SERIKALI YASHINDA RUFAA YA KUPINGA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI
Mahakama ya Rufani imetengua hukumu na amri ya Mahakama Kuu kuzuia wakurugenzi wa halmashauri, manispaa, na majiji kusimamia uchaguzi mkuu kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwa maana hiyo Wakurugenzi wanaruhusiwa na wataendelea kusimamia uchaguzi.
> Mahakama ya rufaa imetoa uamuzi huo baada ya kujiridhisha na hoja za Serikali kuwa Wakurugenzi hao kabla ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi hula viapo vya kukana uanachama wao
> Kesi hiyo ilifunguliwa na Bob Wangwe akisimamiwa na Wakili Msomi Fatma Karume.
__________
Haya wahini mkajiandikishe kupiga Kura na muhawi foleni za kupiga Kura juani na kwenye mvua November 24, 2019 na October 25, 2020 ila mjue kazi yenu ni kupiga Kura tu ila wakubwa ndio wataamua nani awe Kiongozi. Period. Bado kuna mtu anajifariji kuwa Katiba Mpya na Tume HURU ya Uchaguzi sio muhimu sana katika kuamua mustakabali wa Taifa hili?
Mark my words kama upinzani utakubali kushiriki uchaguzi huu wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020 Wabunge wa Upinzani watakaorejea bungeni hawatozidi 10. Upinzani umedhoofishwa na sasa itadhoofishwa zaidi kwenye chaguzi hizi. Better late than never nashauri tujitoe kwenye hizi chaguzi na Dunia ituelewe hivyo. Ni heri kukosa RUZUKU ya uchaguzi na RUZUKU ya chama kuliko kuipokea mara moja na kushiriki huu unajisi wa demokrasia.