Serikali yashinda rufaa, Wakurugenzi kuendelea kusimamia chaguzi

Serikali yashinda rufaa, Wakurugenzi kuendelea kusimamia chaguzi

Kwahiyo waliamua kumsimamisha wakili ndo wapate naman ya kukanyaga Demokrasia vizuri. Hongera sana serikali ya CCM sasa ni kujimwambafai kwa kila nyanja kuanzia mitaa, diwani na Ubunge. Mkishindwa hata mtaa mmoja mmejitakia wenyewe. Hapa kazi tu.
 
Safi Sana !kiapo kinakubalika kisheria, haohao wakurugenzi mbona waliwapekeka wapinzani bungeni Sasa hivi iwe nongwa kwa nini! Acheni deko upinzani tafteni agenda zenye maana wananchi wawaelewe zaidi ya hapo chaguzi zote mtakuwa watu wa kulialia kila siku
Muhimu ni kula kiapo cha kuukana uwanachama!
Magufuli mwenyewe pamoja na kula kiapo kuiheshimu, kuilinda na kuitetea Katiba anaisigina anavyotaka bila woga wala haya

Pamoja na kula kiapo kuwa utawala wake utakuwa wa haki bila kuwabagua Watanzania katika misingi yoyote ile anawapendelea wazi wazi washirika na washikaji wake.

Pamoja na na kuapa kuwa wananchi watakuwa huru kutoa maoni yao anawatumia wasiojulikana kuwateka, kuwatesa, kuwamiminia risasi na hata kuwapoteza wanaomkosoa.

Kwa taifa langu Tanzania neno kiapo si chochote, si lolote na hutumika tu kuhalalisha uovu dhidi ya wanaharakati wanaopigania utawala unaoheshimu sheria na kudai haki.

Heri kiapo anachokula fisi kuwa hatashambulia kondoo wala swala kuliko anachokula kiongozi ndani ya taifa hili. Viapo vyao ni vya kulinda tu maslahi ya wakubwa wao, period.
 
Na kura watapiga wao kwa wao ..Sioni kama kuna Mhimili wowote unao weza kusimama wenyewe kwa kufuata Misingi ya Sheria na Haki za Watu wengine.Katiba inayompa Mtu mmoja Madaraka makubwa ni tatizo kwa kweli.
 
Hata hao majaji huukana uanachama wanapoapishwa lakini hawarudishi kadi za uanachama, hivyo hubaki wanachama.
Linapokuwa la kiserikali kama alivyowahi kusema Jaji Mkuu mstaafu kuwa huwa wanapata wakati ngumu kuamua, na yule wa kesi ya Mrema naye alipostaafu alisema alipata wakati ngumu sana kuamua kwani Rais wa wakati huo ilikuwa aondoke madarakani, nadhani mnakumbuka kile kiroba cha dhahabu.
HIS MASTERS VOICE.
 
Wakati mwingine Mungu anayaruhusu mambo fulani yatokee ili baadae jina lake lihimidiwe zaidi,tunakoelekea heshima itakuwepo na nchi itakaa vzr,wanaodhani wameshinda Leo,kesho watashindwa,Na watapata aibu kubwa sana
 
poleni sana mliojiandikisha mkitegemea maamuzi yasiyo fanana na ya mkuu yataheshimiwa, walio potezea UCHAFUZI huu pongezi sana.
 
SERIKALI YASHINDA RUFAA YA KUPINGA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI

Mahakama ya Rufani imetengua hukumu na amri ya Mahakama Kuu kuzuia wakurugenzi wa halmashauri, manispaa, na majiji kusimamia uchaguzi mkuu kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa maana hiyo Wakurugenzi wanaruhusiwa na wataendelea kusimamia uchaguzi.

> Mahakama ya rufaa imetoa uamuzi huo baada ya kujiridhisha na hoja za Serikali kuwa Wakurugenzi hao kabla ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi hula viapo vya kukana uanachama wao

> Kesi hiyo ilifunguliwa na Bob Wangwe akisimamiwa na Wakili Msomi Fatma Karume.
__________
Haya wahini mkajiandikishe kupiga Kura na muhawi foleni za kupiga Kura juani na kwenye mvua November 24, 2019 na October 25, 2020 ila mjue kazi yenu ni kupiga Kura tu ila wakubwa ndio wataamua nani awe Kiongozi. Period. Bado kuna mtu anajifariji kuwa Katiba Mpya na Tume HURU ya Uchaguzi sio muhimu sana katika kuamua mustakabali wa Taifa hili?

Mark my words kama upinzani utakubali kushiriki uchaguzi huu wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020 Wabunge wa Upinzani watakaorejea bungeni hawatozidi 10. Upinzani umedhoofishwa na sasa itadhoofishwa zaidi kwenye chaguzi hizi. Better late than never nashauri tujitoe kwenye hizi chaguzi na Dunia ituelewe hivyo. Ni heri kukosa RUZUKU ya uchaguzi na RUZUKU ya chama kuliko kuipokea mara moja na kushiriki huu unajisi wa demokrasia.
 
Nashauri sio upinzani wajitoe tu bali wafute vyama kabisa... Maana haiwezekani msusie uchaguzi halafu waendelee kupata ruzuku...
 
Safi Sana !kiapo kinakubalika kisheria, haohao wakurugenzi mbona waliwapekeka wapinzani bungeni Sasa hivi iwe nongwa kwa nini! Acheni deko upinzani tafteni agenda zenye maana wananchi wawaelewe zaidi ya hapo chaguzi zote mtakuwa watu wa kulialia kila siku
Huko nyuma wakurugenzi na watumishi wengine wa uma hawakuwahi kujihusisha moja kwa moja kwenye kutafuta vyeo vya kisiasa (walikuwa hawana makundi ya wazi au mitandao ya kisiasa ndani ya chama chochote).
Wengi wao siasa hivi ni wale makada waliotamani vyeo vya kisiasa wakashindwa.
Hivyo kwa mustakabali mwema wa taifa, watu walioonesha au wenye tamaa ya vyeo vya kisiasa hawafai kuwa waamuzi kwenye uchaguzi.
Ni muhimu haki itendeke na pia ionekane imetendeka kimchakato wa wazi na huru.
Nafikiri mahakama hapa imepitiwa ikaamua bila kuzingatia hali halisi.
 
Back
Top Bottom