Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Serikali yasalimu amri mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo, yakubali kusitisha kamatakamata ya TRA na kuleta mfumo mpya wa kodi

Kiufupi wafanyabiashara wanajipangia walipe kodi ipi na kiasi kipi.. wafanyakazi wa serikali especially walimu mmeona wenzenu wamekaza wamepata wanachokitaka,kuna cha kujifunza hapa.
 
Shida ni kwamba wewe pimbi uko ofsini unafanya kazi chini ya kiyoyozi ma mwisho wa mwezi unalipwa mshahara ndiyo maana unaandika pumba hapa.

Ungekuwa umewahi kufanya biashara ukajuwa namna TRA wanavyo wavizia wafanyabiashara badala ya kuwaeleimisha usingeandika huo utumbo.
Mada inazungumzia malalamiko ya wafanyabiashara na ukiyasikiliza ukitoa swala la machinga mbele ya maduka (tatizo kweli), mengine ni ya uelewa wao tu kwa upande wa wafanyabiashara.

Hayo ya TRA kuvizia watu hakuna anaekataa hizo possibilities, ukikutana na kesi ya namna hiyo with evidence anzisha mada wana JF kwa umoja wetu tutakusaidia kuikemea serikali haki ipatikane.

Lakini kwenye haya malalamiko hadi kugoma 90% ya demands ni limitations za wafanyabiashara tu kwa mambo ambayo yapo wazi ni wao tu kujielemisha.
 
Wacha kutukumbusha huyo Magu aliyeiba kura zote za mwaka 2020 kwa kuogopa kushindwa uchaguzi. Usiturudishe kwenye ule utawala wa kumwaga damu na kunyang'anya fedha za wafanyabiashara kipitia TASK FORCE.

Muache Rais Samia atumie charisma yake ya kutawala nchi. Siasa za kuua na ubabe tulizizika na Magufuli mwenyewe March 2021
Hiyo damu ilimwagika wapi? Nani alimwagwa damu? Nani alinyang'anywa fedha zake? Unaweza kunitajia hao watu na walinyang'anywa kiasi gani?
 
Wanadekezwa hao na Samia Kwa sababu Kila kitu anawasikiliza.

Rais angekuwa Magu au Makonda au Mwigulu na PM Chalamila hakuna rangi wangeacha kuona

View: https://www.instagram.com/reel/C8mEzRNN7QA/?igsh=aDNoeDhzdTh2b3czView attachment 3024811

Wajinga kama hao uliotaja huwa hawachelewi kupigwa pini na wajeda wenyewe. Unakumbuka ile kauli ya kihuni kuwa watafanya usafi wa kudumu kuzuia maandamano, kwamba wamekosa kazi za maana za kufanya?!!

Kwenye utawala enzi za sasa, ukitumia ubabe na udikteta hutoboi
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo amesema wamekutana na wafanyabiashara wa Kariakoo na kutoka sehemu nyingine Tanzania wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo, Majid Mbwana baada ya mapema kutokea Mgomo wa Wafanyabiashara ambapo Biashara zilifungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024. Pamoja na Chalamila kuwasili Kariakoo katika jitihada za kutatua mgogoro huo jitihada zake ziligonga mwamba Baada ya Chalamila kuondoka Kariakoo, bado Wafanyabishara waliendeleza mgomo wa kufunga maduka.

Waziri Kitila amesema changamoto zilizofanya wafanyabiashara kutaka kufunga biashara zao zipo katika maeneo matano ambayo ni:-
  1. Changamoto ya ukosefu wa nyaraka hususan bandarini inayosababisha makadirio ya kodi yasiyo sahihi.
  2. Changamoto ya ukokotoaji ya kiwango cha kodi ambacho wanalipa.
  3. Suala la uwepo wa machinga katika maduka ambayo wanauza
  4. Suala la kamatakamata ambalo limekuwa likiendeshwa na mamlaka ya mapato(TRA)
  5. Changamoto kwenye sheria ya muswada wa fedha(Finance Bill)
Baada ya majadiliano ya kina Serikali imekubaliana mambo yafuatayo
  1. Kuanzia Julai 1, 2024 mamlaka ya mapato Tanzania itakuwa na mfumo mpya wa nyaraka ambao utatumika vizuri zaidi katika kuhakikisha wafanyabiashara wanapata makadirio ambayo ni sahihi.
  2. Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) inasitisha operesheni zake maarufu kama kamatakamata mpaka itakapokamilisha utaratibu huu ili kuweka mfumo mzuri zaidi wa kukusanya mapato.
  3. Suala la ukokotoaji wa kodi ni suala la kisheria, Serikali imelichukua na inaendelea kuliangalia ili kuboresha zaidi mfumo wa ukokotoaji wa kodi hususani bandarini.
  4. Kuendelea kuwapanga wamachinga kama ambavyo Rais aliagiza ili wakae katika maendeo sahihi ambayo hayaingilii biashara za watu wenye maduka ili kila mtu aweze kufaidika, wamachinga na wenye maduka katika eneo la Kariakoo.
  5. Serikali imewataarifu wafanyabiashara kuwa muswada wa sheria ya fedha(Finance Bill) ya mwaka 2024 bado haujapitishwa na sasa uko katika majadiliano bungeni na kamati ya bunge la bajeti imeita wananchi wote waweze kutoa maoni ikiwemo wafanyabiashara hivyo imewaalika yale maoni ambayo wanayo wayapeleke kwenye kamati ya Bunge na wabunge watazingatia maoni yao kabla sheria haijapitishwa.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
 
Attachments

  • 5751768-a1e447678b648f9be776a3662352bcea.mp4
    11.2 MB
That’s just cheap.

Waziri anazungumza TRA wawataarifu wafanyabiashara nyaraka za kuwa nazo kwenye tax estimates. Wakati hayo maelezo yapo kwenye VAT na Income Tax acts.

Hakuna kitu TRA wanafanya nje ya sheria na ni jukumu la mfanyabiashara pia kuzijua hizo sheria.

Sasa watu wanalalamika hawajui nyaraka za kuwa nazo badała ya kuwaelekeza kwenda kwenye vifungu vya sheria, unataka TRA itoe maelezo; uoni shida kubwa hapo ni hao wafanyabiashara kuzoea kufanya kazi kiholela kama hawajui hata sheria gani zinawataka watunze nyaraka gani au wawe nazo.
Labda nikukumbushe tu kuwa tax system lazima iendane na jamii.Income tax Act yetu ni copy and paste ya India,Uk na ilikuwepo toka ukoloni hivyo inakubali kwenye jamij ambavyo mifumo ya Kodi Iko well organized.Africa mkulima au mtu anadeal agricultural sometimes anapata hela nyingi na faida kubwa kuliko mchuuzi wa nguo lakini mkulima hayuko rasmi na Wala hasumbuliwi.Tunahitaji kulea biashara huku tukitengeneza mifumo ya watu kujulikana income bila kutumia nguvu.
 
Labda nikukumbushe tu kuwa tax system lazima iendane na jamii.Income tax yetu ni copy and paste ya India,Uk na ilikuwepo toka ukoloni hivyo inakubali kwenye jamij ambavyo mifumo ya Kodi Iko well organized.Africa mkulima au mtu anadeal agricultural sometimes anapata hela nyingi na faida kubwa kuliko mchuuzi wa nguo lakini mkulima hayuko rasmi na Wala hasumbuliwi.Tunahitaji kulea biashara huku tukitengeneza mifumo ya watu kujulikana income bila kutumia nguvu.
Inatakiwa iwe hivyo,Asante sana mkuu.
 
Hiyo ndio Taarifa ya sasa baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unaoendelea

=======

Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo amesema wamekutana na wafanyabiashara wa Kariakoo na kutoka sehemu nyingine Tanzania wakiongozwa na mwenyekiti wa wafanyabiashara Kariakoo, Majid Mbwana baada ya mapema kutokea Mgomo wa Wafanyabiashara ambapo Biashara zilifungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024. Pamoja na Chalamila kuwasili Kariakoo katika jitihada za kutatua mgogoro huo jitihada zake ziligonga mwamba Baada ya Chalamila kuondoka Kariakoo, bado Wafanyabishara waliendeleza mgomo wa kufunga maduka.

Waziri Kitila amesema changamoto zilizofanya wafanyabiashara kutaka kufunga biashara zao zipo katika maeneo matano ambayo ni:-
  1. Changamoto ya ukosefu wa nyaraka hususan bandarini inayosababisha makadirio ya kodi yasiyo sahihi.
  2. Changamoto ya ukokotoaji ya kiwango cha kodi ambacho wanalipa.
  3. Suala la uwepo wa machinga katika maduka ambayo wanauza
  4. Suala la kamatakamata ambalo limekuwa likiendeshwa na mamlaka ya mapato(TRA)
  5. Changamoto kwenye sheria ya muswada wa fedha(Finance Bill)
Baada ya majadiliano ya kina Serikali imekubaliana mambo yafuatayo
  1. Kuanzia Julai 1, 2024 mamlaka ya mapato Tanzania itakuwa na mfumo mpya wa nyaraka ambao utatumika vizuri zaidi katika kuhakikisha wafanyabiashara wanapata makadirio ambayo ni sahihi.
  2. Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) inasitisha operesheni zake maarufu kama kamatakamata mpaka itakapokamilisha utaratibu huu ili kuweka mfumo mzuri zaidi wa kukusanya mapato.
  3. Suala la ukokotoaji wa kodi ni suala la kisheria, Serikali imelichukua na inaendelea kuliangalia ili kuboresha zaidi mfumo wa ukokotoaji wa kodi hususani bandarini.
  4. Kuendelea kuwapanga wamachinga kama ambavyo Rais aliagiza ili wakae katika maendeo sahihi ambayo hayaingilii biashara za watu wenye maduka ili kila mtu aweze kufaidika, wamachinga na wenye maduka katika eneo la Kariakoo.
  5. Serikali imewataarifu wafanyabiashara kuwa muswada wa sheria ya fedha(Finance Bill) ya mwaka 2024 bado haujapitishwa na sasa uko katika majadiliano bungeni na kamati ya bunge la bajeti imeita wananchi wote waweze kutoa maoni ikiwemo wafanyabiashara hivyo imewaalika yale maoni ambayo wanayo wayapeleke kwenye kamati ya Bunge na wabunge watazingatia maoni yao kabla sheria haijapitishwa.

Pia, Soma=> Mgomo wa Wafanyabiashara: Biashara zafungwa Kariakoo leo Juni 24, 2024
Bandiko refu kama vile ni kitu kipya kisichojulikana.

Hayo mbona yalikubaliwa siku nyingi na Kassim Majaliwa alipokutana nao. Ni watendaji wabovu wa TRA waliolianzisha tena, wachukuliwe hatua.

Serikali ya mama Samia ni sikivu kuliko zote.
 
Back
Top Bottom