Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Hiyo damu ilimwagika wapi? Nani alimwagwa damu? Nani alinyang'anywa fedha zake? Unaweza kunitajia hao watu na walinyang'anywa kiasi gani?
Aliwaua watu zaidi ya 300 huko MKIRU, kuna wale wa kwenye viroba waliokuwa wakitupwa baharini. Aliua Ben Saanane, Azory Gwanda, Kanguye na alimshambulia kwa risasi Lissu kupitia kundi la wasiojulikana.

Aliwateka akina Mohamed Dewji, Roma Mkatoliki na Zakaria Trans. Ila Zakaria akakiwasha akawajeruhi watu wasiojulikana
 
Wengi wanatumia na wanatoboa,kuliko fedheha ya serikali kudhalilishwa.
 
Hakuna swala la uelewa kuna faida gani kubwa inayoonekana wazi wazi ni matokeo ya kulipa kodi.
 
Ilikuwa zamani enzi za giza, siyo sasa.
Kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kufikia muafaka ndiyo uongozi.

Ubabe na udikteta wa kulazimisha mambo yasiyowezekana hauna tija na ndo hupelekea nchi kuwa "a failed state"
Shukiruni ni mwaka wa Uchaguzi,huko Kenya wameuwa 3 ndio wanaojifanya kuwasikiliza.

Na nyie mlitakiwa mfinywe kwanza ndio msikilizwe.

Viva Chalamila.
 
Tax rates anapanga waziri kila mwaka kupitia ‘finance act’ hiyo ndio inaamua rates za income tax, VAT na import duties; pamoja na misamaa au nafuu za biashara serikali inazitoa.

Sasa humo waziri na team yake ya mipango wao ndio wanajua wanalenga nini kwenye fiscal policies zao, targets za uchumi, social policies, kuondoa inequality kwenye jamii, public goods and so on kilicho important kama kipaumbele chao huko serikalini na kwenye chama chao.

Maana yake ni you can’t ‘copy and paste’ finance act ya nchi nyingine (ambayo inapanga kodi) kkwa vipaumbele vya nchi tofauti havifanani wala mtazamo wa kugawana keki ya taifa aufanani.

However Income Tax act na VAT acts (hizi zinaweza fanana na nchi nyingi, ni sheria lakini zipo sana kufuata accounting standards za dunia) na uwa azibadiliki sana ni kwa ajiri ya administration purposes za kodi, kikubwa zinaelezea taratibu za kukusanya kodi information ambazo TRA na person (hilo ndio jina la kikodi kwa biashara ndogo), biashara kikodi ni (usajili wa public or private listed companies).

Shida ya wafanyabiashara wengi hawajasoma hizo sheria za (VAT and Income tax acts) hapo ndipo wanaposhindwa kuelewa hatua za TRA na kudhani wanaonewa.

Moreover kila ‘finance act’ mpya inapoanza kazi, TRA kupitia site yao (ambayo design view yake ni mbaya with so much clustered information inahitaji maboresho) uwa wanaweka necessary info kwenye website yao. Kule unapata info kama za import duties ya bidhaa mbali mbali, VAT zote fully, reduced rates and zero rated products, kuna maelezo ya kupiga hesabu mbali mbali za kodi.

Wakija sasa kama ni hesabu za kodi unatakiwa kujua finance act inasemaje kuhusu hiyo bidhaa VAT rate gani, import duty ni kiasi gani etc. Same kama ni income tax unatakiwa kujua how they calculate turnover ya chini tsh 100 na what changes ukizidisha.

Routine zingine za kuandaa vitabu vya biashara na jinsi TRA watakavyodai (fanya kazi ya kukusanya kodi) soma sasa ‘VAT na Income tax’ acts. Wafanyabiashara wa Tanzania they don’t read those acts wakitoka hapo wanalaumu TRA kwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.
 
Kwa Mtazamo wangu

TATIZO LA KARIAKOO NI ZAIDI YA WAFANYABIASHARA,WACHUUZI..LETS BE SERIOUS.

Tatizo la kariakoo haliwezi Kwisha ikiwa total supply chain ya mizigo inayouzwa kariakoo isiporekebishwa au kudhibitiwa kupitia maamuzi magumu na kutooneana haya wala aibu..

Bidhaa nyingi zinazouzwa kkoo zinaingizwa (Imported) toka China,India,Uturuki,Thailand,Vietnam,Zambia,Uganda,etc..Mfumo wa uingizaji na ulipiaji kodi wa mizigo husika ndio mzizi wa shida na tatizo lililopo na litakalokuwepo..

Cartel inayoratibu Logistics na supply chain ya mizigo ya wafanyabiashara wa karikoo isipodhibitiwa kila nyakati tutaona fukuto na migomo isiyohitaji siasa Bali utashi wa maamuzi magumu kudhibiti wahujumu uchumi tunaowalinda..

Mathalani,Mfanyabiashara akiagiza mzigo wa viatu Kwa kontena na kulipa ushuru stahiki kisha kuwa na nyaraka zote Za kikodi (Import duties,Port charges,Wharfage,VAT) inamgharimu milioni 45….NOTE:- Ila akiagiza mzigo huo huo kwa kutumia Logistics Cartels inamgharimu Milioni 15 tu pasipo nyaraka zozote lakini Ana uhakika wa kufikishiwa mzigo dukani au warehouse kwake pasipo usumbufu..

Sasa wale wafanyabiashara waliokuwa wakikomaa na kufuata taratibu stahiki wamejikuta wakishindwa kushindana ktk soko na kufirisika ama kufa kibiashara sababu ya ughali wa bidhaa dhidi ya wale wanaotumia Logistics Mafia..

On the other hand wanaotumia huduma za logistics cartel au mafia inawawia Vigumu sana kufanya compliance za kikodi sababu ya kukosa nyaraka muhimu kussuport mapana ya stock zao..Mauzo yao,returns zao..Hapa ndio kwenye shidaa haswaa…Wengi wana stock kubwa kuliko vielelezo vya manunuzi ya stock husika..Wamegeuka wachuuzi..Wanaouza ambacho hawana nyaraka Za wametoa wapi..SHIDA.

Logistics Cartel/Supply chain Mafia:-Ni kundi hatari lenye nguvu kupitia wanasiasa wakubwa waliopo na wastaafu..Wana ukwasi mkubwa na umaarufu mkubwa ktk Kiwango cha kuogopeka na Wakubwa wa TRA,Polisi,Etc..Wana nguvu mnooo ya kufanya wakubwa ktk mamlaka Za kodi watumbuliwe,Wafanyakazi wahamishwe,Wawe demoted..Wapate Stroke..Nina hakika hata CG wa TRA anawaogopa..Hana la kuwafanya..Inasemekana baadhi ya viongozi ni marafiki wakubwa..

Cartels hizi zimehodhi Supply chain Za uagizaji bidhaa,usafirishaji,Ulipaji kodi,Udanganyifu (under declaration&Falsa Declarations),Uzungushaji mizigo (Taarifa Za kampuni Za tracking devices Za mizigo ya transit zina mengi)..Wanamiriki makampuni ya uagizaji,Usafirishaji,Bonded Warehouses,ICD’s,CFS..yaani acha tu..Nani wa kuwagusa?!

Kwa hakika tunapoteza kodi nyingi sana zinazoingia mifukoni mwa wachache tunaowaimbia mapambio ya utajiri na ubilionea huku wachache wakikamuliwa hata kuzirai kibiashara..Bila maamuzi magumu na dhabiti tutaendelea kukwama na kuumiza wasiostahili..

Tukiamua Tunaweza..Viongozi wenye dhamana Simameni kwenye haki na ukweli..
 

Sijasikia issue ya wafanyabiashara wa kichina ambayo wafanyabiashara wa kitanzania walilalamika,inaongelewa😱
 
Sijasikia issue ya wafanyabiashara wa kichina ambayo wafanyabiashara wa kitanzania walilalamika, inaongelewa
 
Wafanyabiashara have not gained much. Walichofanya ni ku delay makali . Serikali wa ache unafiki. Wanategemea TRA wataweza ku meet targets zao za tax collection kama the government does support them. I believe wako watu wanaweza ku replace hao wafanyabiashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…