari kubwa kwa uchumi wetu, hasa wa wakulima wadogo wadogo na afya za watanzania.Kwa vile janga la GMOs ni letu sote,tusome barua ya Dr.Richard Mbunda kwa makini halafu totoe mawazo yetu kama JF.Naomba baada ya hilo angalizo niombe moderators wasitoe uzi huu, ili watu waweze kutoa mawazo yao.Michango itakayotolewa hapa ina maana kubwa kwa kizazi hiki na vizazi vingi vijavyo.


Barua ya Wazi kwa Rais wa Tanzania: Je, GMOs ni Sera ya Serikali?

Na Dkt. Richard Mbunda - UDSM

Mheshimiwa Rais;

Heri ya siku ya kuzaliwa!

Kwa heshima na taadhima, niruhusu mimi mtoto wa mkulima mdogo na mwananchi wa nchi yetu tukufu nikusalimu. Hali yangu mimi na wanafamilia wenzangu, ambao ni wakulima wadogo nchini, si njema kabisa. Mheshimiwa Rais, kama ujuavyo, sisi ni takribani asilimia zaidi ya 70 ya wananchi wote, na naamini kuna ndugu zako wa damu ambao ni sehemu ya jamii hii ya watanzania.

Ukulima mdogo ndiyo uhalisia wetu. Hatuwezi kuukataa kwa sasa, japo wengi tuna matumaini ya kupiga hatua, kama serikali itatuwekea misingi thabiti. Lakini hali yetu ni ile Waswahili wanasema ‘bora ya jana kuliko leo.’ Mikakati ya kumkwamua mkulima mdogo nitaieleza katika kitabu changu, lakini kwa leo niruhusu tu nikuulize swali la kisera.

Mheshimiwa Rais, tarehe 28 Septemba, 2018 Jijini Geneva, Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilipitisha Azimio la Haki za Wakulima Wadogo. Azimio hili ni ushindi kwa wakulima wadogo duniani dhidi ya Makampuni hodhi katika sekta ya kilimo katika mapambano yaliyochukua zaidi ya miaka 17. Azimio hili linazungumzia haki za ARDHI, MBEGU, BAIOANUAI (Biodiversity) na SOKO LA NDANI LISINAJISIWE NA BIDHAA KUTOKA NJE.

Kimsingi haki hizi zinaendana na Uhuru wa Chakula (Food Sovereignty) kwa nchi maskini, ambao ndiyo uhuru pekee tuliobaki nao. Kinachonishangaza Mheshimiwa Rais ni kuwa, pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wakulima wadogo nchini, Tanzania haikuwakilishwa katika Azimio hili muhimu. Jumla ya nchi 34 zilikubali Azimio, nchi 11 zilikaa pembeni (abstain) na kama ilivyotegemewa, nchi zilizoendelea zilipinga Azimio hili. Mheshimiwa Rais, tulipitwa au hatujali? Namshukuru Mungu wa wanyonge Azimio limepita.

Lakini Mheshimiwa Rais, mienendo ya Serikali inatupa mashaka makubwa zaidi sisi familia ya wakulima wadogo. Naliongea hili kwa ujasiri kwa kuwa nimekulia kilimo na naishi na wakulima wadogo. Hata utafiti wangu wa uzamivu uliwalenga wakulima wadogo na unahusu Uhuru wa Chakula Tanzania.

Mheshimiwa Rais, serikali imekuwa ikipigia chapuo teknolojia ya uhandisijini wa mazao ya GMOs nchini. Tumeliona hilo katika Programu ya ASDP II uliyoizindua hivi karibuni, ambayo inatamka wazi mwelekeo wa kilimo chetu kwa matumizi ya GMOs, siyo tu katika mimea, bali hata wanyama (ikanifanya niwaze majaliwa ya ng’ombe za rafiki zangu Wamasai). Angalau basi tukusikie kwa maneno yako, je, wewe ni shabiki wa teknolojia hiyo na kwamba ni mdau wa mradi ya GMOs katika utafiti unaoendelea Makutupora, ambayo sasa inahalalishwa hapa nchini kupitia vyombo vya habari?

Barua yafaa iwe fupi ili isomeke kwa haraka na kueleweka kirahisi. Hivyo, Mheshimiwa Rais, nitaandika kwa uchache kuhusu sababu kwa nini Tanzania haihitaji GMOs. Lakini ninazo makala ndefu za kitaaluma zinazohusu jambo hili.

Sababu mojawapo ya kukataliwa GMOs inatokana na athari zake katika mazingira. Kwa mfano, katika utafiti uliofanywa na Mwanazuoni John Paul na kuchapishwa mwaka huu wa 2018, ikiwa na kichwa Genetically Modified Organisms (GMOs) as Invasive Species unaonesha kuwa GMOs ni viumbe vamizi. Huharibu mazao asilia, mimea mingine, wanyama na kuleta athari katika mazingira ya viumbe hai.

Hata katika elimu ndogo ya Kilimo tuliyojifunza sekondari, Mheshimiwa Rais, mahindi huzaa kwa uchavushaji. Kama mahindi ya GMOs na ya kawaida yatapandwa pamoja tutegemee nini? Kimsingi mahindi ya mbegu zisizo za GMOs yakiingiliana na ya GMOs yatapotea na kutuletea balaa kubwa la utegemezi huko mbeleni. Izingatiwe kuwa mbegu za GMOs hazirudiwi kupandwa zikatoa mazao.

Mheshimiwa Rais, napenda kujua kama hayo majaribio ya Makutupora yanajibu wasiwasi huu. Kwamba mbegu zao za GMOs hazitaathiri mbegu zetu, mimea mingine na mazingira kwa ujumla! Au ni utafiti unaoonesha tu kuwa GMOs zitastawi nchini? Mheshimiwa Rais unisamehe kwa kusema hili, hata bangi, ule mmea tunaoupiga vita, bado unastawi katika nchi yetu tukufu, tena vizuri mno.

Kupotea kwa mbegu zetu [kutokana na kuingiliana na mbegu za GMOs] kutatufanya tuwe watumwa wa makampuni ya mbegu. Mheshimiwa Rais, naamini umefuatilia habari kuhusu kampuni ya Monsanto, ambayo sasa imenunuliwa na kampuni ya Bayer ya Ujerumani kwa zaidi ya shilingi trilion 120 (USD 62 bn). Monsanto imekuwa ikipigwa vita hasa Amerika ya Kusini kwa namna ilivyotaka kuwafanya watu wake watumwa wa chakula. Pale ambapo tutapoteza mbegu zetu za asili, au tulizoziendeleza muda mrefu kupitia taasisi zetu za utafiti, tutakuwa tumekubali kuwa mateka.

Mheshimiwa Rais, wewe umekuwa ukipinga ubeberu kwa nguvu zako zote, na nisingependa hili la utumwa wa mbegu litokee katika utawala wako. Afrika Kusini, ambako waliruhusu GMOs tangu miaka ya 90, sasa zaidi ya asilimia 90 ya mahindi ni GMOs na wakulima wanalazimika kulipa ziada ya ada ya teknolojia kwa Monsanto. Pamoja na kubeparisha kilimo chao, bado Afrika Kusini hawajaweza kutokomeza njaa.

Suala la utamaduni wa chakula ni muhimu pia liongelewe katika muktadha huu. Kuna ladha, harufu nzuri na uasili wa chakula. Kama ujuavyo, Mheshimiwa Rais, hizi ni sifa pekee zinazotofautisha chakula chetu. Na tunapaswa kuvitunza vyakula hivi kwa choyo kubwa - hasa kwa kuwa sisi ni kitovu cha utalii Afrika.

Tukisoma baadhi ya makabrasha na shuhuda za wageni, tunaona watalii wanakizungumzia chakula chetu katika namna ya sifa ya pekee. Mheshimiwa Rais, pengine unakumbuka kuwa, mmoja kati ya watetezi wa GMOs Robert Paarlberg aliwahi kusema mwaka 2009 kuwa “chakula kilichozalishwa kiasili (organically) kina ladha na harufu ya kuvutia zaidi kuliko vyakula vya GMOs ndiyo maana nchi za Ulaya hazitaki GMOs" lakini "masikini wa Afrika hawapaswi kuwa na uchaguzi” Je, ni kweli tumefika sehemu ambayo hatupaswi kuwa na uchaguzi kwa kuwa sisi ni maskini?

Mheshimiwa Rais, katika makala yenye kichwa No Scientific Consensus on GMO Safety iliyochapisha wa wanasayansi 15 kwa pamoja katika Jarida la Environmental Sciences Europe mwaka 2015, tunaelezwa kwamba japo kumekuwa na jitihada za kuuaminisha ulimwengu kuwa GMOs ni salama kwa afya, lakini kimsingi hakujawa na muafaka wa usalama wa GMOs. Na kuna baadhi ya tafiti zilizoenda mbele kueleza kuwa GMOs zina madhara kiafya. Baadhi ya madhara ya afya yanayotajwa ni pamoja na uzio na saratani. Je, utafiti unaofanyika Makutupora unalenga kuleta majibu ya wasiwasi wa madhara ya afya yatokanayo na GMOs?

Monsanto imeshtakiwa zaidi ya mara hamsini huko Marekani na hivi karibuni ilipatikana na hatia, wananchi wakiilalamikia bidhaa zao kuwaleatea saratani. Kuhusu chakula cha GMO jibu la kampuni hiyo limekuwa hilo hilo kuwa hawalazimiki kisheria kudhibitisha kuwa vyakula vyao havina madhara. Wanaojiita wanasayansi wetu nchini hawatuambii ukweli, labda kwa maslahi yao binafsi. Lakini katika majadiliano tuliyofanya HakiArdhi hivi karibuni, mmoja wa wanasayansi hao, baada ya kubanwa na wakulima, alikiri kuwa uangalifu unahitajika hasa katika mimea iliyobadilishwa kuzalisha sumu ili kuua wadudu.

Mheshimiwa Rais, Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa Tanzania bado hatujafikia hata asilimia 30 ya matumizi ya mbegu bora, mbolea na viuatilifu. Bado tumekuwa tukizalisha zaidi ya asilimia 120 ya chakula kinachohitajika nchini. Wiki tatu zilizopita nilikuwa Mkoa wa Rukwa (Sumbawanga) na nilikutana na Wazalishaji wanaolalamikia soko la mahindi na siyo changamoto za uzalishaji. Tena kuna waliovuna mahindi ya kutosha bila hata kutumia mbolea.

Lakini watu wa GMOs wanatuletea taarifa kuwa kuna uzalishaji mdogo sana na mahindi yanashambuliwa sana na wadudu. Kimsingi wanatangaza Hali ya Hatari (National Emergency) kwa jinsi wanavyotuonesha wadudu wala mahindi katika video zao. Mheshimiwa Rais, ni kweli tumefikia huko? Kama ni kweli mbona hujatutangazia hali ya hatari ili basi GMOs tuipokee kama hatua yetu ya kupunguza kifo cha haraka? Na kama siyo kweli, kwa nini tunalazimishwa kuruka kutoka kutumia mbegu za asili kwa asilimia 80 za sasa hadi GMOs, teknolojia ya juu kabisa wakati hatujaweza kuvuna tija itokanayo na mbegu bora za OPVs na Hybrid?

Kuna agenda gani hapo? Tunakimbilia wapi? Tunapitwa na nini?

Mheshimiwa Rais, sipendi nikuchose sana. Naomba niulize swali moja la mwisho. Ubora tulio nao kama nchi ukilinganisha na nchi zingine (Comparative Advantage) wanaouongelea wachumi au kile wasomi wa fani ya Biashara wanachokiiita eneo la ubora (niche) wetu lipo katika nini? Sidhani kama tunaweza kushindana na Marekani katika kuzalisha mahindi ya GMOs, chakula chenye unyanyapaa duniani kote. Sisi tunapaswa kuwa msingi wa chakula salama Afrika Mashariki na kwingineko duniani. Wakulima wetu wanapaswa kuwa msingi wa kuzalisha chakula hiki na kunufaika kama ilivyo sasa, ambapo soko bado si la uhakika.

Katika utafiti wangu nilitembelea vituo vya utafiti wa kilimo. Nikiri kuwa ni taasisi nyeti na zina wataalam (japo wametelekezwa) wanaoweza kutusaidia katika kuboresha mbegu zetu za asili kama wakiwezeshwa. Sote tunajua mbegu bora siyo lazima iwe ya GMOs.

Mheshimiwa Rais, tukumbuke kuwa wakati wa Utawala wa Rais Dkt. Jakaya Kikwete, mradi wa GMOs wa WEMA haukuanza nchini japo ulipaswa kuanza 2008. Hii ilitokana na kifungu kinachohusiana na dhamana ya uharibifu kijulikanacho kwa Kiingereza kama ‘strict liability’ kilichopo katika kanuni zetu za usalama wa viumbe na uhai (Biosafety). Kifungu hiki kilisema mtu atakeyeingiza GMOs nchini atawajibika moja kwa moja kwa madhara yoyote yatakayotokana na GMOs kiafya, kimazingira na kiuchumi.

Hiki kifungu kiliwachelewesha watu hawa wa WEMA kuanza utafiti mpaka mwaka 2016 Serikali ilipolegeza masharti na kuweka kifungu kinachosema ‘strict liability’haitatumika katika utafiti. Kama GMOs ni kitu chema kama WEMA unavyodai na ni ukombozi wetu, waliogopa nini kuanza 2008 hadi wakashawishi kanuni zibadilike? Hata sasa wanadai sheria zetu zinawabana wanataka tulegeze zaidi watuletee balaa tushindwe pa kuwabana.

Walaji wa chakula kinacholimwa na wakulima wadogo hawapo salama pia. Muda si mrefu tutaanza kuona maduka makubwa (supermarkets) za vyakula vya asili (organic food) ambavyo watu wa kada ya juu tu ndio pekee watamudu kununua. Wameshaanza na madogo madogo. Tunaendelea kutengeneza matabaka kwa maslahi ya mwekezaji.

Mheshimiwa Rais, huenda barua hii haitakupendeza. Najua pia barua hii haitawapendeza wadau na watunga sera wanaopigania GMOs izidi kutamalaki nchini. Hakika itaichukiza kampuni husika inayowekeza katika mradi wa WEMA huko Makutupora.

Wanatudhihaki kuwa sisi tunapinga sayansi. Lakini ni sayansi zipi tumezipinga hapa nchini? Kama alivyowahi kusema mwanazuoni nguli Karl Polanyi mwaka 1944, hatuwezi kuiruhusu teknolojia ya kinyonyaji na inayokusudia kunufaika na majanga ya watu itamalaki.

Mheshimiwa Rais, nakushukuru kwa kusoma hii barua. Hatimaye nimetimiza wajibu wangu. Nimesema ukweli na sina haja ya kujificha
hongera kwa kusaidia taifa na jamii kwa ujumla.
 
Naunga mkono hoja ya kuzuia GMO kwa sababu kama mbegu ya kizazi cha kwanza haiwezi kutoa mbegu inayoweza kuzaa tena na kuleta propagation na continuity basi hilo ni balaa, maana tutalazimika kuagiza mnegu toka kwa hilo likampuni kwa bei watakayopanga wao kila msimu wa kilimo, kwasababu mbegu za asili zitakuwa zimetoweka kutokana na mwingiliano na mbegu hizi, huu ni utumwa mbaya sana, na hakua utumwa mbaya kama wa chakula, tubaki na mbegu zetu asili..! Huyo dokta kaokoa taifa la sasa na vizazi vijavyo, tunahitaji madokta wazalendo kama huyo..!
 
Kuna mtu anajiita Graph hii inamfaa. Maana jamaa sijui ana ulimbukeni wa technology au vipi. Inaonekana kwake yeye every technology has positive impact.

Uje ujionee huku kama watu wameweka hela mbele na hawajali afya yako wala mazingira.
 
Binafsi,nitoe pongezi kwa Serikali juu ya hii GMOs,pia Tunahitaji watafiti ka Mkuu Areafiftyone ambao wanaonyesha walisoma kwa maslahi pana ya wananchi ,na sio matumbo yao,Mkuu Areafiftyone hongera Sana,Ni Jana tu hapa Jf nilisoma makala kuhusu GMOs ilivo tishio kwa wakulima mf huko India .
 
[QUworld.sandpiper, post: 29313019, member: 496910"]Acha hasira, mchumia tumbo!!!? jieleze kwa hoja
kwenye hiyo experiment
A Comparison of the Effects of Three GM Corn Varieties on Mammalian Health
kwenye discussion kinasema hivi ;The experiments clearly need to be repeated preferably with more than one species of animal. Secondly, the length of feeding was at most only three months, and thus only relatively acute and medium-term effects can be observed if any similar to what can be derived in a process such as carcinogenesis or after endocrine disruption in adults 21. Proof of toxicity is hard to decide on the basis of these conditions. Longer-term (up to 2 years) feeding experiments are clearly justified and indeed necessary. This requirement is supported by the fact that cancer, nervous and immune system diseases, and even reproductive disorders for examples can become apparent only after one or two years of a given intervention treatment under investigation, but they will not be evident in all cases after three months of administration when first signs of toxicity may be observed .
The bottom line these experiments were not conclusive enough to indicate the effects of GM . Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa tunahitaji kuwa na solution katika kilimo chetu . Waliojaribu kulima wanajua hasara zilivyowapata pale mvua zilipokata ghafla au ugonjwa wa mazao ukitokea . Mkulima amekuwa mtu wa kubahatisha . Tutabaki kuletewa mchele wa msaada kutoka India na kuendelea kuagiza vyakula kutoka nje ambavyo madhara yake hata hatujui , Umesahau mahindi ya njano , unga wa yanga? . Toa solution tufanye nini basi kama wewe ni Mwanasayansi uliokomaa. Tuna wasomi wenye PHD na Maprofesa lakini sijaona lini walikuja na suluhisho la matatizo ya Watanzania kwenye sekta mbalimbali. Negative People have a problem for every solution !!!![/QUOTE]
Naomba usome conclusion vizuri,do not rush because the results scare you!Halafu remember,mimi sio mchumia tumbo kwa kuwa nawatetea Watanzania maskini nchi yao isiharibiwe na wasilishwe matakataka.Wewe ndio mchumia tumbo.


5. Conclusions
Patho-physiological profiles are unique for each GM crop/food, underlining the necessity for a case-by-case evaluation of their safety, as is largely admitted and agreed by regulators. It is not possible to make comments concerning any general, similar subchronic toxic effect for all GM foods. However, in the three GM maize varieties that formed the basis of this investigation, new side effects linked to the consumption of these cereals were revealed, which were sex- and often dose-dependent. Effects were mostly concentrated in kidney and liver function, the two major diet detoxification organs, but in detail differed with each GM type. In addition, some effects on heart, adrenal, spleen and blood cells were also frequently noted. As there normally exists sex differences in liver and kidney metabolism, the highly statistically significant disturbances in the function of these organs, seen between male and female rats, cannot be dismissed as biologically insignificant as has been proposed by others 4. We therefore conclude that our data strongly suggests that these GM maize varieties induce a state of hepatorenal toxicity. This can be due to the new pesticides (herbicide or insecticide) present specifically in each type of GM maize, although unintended metabolic effects due to the mutagenic properties of the GM transformation process cannot be excluded 42. All three GM maize varieties contain a distinctly different pesticide residue associated with their particular GM event (glyphosate and AMPA in NK 603, modified Cry1Ab in MON 810, modified Cry3Bb1 in MON 863). These substances have never before been an integral part of the human or animal diet and therefore their health consequences for those who consume them, especially over long time periods are currently unknown. Furthermore, any side effect linked to the GM event will be unique in each case as the site of transgene insertion and the spectrum of genome wide mutations will differ between the three modified maize types. In conclusion, our data presented here strongly recommend that additional long-term (up to 2 years) animal feeding studies be performed in at least three species, preferably also multi-generational, to provide true scientifically valid data on the acute and chronic toxic effects of GM crops, feed and foods. Our analysis highlights that the kidneys and liver as particularly important on which to focus such research as there was a clear negative impact on the function of these organs in rats consuming GM maize varieties for just 90 days.


Finally naomba usome article ifuatayo,labda itasaidia kuondoa hili pazia jeusi ulilofunikwa na Monsanto kuhusu GMOs.

Please read the following!

Genetically modified products and their potential to environmental harm.


The debate around genetically modified organisms (GMO) is huge and heated on either side. However one of the major considerations when arguing against the use of GMO products is the potential for environmental harm. But what exactly are the environmental risks to consider with regards to GMOs?
First of all, it is important to understand what a GMO is precisely. The World Heath Organization (WHO) defines them as organisms whose DNA has been altered in a non-natural way. GM plants are usually changed to be insect resistant, virus resistant, or herbicide tolerant. With these changes come some potentially problematic environmental challenges.



Firstly, toxicity is a huge issue surrounding chemical pesticides and herbicides, used commonly with GMOs, in addition to the toxicity inherent to these plants. GMOs may be toxic to non-target organisms, bees and butterflies being the most talked-about examples currently. Bees are hugely important in the pollination of many food crops, but are unfortunately extremely endangered by modern agricultural techniques, such as GM crops. Monarch butterflies are specifically at risk from GMO maize plants. In addition to bees and butterflies, birds are also at risk from pesticides, and work as biological control agents and pollinators, again, like bees.
Furthermore, the longterm effects of GMOs are not certain. Pests that are targeted by these agricultural methods can adapt to pesticides and herbicides, in addition to the DNA changes in GM plants to make them ¨resistant.¨ This means that they will not always be effective, but their toxic legacies will remain.
Cumulative effects of products such as GMOs are important to take into consideration. Evidence also suggests that small genetic changes in plants may produce even larger ecological shifts, meaning that there is potential for GMO´s to become persistent and weedy in agricultural conditions, since they are modified to be resistant to some modern agricultural techniques. This can also mean being invasive in natural settings, where GMOs, of course, do not occur naturally. It is not impossible for new, human modified, plants to become invasive species in delicate, natural ecosystems.



Finally, biodiversity, while it is critical in all ecosystems and to the sustainability of all species, is put at risk by GMOs. When GM crops are planted, generally in a monocrop fashion, many heritage seeds are no longer used. The nature of GMOs means fewer weed flowers and, therefore, less nectar for pollinators. Toxins released into the soil through the plants´ routes mean fewer soil bacteria, which are integral to healthy soil for plants to grow without the use of chemical fertilizers. Toxic residues are left in the soil of GM crops. Nutrients are not returned to the soil in mono crops and from GMO foods, meaning that soil is becoming dry and void of all nutrients, generally integral to the growing process. A cycle of dependence on GMO seeds and chemical fertilizers, pesticides, and herbicides is then created in order to grow a single crop. In addition to soil issues, the irrigation used to grow GM foods naturally carries all of these problems into water sources and into the air. This exposes different bacteria, insects, and animals to the same problems.
All of these impacts must be taken into consideration in the larger picture; GMO´s DNA may end up in soil, compost, animal feed and byproducts, and other living organisms from insects to larger pests. Bees can transport pesticides, herbicides, and DNA through the air into the environment. Once a plant is introduced in an agricultural environment, it is reasonable to assume it will become part of a larger ecosystem, meaning the problem of environmental damage done by GMOs is much larger than simply potentially harming our health.
Aside from environmental issues, GMOs are the topic of social and ethical debates as well. It goes without saying that we live in an inter-connected world, where the way we interact with nature can cause a complex array of consequences. Being informed on the food we are consuming, and the way modern agricultural techniques are affecting the environment, is one effective way of consciously interacting with the natural world
 
Back
Top Bottom